Asante Profesa Ndalichako kwa majibu yako kwa Erick Shigongo

Asante Profesa Ndalichako kwa majibu yako kwa Erick Shigongo

Musukuma, Shigongo, Lusinde na Kishimba hawana hata hadhi ya kuwa wafagiaji wa barabara za vumbi. Ujambazi Uzandiki na pengine kupora haki za wengine kuishi ndio zimewafikisha hapo wala sio akili. Ndakichako wambie hao wabakie na ujuaji wao
... hilo eneo linaonekana lina ushirikina balaa! Watu kama hawa walipenyaje wakati wasomi wapo?
 
Hivi

Hivi ni kweli, kwamba kuna kipindi serikali ilibadili vigezo vya kuingia na kusoma vyuo vikuu,na kuruhusu darasa la saba?? Kama ni hivyo sishangai ndo maana siku hizi tuna wasomi wengine hata wakijadili issues, wanakuwa hawana tofauti sana na wakati mwingine afadhali na darasa la 7.... kazi iendelee.
Tatizo ni kubwa zaidi hilo la darasa la 7 kusoma chuo! Mfumo wetu wa elimu, unazuia watu kuwa wabunifu! Hao wabunge ‘mkumbaro’ wanapoponda wasomi, kuna wakati wanakuwa sahihi! Kuna wasomi ambao wamepita madarasa, wamekariri tu, lakini hawajaelimika! Pia kuna ma-PHD na masters fake kibao!
 
Hao darasa LA Saba mna takiwa muwakatae kwa ninyi wenye digree na masters sijuh kutumia hizo nafasi za kugombea huo uwakilishi. Vinginevyo acheni chuki na wivu dhidi yao, ikiwa wao wameiona fulsa na kutumia that means Wana uelewa.
Jamii kama kwel hatuwataki hao watu kwenda kuchambua na kuchangia mijadara mikubwa yenye kuhitaji elimu kubwa basi tuwakatae kwenye chaguzi kwa kuonesha wanao faa kutumia fulsa hiyo kuchukua hatam.
Kwanini hao darasa la 7 wanawatukana na kuwadharirisha wasomi.
 
Ujinga wake aupeleke huko huko Open. Nawapongeza UDSM. Jitu halijui hata Quadratic Equation linataka kufanya Masters.
Litawezaje ku analyze Data kama sio kununua watu walifanyie. Hata hivyo ku defend lingeshindwa tu
 
Na huyo Kishimba na yeye baada kuwatetea Wananchi wake amekalia ku challenge wasomi. Kisa kapata pesa.
Watu wanapaswa watofautishe Utajiri na Elimu. Huwezi kutukana wasomi wakati hicho kipaza sauti unachotumia bungeni kimevumbuliwa na wasomi. Kazi ya msomi ni kutatua changamato za jamii. Utajiri ni matokeo tu.
 
Musukuma, Shigongo, Lusinde na Kishimba hawana hata hadhi ya kuwa wafagiaji wa barabara za vumbi. Ujambazi Uzandiki na pengine kupora haki za wengine kuishi ndio zimewafikisha hapo wala sio akili. Ndakichako wambie hao wabakie na ujuaji wao
Mkuu, kufanya ujambazi ukatajirika na uko huru hujafungwa gerezani hiyo sio akili?!
 
Ujinga wake aupeleke huko huko Open. Nawapongeza UDSM. Jitu halijui hata Quadratic Equation linataka kufanya Masters.
Litawezaje ku analyze Data kama sio kununua watu walifanyie. Hata hivyo ku defend lingeshindwa tu
Kwanza chuo chenyewe anachokitaka kinachukua vipanga tupu. Enzi zetu hadi div III ya mwanzo walikuwa wanachukua COET... Ila kwa sasa watoto wanapelekeana moto kiasi kwamba div II ni mbinde kupata nafasi. Shigongo akajiunge hata na chuo cha nyuki tabora au chuo cha ufundi stadi VETA Oljoro campus.
 
Kwaiyo watafutilia mbali hicho certificate ya Shigongo?
 
Akiumwa anapelekwa hospitali...anatibiwa na msomi....

Anasahau pia msomi huyo Ni tunda la mwalimu wake profesa.....
 
Hao darasa LA Saba mna takiwa muwakatae kwa ninyi wenye digree na masters sijuh kutumia hizo nafasi za kugombea huo uwakilishi. Vinginevyo acheni chuki na wivu dhidi yao, ikiwa wao wameiona fulsa na kutumia that means Wana uelewa.
Jamii kama kwel hatuwataki hao watu kwenda kuchambua na kuchangia mijadara mikubwa yenye kuhitaji elimu kubwa basi tuwakatae kwenye chaguzi kwa kuonesha wanao faa kutumia fulsa hiyo kuchukua hatam.
Hatuwezi kuwakataa hivi hivi. Lazima kwanza yafanyike mabadiliko kuhusu sifa za kugombea Ubunge. Hilo la kujua kusoma na kuandika ama Kiwashili ama Kiingereza lisiwe kigezo muhimu katika kugombea Ubunge. Sifa nyingine ziongezwe ili kukidhi mahitaji ya dunia ya sasa na mazingira yaliyopo sasa.
 
