Sakata la bandari ya Bagamoyo kuuzwa kwa Waarabu latua Bungeni. Prof. Kitila asema Serikali haijaingia makubaliano yoyote ya uwekezaji

Sakata la bandari ya Bagamoyo kuuzwa kwa Waarabu latua Bungeni. Prof. Kitila asema Serikali haijaingia makubaliano yoyote ya uwekezaji

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ajibu sakata la Bandari ya Bagamoyo. Asema Serikali haijaingia makubaliano yoyote ya uwekezaji

1739533343843.png
Soma: Ubalozi Wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Watoa Maelezo ya Kina juu ya Upotoshaji unaoendelea Mitandaoni

"Serikali ipo katika hatua mbalimbali za kutekeleza program ya ujenzi wa eneo maalum la kiuchumi la eneo la Bagamoyo na hili ni moja ya miradi 17 ya kielelezo iliyopo katika mpango wa tatu wa maendeleo ya miaka mitano 2021/22-2025/26"

"Pamoja na mambo mengine eneo hili linahusisha ujenzi wa miradi mingi lakini moja ni ujenzi wa Bandari, Kongani za Viwanda, Kongani za TEHAMA, Ukanda huru wa biashara na kituo cha Reli. Kwahiyo sio mradi mmoja na ndio maana tunaita program"

"Utekelezaji wa program hii utatekelezwa na sekta binafsi kwakushirikiana na serikali kupitia mpango wa ubia katika sekta binafsi na sekta ya umma yaani Public–private partnership (PPP)"

"Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje wameonyesha nia ya kuwekeza, wadau hawa wako katika hatua mbalimbali za mazungumza na taasisi husika. Serikali haijaingia makubaliano yoyote na mwekezaji yoyote kwasasa, wala hatuna mkataba na mwekezaji yoyote katika miradi ya Bagamoyo ikiwemo niliyoitaja wa Bandari"


Soma: Tetesi: - Saudi Arabia yapewa haki ya umiliki na uendeshaji wa bandari ya Bagamoyo kama sehemu ya mradi wa East Gate

========================================================

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UENDELEZAJI WA ENEO MAALUM LA KIUCHUMI LA BAGAMOYO (BAGAMOYO SPECIAL ECONOMIC ZONE-BSEZ)
GjvS1ifXQAEw_4c (1).jpg

GjvS1ibWIAA6svM (1).jpg
 

Attachments

  • GjvS1ibWIAA6svM.jpg
    GjvS1ibWIAA6svM.jpg
    22.8 KB · Views: 2
14 February 2025
Bungeni, Dodoma
Tanzania

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Mussa Azzan Zungu leo asubuhi katika kikao cha bunge linaloendelea mjini Dodoma amemtaka waziri Prof. Kitila Mkumbo kuelezea kuhusu sakata la Bandari ya Bagamoyo kudaiwa kuuzwa / kupewa mwekezaji

Madai Bandari ya Bagamoyo Kuuzwa Kwa Mwekezaji wa Saud Arabia Serikali Yatoa Neno, "Sio Kweli"​



View: https://m.youtube.com/watch?v=44XGR6QbatI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Kitila Mkumbo ametoa taarifa ya Serikali kufuatia kuenea kwa habari katika vyombo vingi kwa media hapa nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote

Ni juu ya eneo maalum la kiuchumi la Bagamoyo linalohusu bandari kuwa limeuzwa kwa Mwekezaji kutoka Falme za Kiarabu.
1739543080674.jpeg

Mpango wa Maendeleo Eneo Maalum la
1. Ipo katika ujenzi wa eneo la uwekezaji maalum
2. Inahusisha ujenzi wa miradi mingi ikiwemo bandari, reli
3. Utafanywa na sekta binafsi na umma PPP
4. Wadau wengi wameonesha nia ktk programu hii kama ni reli wanazungumza
5. Serikali haijaingia mkataba na mwekezaji yoyote
6. Hivyo taarifa kuwa kampuni ya SADC kutoka Saudi Arabia siyo kweli
7. Umma utajulishwa kikamilifu programu hiyo itapoanza

1739528307350.jpeg
 
Muda huwa haudanganyi taratibu mambo yataanza kuwa wazi
 
Hata taarifa za DP world zilikuwa si za kweli...

