Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amekanusha taarifa zilizozagaa mtandaoni kuwa serikali imeingia mkataba na kampuni mojawapo ya Saudi Arabia, kuwekeza eneo maalum la uchumi la Bagamoyo ikiwemo Bandari.
Profesa Kitila Mkumbo ametoa ufafanuzi huo leo, Ijumaa 14 Februari katika Bunge la 12, Mkutano wa 18, Kikao cha kumi na nne, baada ya Naibu Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka atoe tamko kuhusiana na habari hizo zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na uwekezaji Bandari ya Bagamoyo.
“Mheshimiwa Waziri kabla ya yote toa tamko kuhusiana na habari zilizosagaa mtandaoni kuhusiana na no maalum la uchumi ikiwemo Bandari ya Bagamoyo” alisema Naibu Spika Zungu.
Profesa Kitila alianza kwa kueleza vipengere sita ambavyo ni lazima vifuatwe ili kukamilisha uwekezaji na kubainisha kuwa taarifa zinazosambazwa hazina ukweli wowote.
“Hatuna makubaliano wala mkataba wa eneo hilo maalum la kiuchumi na kampuni yoyote na taarifa kuwa tumeingia mkataba na kampuni ya Saud Arabia eneo la Uchumi la Bagamoyo hayana ukweli” alisema.
Bunge limeahirishwa hadi 8 Aprili mwaka huu 2025 na litadumu hadi 25 Juni 2025 litakapohutubiwa na kuvunjwa rasmi na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.