Simba wangejiuliza Man U anapata kiasi gani kwenye TV, na Simba wanapata kiasi gani kwenye TV.
Jibu ni USD 630 million kwa mwaka 2020.
Mkataba wa Azam Tv na Bodi ya Ligi ni USD 10 million kwa miaka 5; yaani USD 2 million kwa mwaka kwa timu zote za ligi.
Simba hapo sanasana anapata 200mil. ambayo ni kama USD 100,000/- kwa mwaka. Na mkataba unaishia mwaka huu.
Swali ni kwanini Dewji hazungumzii Azam TV anazungumzia Sportspesa?
Jibu:
Katika utafiti wowote wa mapato ya michezo, TV hutumika kama chombo cha kupima population assignment.
Watafiti hutumia Average TV viewership (Broadcasting) na mahudhurio (Match day) kama "n". Pia kampuni za matangazo hutumia hii ku- bargain bei ya TV commercial.
Hata kit sponsorship huwa haisemwi tu kutoka kichwani. Mnakaa mezani na wewe kama mwenye timu unatoa takwimu zako za Match day viewership (average) kwenye TV na Uwanjani.
Data za Matchday hasa kwenye TV za Tanzania si rahisi kuzipata, kwa hiyo kubargain kwa kutumia hii njia, si rahisi. Ingawa data za uwanjani zipo ila ni ndogo sana na huwa affected na mambo mengi.
Njia ya pili ni mauzo ya merchandise. Yaani jezi, bilauri, key holders etc ...
Hii pia ni njia mojawapo ya kuwaambia sponsors kwamba, angalia mimi nauza kiasi hiki kwa mwaka. Ukiweka matangazo yako utakuwa na uhakika wa kuongeza mapato kwa sababu mimi navutia macho mengi ambayo inamaanisha mifuko mingi. Hii method ni ya uhakika na pia ni rahisi kupata Data zake hapa Tanzania.
Manchester walipata Mauzo ya USD 275 milion; Je Simba walipata mauzo ya USD milioni ngapi? Wakiweza kufananisha hii, basi hiyo proportion waitumie pia kubargain na SportsPesa.
Siyo kuongea tu.