Asante 2022, nilipata mil. 4.5 kimasihara

Every action there is equal and opposite to the reaction ...
Niliuziwa mabati ya wizi kwa bei ya mteremko

Baadae wizi ukagundulika wakakamatwa watu kibao waliokuwa wanahusika kwenye huo mradi wa serikali,wengi wao wakiwa wamewaonea tu maana walikamata mpaka wasomba maji na mlinzi ambae walikuwa hawajamlipa hata mshahara toka aanze kuwa hapo

Nikaogopwa kutajwa au kufanya upekuzi nyumbani kwangu,nikaamua niyakimbize mabati mbali ninapoishi kwenye nyumba nyingine umbali kama km 30 niliyasafirisha usiku sana

Ile narudi baada ya kuyafikisha salama,nikapata ajari nilimgonga boda boda,hela iliyonitoka ni nyingi mno kuna wakati hadi nawaza ni zile laana za wale lala hoi waliobambikiziwa kesi maana walitoa hela kutoka polisi hawakuachiwa hv hv
 
Je umeiingiza kwenye biashara ili ikusaidie zaidi? Nina shaka na jibu utakalotoa.
 
Kuna boss wangu mmoja anaweza akakutumia pesa na asikupigie hata wiki ndio akakuambia hiyo pesa ni ya matumizi fulani alafu ana tabia ya kutuma pesa nyingi sana,

sasa nafikiria tu mimi ningekuwa kama wewe sijui ingekuaje!! By the way , karma haiongopi! Hiyo ni jasho ya mtu na utaitapika kwa njia yeyote ilee yaani utalipa gharama tu Na usisahau kutupa mrejesho yakisha kurudia.
 
Hahahaaa Kuna jamaa yangu alikuwa mwalimu shule za serikali, baadaye akasomea Mambo ya maabara akapata kazi za halmashauri moja hivi lkn ni serikalini. Akawa anapata mishahara miwili kwa mwaka mzima. Unajua nn kilimtokea? Ilijulikana wakamsimamishia mshahara kwa miaka 3 alafu ana mke na watoto, nusu awe chizi *****
 
Kama nakuona vile ulivokua unakimbiza mabati[emoji23]
 
Kama hiyo laini imesajiliwa NIDA watakukama tu, utake usitake. Ili usikamatwe labda uhame nchi!!
 
Dah nisemeje Mimi niliwahi kupata hela kwa staili hiyo haikua kubwa lakini ilikuja kuniletea matatizo Sana ilikua hivi.

Siku hiyo nilikua nimekaa na njaa kwa masaa 42 bila kula chochote njaa imetamalaki na msaada nilikosa kabisa mpaka leo najiuliza ilikuaje nilikosa hata 500 na hakuna hata mtu aliyenisave hadi home..hii ilitokana na Mimi kulazimisha kuhama nyumbani na kwenda kupanga pasipo ridhaa za wazee.

Basi bwana nikiwa nimejilaza napiga hesabu nimgongee mpangaji mwenzangu na hapo ndo kwanza Nina wiki mbili kwenye hiyo nyumba ,akaja rafiki yangu na yeye choka mbaya tukawa tunapiga stori na yeye alikuja kunililia njaa tangu Jana yake hakula...Mara pa mlio wa sms kwenye laini ya tigo kucheki ni elfu 30 moyo ukafanya paah bila kuchelewa nikaenda kuitoa ile hela nikapata elfu 28.

Hao Cha kwanza mgahawani ita menyu gonga pale sahani mbili kila mtu Mara simu ikaita napokea ni mdada akaomba arudishiwe hela japo elfu 20 tu maana alikua anamtumia kaka yake atoe ili apate elfu 20 ya matibabu ya kijana wake na iliyobaki apate rizki ya chakula...dah kwa ukaidi nikagoma sijaona hela ,aliniomba Sana nikamwambia sijaona hela Basi akaniambia neno moja "Kama hiyo rizki ni yako halali Basi Mungu atakuacha Ila Kama sio ya halali utapoteza vingi na utajutia kwa dhulma yako" nikakata simu nikamblock(blacklist).Ila hakukoma alitumia namba nyingine alinisumbua siku nzima nikaamua kutoa laini.

Sijui Kama ilihusiana na lile tukio lakini miezi 11 baadae nikapata pesa za kutosha kwangu(kiuanafunzi) Ila zilipotea vibaya nilipata uchungu balaa.ikabdi nikatoe sadaka ile 30 kwa nia kua namlipa Yule dada niliichenji na kugawa kwa wale omba omba kila niliyemkuta mpaka ikaisha ile siku yote,maana sikua na namna ya kumpata.

Now Sina shida ila fikra zangu naamini nililipia ile hela kwa njia nyingine ndo nikawa salama.

NB😀hulma haifai wazee
 
Hiyo pesa utakuja kuilipa ,either wewe mwenyewe ,au watoto wako ....


Every action there is equal and opposite to the reaction ...
Sio kweli,Kuna vitu sometimes huwa Ni neema tu...mi niliwahi pata pesa toka kwa wakaka na sijawahi kupigiwa
 
Hahahahahaha
 
Munadanganyana sana mara sijui karma mara hivi,hebu niwaambie kitu kimoja acheni imani za kijinga mimi ukikosea muamala kuanzia laki 2 sikurudishii hata iweje nakumbuka kuna demu mmoja wa kichaga alikosea hela akatuma kwangu laki 5 aisee nilikodi bodaboda mpakka town kwenda kuipakua hela yangu ya bure yule dada alipiga simu sana ananiomba nimrudishie nikawa namuambia niko barabarani dada nikifika hom tu nakurudishia kumbe nipo barabarani kwenda kwa wakala na mpaka leo hakuna cha karma wala nini
 
usijisifie dhulma mkuu, yajayo yanafurahisha
 
Hizo namba zilizotumika kwenye miamala si zimesajiliwa kwa majina yako na ulitumia kitambulisho, basi kaa kwa kutulia hakuna ujanja wowote uliofanya hapo utanaswa kiulaini kama kuku bandani.....
 
Aisee sasa nifanyeje na nilishaitumia na sijawahi pigiwa na mtu kwamba kakosea kutuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…