Asante Profesa Ndalichako kwa majibu yako kwa Erick Shigongo

Asante Profesa Ndalichako kwa majibu yako kwa Erick Shigongo

Kwani vitu vikubwa alivofanya Shigongo kwenye jamii ni vipi?...kuuza magazeti na kuandika vitabu ndo vitu vikubwa?
 
Ifike wakati,elimu iheshimiwe.Hatuwezi kama taifa kuwapongeza watu kama akina Musukuma kwa kejeli zao juu ya elimu.Elimu haichezewi kokote duniani.Wana hela ndio,lakini isiwe sababu ya wao kukejeli elimu na kuuona uprofesa hauna maana.
Hawana lolote, wangekuwa na hela na wanakazi za kufanya wasingeangaika na viposho vya laki 2 kutwa,wako bungeni kwa lengo la kuendeleza haramu zao.
 
Na huyo Kishimba na yeye baada kuwatetea Wananchi wake amekalia ku challenge wasomi. Kisa kapata pesa.
Watu wanapaswa watofautishe Utajiri na Elimu. Huwezi kutukana wasomi wakati hicho kipaza sauti unachotumia bungeni kimevumbuliwa na wasomi. Kazi ya msomi ni kutatua changamato za jamii. Utajiri ni matokeo tu.
Wavumbuzi wengi hawakuwahi kwenda shule za maana.
 
Tanzania wenye elimu wamesoma ila hawajaelimika ndio issue kubwa inayosumbua Taifa so wote wanaonekana sawa... na waliosoma hawana la kusaidia Taifa zaidi ya blah blah tu na wizi na upendeleo na majivuno fake
Very true
 
Tatizo ni kubwa zaidi hilo la darasa la 7 kusoma chuo! Mfumo wetu wa elimu, unazuia watu kuwa wabunifu! Hao wabunge ‘mkumbaro’ wanapoponda wasomi, kuna wakati wanakuwa sahihi! Kuna wasomi ambao wamepita madarasa, wamekariri tu, lakini hawajaelimika! Pia kuna ma-PHD na masters fake kibao!
Safi
 
Hatuwezi kuwakataa hivi hivi. Lazima kwanza yafanyike mabadiliko kuhusu sifa za kugombea Ubunge. Hilo la kujua kusoma na kuandika ama Kiwashili ama Kiingereza lisiwe kigezo muhimu katika kugombea Ubunge. Sifa nyingine ziongezwe ili kukidhi mahitaji ya dunia ya sasa na mazingira yaliyopo sasa.
Je hao wasomi Wana mchango gani WA maana bungeni , if that case
 
Heeeeh mbna sikua najua hili, kua std 7 anasoma Degree bila o level wala advance level, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Udsm haiingiliwi kwenye taratibu zake? huyu mama vipi.. mwaka jana kuna viongozi wa Daruso walisimamishwa masomo kwa maelekezo ya Ndalichako. Mwaka 2016 kuna vijana wao wa DUCE walimpa kipigo cha mbwa koko bwana mdogo huko Mbeya wakafukuzwa kwa maelekezo ya serikali.
 
Kwanza chuo chenyewe anachokitaka kinachukua vipanga tupu. Enzi zetu hadi div III ya mwanzo walikuwa wanachukua COET... Ila kwa sasa watoto wanapelekeana moto kiasi kwamba div II ni mbinde kupata nafasi. Shigongo akajiunge hata na chuo cha nyuki tabora au chuo cha ufundi stadi VETA Oljoro campus.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kule jimbo la Geita vijijini kwa Musukuma sijui kama wananchi Walichagua mbunge wa kwenda bungeni kubeza wasomi au shida za wananchi wa jimbo lake ni wasomi wa nchi hii.Ameacha kuzungumzia shida za wananchi wa jimbo lake kila akisimama yeye na maprofessor wa nchi hii.
Au inawezekana jimboni kwake wananchi
wanahudama safi za maji na salama, madawati na madarasa yanatosha na barabara nzuri jimbo zima na huduma za afya bora.Walio wahi fika huko mtujuze.
 
