Asante Lissu amesababisha ajira za walimu kutangazwa, hotuba ya bajeti ya Waziri hapakuwa na hilo

Asante Lissu amesababisha ajira za walimu kutangazwa, hotuba ya bajeti ya Waziri hapakuwa na hilo

mumburya

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2012
Posts
321
Reaction score
448
Ni mtu mpuuzi tu anayeweza kumdharau mtu kama Tundu Lissu. Lissu kasema Serikali haijaaijiri walimu tangu 2014, hapo hapo serikali inaitupa bajeti ya Ndalichako na kaika hali ya kupaniki inatangaza kufungua dirisha la kuajiri walimu kwa maelfu. Katika hotuba ya waziri wa elimu, yeye aliahidi ajira hizi hapa:

1. Kuajiri watumishi wa Mamlaka ya VETA ili kuziba nafasi zilizo wazi; (Uk.77.)
2. Kuajiri jumla ya wafanyakazi 164 kati yao wanataaluma ni 45 na waendeshaji ni 119; katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (uk 86).

Hotuba nzima sioni ajira za walimu wa Shule za Msingi wala Sekondari. Hotuba ya bajeti nimeiambatanisha hapa.

KAMA SI CHANGA LA MACHO, BASI HII NI KALI YA KARNE, TUNDU LISSU KAIFUMUA BAJETI YA SERIKALI. Kifupi ni kwamba TUNDU LISSU ameanza kuwatumikia Watanzania. WANAOEMA VYAMA VYA UPINZANI VIFE HAWAJUI WANACHOSEMA.
 

Attachments

Huu ni mlungula NEC na TAKUKURU wachukuwe hatua stahiki bila kusahau matumizi ya "Kisukuma" kwenye kampeni ambayo ni kinyume cha sheria na taratibu za uchaguzi.
 
Mkuu ambaye amejaribu kutuma maombi naomba ajitokeze atupe ushuhuda hususani kutokea kwenye mikowa ya kanda ya ziwa
 
kwa lugha nyingine jiwe ameanza kutoa rushwa, hayo ni mambo aliyotakiwa kuyafanya kitambo. wananchi wapokee lakini wasimpe kura.
Unaweza kuona kama ni rushwa lakini matatizo makubwa yapo kwenye katiba ya nchi. Haijaweka usawa wa wagonbea uraisi wakati wa kampeni. Magufuli bado ni rais na atakoma kuwa rais baada ya kuapishwa raisi mwingine atakayekuwa ameshinda uchaguzi. Kama atashinda ataendelea kuwa rais.

Sasa tunaona yuko kwenye kampeni ya kuomba urais lakini katiba inampa mamlaka ya kazi zote za rais. Ndiyo maana anafanya hayo anayofanya sasa hivi. Anakosolewa upande wa pili, hapo hapo anapata nafasi ya kufanyia kazi yale aliyokosolewa na mgombea mwenzake wa urais.

Tukubali tu kwamba mpaka pale tutakapopata katiba itakayoweka usawa wakati wa kugombea nafasi ya rais wa nchi, ndiyo mambo kama haya yatakoma. Anachofanya Magufuli sasa hivi siyo rushwa, anayo mamlaka kikatiba. Anaweza kuteua, kutengua na kufanya chochote kile kilicho chini ya mamlaka yake kama rais.
 
Hadi October mashehe wataachiwa kwa moto huu anaopelekewa meko.
 
Back
Top Bottom