MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Habari wakuu,
Natumaini kila mmoja anaendelea vyema. Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni. Pia nina uhakika wa uhuru baada ya kutoa maoni kwa sababu huu uzi haugusi mamlaka za kidola bali viongozi wachache wanaopotosha umma.
Jana nilitazama video iliyokuwa ikimuonyesha Mh Eric Shigongo akitishia kuchomoa shilingi kwenye bajeti ya wizara ya elimu kwa hoja zilizokosa weledi. Kabla ya kuangalia hoja ya huyu mbunge tujikumbushe kwamba siku za karibuni huko bungeni kumezuka utata wa baadhi ya bunge kudai kwamba wasomi sio lolote bora walioishia darasa la saba. Hoja imetokana na wao kupata mafanikio makubwa kiuchumi na kisiasa bila kwenda shule. Ni mambo ya kushangaza sana.
Mh Shigongo ni mtu ambaye hakubahatika kupata elimu ya sekondari. Aliishia darasa la saba na kupata elimu kwenye mambo ya afya ambapo pia upataji wa hiyo nafasi ya chuo pia ilikuwa ni kama bahati. Mwenyewe mara zote amekuwa akisema umaskini ndo ulisababisha iwe hivyo kwa upande wake. Baada ya mapambano mengi sana maishani hatimaye Ndugu Shigongo akapata nafasi ya kusomea shahada ya kwanza Chuo Kikuu kupitia nafasi za watu walioshia darasa la saba ila hawakupata elimu ya sekondari. Kigezo kikuu cha nafasi hizi ni uwe umefanya vitu vikubwa vya kipekee kwenye jamii na una nia ya kuongeza elimu.
Ni utaratibu uliokuwa na baraka za tume ya vyuo vikuu (TCU). Jamaa alisomea TUDARCO. Sio vyuo vyote vilifanya huu utaratibu. Kwa mujibu wa Waziri wa elimu ni kwamba seneti za vyuo haziingiliwi kwenye kuweka vigezo vya kujiunga vyuoni ili mradi hawavunji kanuni za TCU na wizara. Tatizo la Shigongo kwa mujibu wa maelezo yake ni baada ya UDSM kumtaka aambatanishe cheti cha kidato cha nne wakati akiomba nafasi ya kusoma Masters. Hili jambo lilimkera Shigongo hadi kutaka kuchomoa shilingi kwa hoja kwamba TZ inakiuka taratibu zinazotumika nchi nyingi za kutambua vipaji na mambo makubwa yaliyofanywa na baadhi yetu ila bahati mbaya huko nyuma hawakubahatika kupata kusoma sekondari.
Mh Waziri wa elimu kwenye majibu yake kwanza alisema UDSM haiingiliwi kwenye taratibu zake. Pia huo utaratibu uliomwezesha Shigongo kupata nafasi ya kusoma Chuo Kikuu ulisitishwa baada ya kutokea janja janja nyingi. Na pia kwa sababu wabunge wengi ambao hawajasoma wamekuwa wakidai vyeti vya elimu ni makaratasi tu kwanini walilie tena kwenda chuo? Si bora wabaki kwenye ujuaji wao kuliko kulilia kitu walichosema hakina maana?
Binafsi nampongeza Mama Ndalichako kwa kutoa majibu mafupi yaliyojaa points tupu. Huo utaratibu uliotumika kumpatia shahada Mr Shigongo ni mzuri lakini kutokana na janja janja ya sisi wenyewe basi ni utaratibu hatari usio salama. Nchi yetu haina rekodi nyingi zinazowahusu wananchi mmojammoja kiasi kwamba ni ngumu kupata uhalali wa mafanikio tunaowaona nayo wengi. Utakuta mtu anaonekana genius kwenye biashara kumbe nyuma ya pazia kuna haramu za kutosha. Ushauri wangu ni hawa watu waliopata mafanikio kama wanataka vyeti waende kwenye hizi centres za mitihani ya QT ili wapate vyeti kihalali na wajue kabisa elimu haina mbadala. Bila wasomi wa kutosha ni ngumu nchi kusonga mbele. Kama mtu hana elimu na hataki kukaa darasani basi abakie tu na hela zake hakuna haja ya kusumbuana. MWISHO kabisa kuna haja ya KATIBA kubadilishwa ili kutoingiza vilaza bungeni.