Udsm haiingiliwi kwenye taratibu zake? huyu mama vipi.. mwaka jana kuna viongozi wa Daruso walisimamishwa masomo kwa maelekezo ya Ndalichako. Mwaka 2016 kuna vijana wao wa DUCE walimpa kipigo cha mbwa koko bwana mdogo huko Mbeya wakafukuzwa kwa maelekezo ya serikali.
Hayo matukio uliyo yaainisha yanahusiana vipi na shigongo kutaka kupewa Masters ya buree? Wee vipi khaaaah
 
Hayo matukio uliyo yaainisha yanahusiana vipi na shigongo kutaka kupewa Masters ya buree? Wee vipi khaaaah
Hujasoma ukaelewa! wanasema UDSM Haiingiliwi kwenye taratibu zake, vp mbona kipindi cha jiwe imeyumbishwa mpaka ikawa utopolo.
 
Ujinga wake aupeleke huko huko Open. Nawapongeza UDSM. Jitu halijui hata Quadratic Equation linataka kufanya Masters.
Litawezaje ku analyze Data kama sio kununua watu walifanyie. Hata hivyo ku defend lingeshindwa tu
Kwani kila kitu sini pesa sikuhizi! Mtapiga sana porojo ila kati ya hard paper unayopewa baada ya kuspend million 7 kwa miaka mitatu na kumiliki billion 3 benki kipi ni bora?
 
Ujinga wake aupeleke huko huko Open. Nawapongeza UDSM. Jitu halijui hata Quadratic Equation linataka kufanya Masters.
Litawezaje ku analyze Data kama sio kununua watu walifanyie. Hata hivyo ku defend lingeshindwa tu
Hivi tangu usome quadratic equation na log umesha apply kwenye kazi au maisha?
Nimejifunza hvi vitu ila sijaa apply kwenye life mpk leo
 
Elimu bila pesa ni ujinga tu, kuelimika ni uwezo wa kugeuza Elimu kuwa pesa kama hilo haliwezekani basi hata ukiwa na elimu unaonekana Mburula tu!
 
hii lugha Yao ntachomoa shilling ni upuuzi first class. Uchomoe shilling my A$$. Wakati tunaona bugdets zinapitishwa tu na shilling zenu mlizochomoa mkaweka matracoin mwenyu. Shen,¥ typ
Matra-coin
 
Hujasoma ukaelewa! wanasema UDSM Haiingiliwi kwenye taratibu zake, vp mbona kipindi cha jiwe imeyumbishwa mpaka ikawa utopolo.
Kuna mambo baadhi inaweza kuingiliwa, ila sio hili la shigongo khaaaah
 
Si bora wabaki kwenye ujuaji wao kuliko kulilia kitu walichosema hakina maana?
Maelezo mazuri halafu katikati umejaribu kwa kumshambulia mtu binafsi badala ya hoja
Hoja imetolewa na shigongo,we unashambulia wengine ambao wameponda vyeti
 
hii lugha Yao ntachomoa shilling ni upuuzi first class. Uchomoe shilling my A$$. Wakati tunaona bugdets zinapitishwa tu na shilling zenu mlizochomoa mkaweka matracoin mwenyu. Shen,¥ typ

Ukifuatilia kwa umakini ktk vikao vya Bunge vilivyopita hawa watu type ya shigongo hawakuwa viherehere wa kuongea ujingajinga kama huu wa kutoa shillingi kwenye bajeti bali hii imekuja kwa fujo sasa hivi baada ya watu wasio na elimu kuingia Bungeni kwa mgongo wa kidicteta, ajabu kabisa haowaoni aibu kusema eti waliosoma hawana tofauti na wao kisa wana vijisenti vya ujanjaujanja vilivyowasaidia kuingia Bungeni na kuanza kuonyesha ujinga wao ktk jamii,

Ningependa wizara ya elimu hivi sasa ingefanya uhakiki wa vyeti vyote vilivyotolewa kiujanjajanja kutoka vyuo visivyoeleweka itoe msimamo kuwa havitambuliki na walionavyo wakafungie maandazi kwani huwezi toka darasa la saba ukaenda varsity na ukapata degree hata kama umeenda kusomea kiswahili haiwezekani
 
Hoja ha
Elimu bila pesa ni ujinga tu, kuelimika ni uwezo wa kugeuza Elimu kuwa pesa kama hilo haliwezekani basi hata ukiwa na elimu unaonekana Mburula tu!
Hoja hapa ni moja Mkuu yeye amechaguliwa na wananchi wa jimbo lake kwenda bungeni kuwasemea shida, kutetea masrahi ya wana Geita vijijini na kero mbalimbali za Geita vijijini ili zifike serikalini wala hakuchaguliwa kwa lengo la kuponda wasomi wa nchi hii. Ikiwa wasomi hasa maprofessor wa nchi hii ni moja ya kero jimboni kwake basi yuko sawa.
 
Back
Top Bottom