Ila ni muhim uwekezaji ukafanywa kwa manufaa ya nchi
 
Mtoa mada hizo ni sinema za CCM bungeni hapo kilakitu wameshapanga Huko kwenye party caucus
 
14 February 2025
National Parliament, Dodoma
Tanzania

That the port of Bagamoyo will be sold to a Saudi Arabian investor, the government of Tanzania says, "It is not true"


View: https://m.youtube.com/watch?v=44XGR6QbatI

The Deputy Speaker of the Parliament of the United Republic of Tanzania, the honorable Mussa Azzan Zungu, this morning in the ongoing parliamentary session in Dodoma, has asked the minister Prof. Kitila Mkumbo to explain about the Bagamoyo Port saga allegedly sold / given to an investor from Saudia Arabia

Prof. Kitila Mkumbo the minister in charge on Investment has said Allegation that the port of Bagamoyo will be sold to a Saudi Arabian investor, the government says, "It is not true"

The Minister of State, Office of the President, Professor Kitila Mkumbo has issued a government statement following the spread of news in many media outlets here in Tanzania and around the world, that a Saudi Corporation has strike and finished a deal for acquisition of the Bagamoyo port.

The minister further went to clarify that the Bagamoyo port is part of a bigger programme on its initial stage, which will include construction of a rail network, industries and a modern port, so with that honourable members of this Parliament you can see we (the government) have not reached a stage for shortlisting companies that have shown interest in building a railway line to Bagamoyo, roads not to mentioned for the acquisition of Bagamoyo port.

1739528322783.jpeg

Photo : The Saudi Chambers of Commerce delegation in Tanzania, that met with the Tanzanian officials for talks on investment opportunities.
 
Mimi sidanganyiki na hizo drama za linaloitwa bunge wakati ni kikao cha CCM.

Wamepangana hapo kuwahadaa kwamba kuna wapinzani wa uuzwaji bandari kumbe washabeba mgao wa 10%

Mkija kufumbua macho mkataba ulishasainiwa na vifungu vya kuuvunja ni hasara kwa nchi.
 
1739528924975.jpeg

Prof. Kitila Mkumbo akitolea ufafanuzi wa bandari ya Bagamoyo


More info :


13 February 2025

Riyadh, Saudi Arabia

Ufalme wa Saudia wananunua Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania, bandari hii ni lango na kitovu muhimu zaidi cha usafirishaji katika Afrika Mashariki​



Kingdom inanunua Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania, lango muhimu zaidi la usafirishaji katika Afrika Mashariki
Mkurugenzi mkuu wa Bandari akibadil8shana makabrasha na kiongozi wa ujumbe wa Saudia mbele ya camera

Imeandikwa na Ahmed Hamad

Februari 12, 2025


Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Saudia, Hassan bin Mujib Al-Huwazizi ( Hassan Alhwaizy) , alifichua kuwa mamlaka husika ya Tanzania imetoa haki ya upataji na ununuzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania kwa Kampuni ya Uwekezaji na Maendeleo ya Saudia (SADC) kama sehemu ya mradi ambao kampuni hiyo imeuita “East Gateway Project”, akimaanisha ukanda wa Afrika Mashariki.


Al-Huwazizi ( Hassan Alhwaizy) alisema kuwa hatua hii itaunga mkono jukumu la Ufalme kama kichocheo kikuu cha maendeleo ya kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, na jitihada zake za kupanua uwekezaji wa kigeni, hasa katika bara la Afrika, pamoja na kuboresha uwezo wake wa vifaa ili kufikisha mauzo ya Saudi katika masoko ya kimataifa.


Hayo yamejiri wakati wa Jukwaa la Biashara la Saudia na Tanzania, kwa kuungwa mkono na Shirikisho la Vyama vya Saudia linalotembelea Tanzania ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kufungua masoko mapya katika bara la Afrika, katika hatua ya kimkakati yenye ubora wa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Ufalme na Zanzibar, na kufungua upeo mpya wa uwekezaji wa Saudia katika eneo hilo

Ununuzi wa kampuni ya SADC wa Bandari ya Bagamoyo unawakilisha mabadiliko ya ubora katika maendeleo ya miundombinu ya baharini na vifaa katika Afrika Mashariki, kupitia utaalamu mkubwa wa Saudia katika eneo hili, ambayo itaongeza nafasi ya kanda kama kitovu cha biashara ya kimataifa, na kufungua upeo mpana kwa uwekezaji wa Saudi katika sekta muhimu kama vile nishati, madini, biashara, vifaa, viwanda vya nishati na nishati.

Inatarajiwa kwamba ununuzi wa Saudia wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania utachangia katika juhudi za Ufalme wa kuinua uchumi wake, kuunda vituo vipya vya uwekezaji na uuzaji, kuchangia mauzo ya bidhaa za Saudia kwenye masoko ya Afrika, na kuchochea harakati katika bandari za Ufalme huo.

Bandari ya Bagamoyo ina umuhimu mkubwa kwa Ufalme wa Saudia, kwani ndiyo lango kuu la usafirishaji katika Afrika Mashariki, itahudumia Tanzania na nchi jirani, na itakuwa bandari kuu ya kusafirisha malighafi na maliasili za Afrika kwa nchi mbalimbali duniani au kuagiza bidhaa katika nchi za Afrika.
 
Back
Top Bottom