Musukuma, Shigongo, Lusinde na Kishimba hawana hata hadhi ya kuwa wafagiaji wa barabara za vumbi. Ujambazi Uzandiki na pengine kupora haki za wengine kuishi ndio zimewafikisha hapo wala sio akili. Ndakichako wambie hao wabakie na ujuaji wao
Hizo ni chuki binafsi.Na kama hutaziacha basi tegemea kuwa masikini kabisa na usiyena maana katika jamii
 
Habari wakuu,

Natumaini kila mmoja anaendelea vyema. Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni. Pia nina uhakika wa uhuru baada ya kutoa maoni kwa sababu huu uzi haugusi mamlaka za kidola bali viongozi wachache wanaopotosha umma.

Jana nilitazama video iliyokuwa ikimuonyesha Mh Eric Shigongo akitishia kuchomoa shilingi kwenye bajeti ya wizara ya elimu kwa hoja zilizokosa weledi. Kabla ya kuangalia hoja ya huyu mbunge tujikumbushe kwamba siku za karibuni huko bungeni kumezuka utata wa baadhi ya bunge kudai kwamba wasomi sio lolote bora walioishia darasa la saba. Hoja imetokana na wao kupata mafanikio makubwa kiuchumi na kisiasa bila kwenda shule. Ni mambo ya kushangaza sana.

Mh Shigongo ni mtu ambaye hakubahatika kupata elimu ya sekondari. Aliishia darasa la saba na kupata elimu kwenye mambo ya afya ambapo pia upataji wa hiyo nafasi ya chuo pia ilikuwa ni kama bahati. Mwenyewe mara zote amekuwa akisema umaskini ndo ulisababisha iwe hivyo kwa upande wake. Baada ya mapambano mengi sana maishani hatimaye Ndugu Shigongo akapata nafasi ya kusomea shahada ya kwanza Chuo Kikuu kupitia nafasi za watu walioshia darasa la saba ila hawakupata elimu ya sekondari. Kigezo kikuu cha nafasi hizi ni uwe umefanya vitu vikubwa vya kipekee kwenye jamii na una nia ya kuongeza elimu.

Ni utaratibu uliokuwa na baraka za tume ya vyuo vikuu (TCU). Jamaa alisomea TUDARCO. Sio vyuo vyote vilifanya huu utaratibu. Kwa mujibu wa Waziri wa elimu ni kwamba seneti za vyuo haziingiliwi kwenye kuweka vigezo vya kujiunga vyuoni ili mradi hawavunji kanuni za TCU na wizara. Tatizo la Shigongo kwa mujibu wa maelezo yake ni baada ya UDSM kumtaka aambatanishe cheti cha kidato cha nne wakati akiomba nafasi ya kusoma Masters. Hili jambo lilimkera Shigongo hadi kutaka kuchomoa shilingi kwa hoja kwamba TZ inakiuka taratibu zinazotumika nchi nyingi za kutambua vipaji na mambo makubwa yaliyofanywa na baadhi yetu ila bahati mbaya huko nyuma hawakubahatika kupata kusoma sekondari.

Mh Waziri wa elimu kwenye majibu yake kwanza alisema UDSM haiingiliwi kwenye taratibu zake. Pia huo utaratibu uliomwezesha Shigongo kupata nafasi ya kusoma Chuo Kikuu ulisitishwa baada ya kutokea janja janja nyingi. Na pia kwa sababu wabunge wengi ambao hawajasoma wamekuwa wakidai vyeti vya elimu ni makaratasi tu kwanini walilie tena kwenda chuo? Si bora wabaki kwenye ujuaji wao kuliko kulilia kitu walichosema hakina maana?

Binafsi nampongeza Mama Ndalichako kwa kutoa majibu mafupi yaliyojaa points tupu. Huo utaratibu uliotumika kumpatia shahada Mr Shigongo ni mzuri lakini kutokana na janja janja ya sisi wenyewe basi ni utaratibu hatari usio salama. Nchi yetu haina rekodi nyingi zinazowahusu wananchi mmojammoja kiasi kwamba ni ngumu kupata uhalali wa mafanikio tunaowaona nayo wengi. Utakuta mtu anaonekana genius kwenye biashara kumbe nyuma ya pazia kuna haramu za kutosha. Ushauri wangu ni hawa watu waliopata mafanikio kama wanataka vyeti waende kwenye hizi centres za mitihani ya QT ili wapate vyeti kihalali na wajue kabisa elimu haina mbadala. Bila wasomi wa kutosha ni ngumu nchi kusonga mbele. Kama mtu hana elimu na hataki kukaa darasani basi abakie tu na hela zake hakuna haja ya kusumbuana. MWISHO kabisa kuna haja ya KATIBA kubadilishwa ili kutoingiza vilaza bungeni.
Yaan ww ni mpuuzi ambao wapuuzi wanakukanyaga juu,wanaenda kwa wapuuzi wengine.Yaan umejaza page na page kumbe unashabikia majibu ya kijinga kabisa.Yaan ww unatabia za kike.Unapenda ushindani na kushabikia utopolo tu.
 
Kwanini umekosa ubunifu kwenye matusi yako? Una cheti cha kidato cha nne?
 
Musukuma, Shigongo, Lusinde na Kishimba hawana hata hadhi ya kuwa wafagiaji wa barabara za vumbi. Ujambazi Uzandiki na pengine kupora haki za wengine kuishi ndio zimewafikisha hapo wala sio akili. Ndakichako wambie hao wabakie na ujuaji wao
Utakufa kwa wivu bwege wewe, tuonyeshe mali zako zilizo halali.
 
Back
Top Bottom