Asante Profesa Ndalichako kwa majibu yako kwa Erick Shigongo

Asante Profesa Ndalichako kwa majibu yako kwa Erick Shigongo

Hawa jamaa ni wajinga sana na tukiwachekea chekea wanaweza kweli kutumia ujinga wao kutunga sheria ambazo Nchi yetu itaonekana kituko huko duniani.
Mfano
1. Mbunge anataka kianzishwe chuo cha wizi ili iweje sasa. Hii si itasaidia kuharibu jamii? Maana ya Elimu ni Kuikomboa/ kuisaidia jamii na sio Kuiangamiza jamii
2. Mbunge anataka muda wa kusoma University uwe miezi 8. Hivi anaelewa kuwa mitaala ( Curriculum) ambayo ipo recognized all over the World. Watu wamefanya utafiti na kukubaliana mtu anatakiwa asome University ( minimum 3 yrs)
3. Anaponda Elimu ya Manunuzi ( Procurement) kuwa ni kuuza tu vitu madukani!!. Hivi anajua huyo mtu wa Procurement lazima ajue flow nzima ya Order requisition, Order processing, purchasing preparation (PO), Delivery Processing (mfano issuing Delivery note), inventory control, Tenders preparation, Evaluation, Local & International Vendors Contracts, Enterprise Resource Planning, Supply Chain
4. Waone tofauti ya Mo, Bakhresa, Mengi, Rostam na Wao. Hakuna siku akina Mo walishambulia watu waliosoma
5. Rekodi za TRA zinaonyesha Leading Tax Payers ni Bakhressa , IPP, MTEL. Naomba TRA ianze kuwafuatilia hao jamaa isije kuta hata kodi za serikali hawalipi vizuri
 
Nimeguswa na yafuatayo:-

1. Namfulia kofia Profesa Joyce Ndalichako kwa majibu mubashara aliyoyatoa kwa Msukuma na Shigonga Erick. Kama elimu ni makaratasi hakuna sababu ya kulalama Bali walalame na biashara zao. Eti recognition of prior learning! Hapa ni Tanzania na si Uingereza, Australia au Marekani. Kama Shigongo anataka aendelee na prior learning ya masters aende kwenye hayo mataifa ya recognition of prio learning anayoyataja.

2. Mtu anaweza akaonekana genius wa biashara kumbe nyumba ya pazia kuna haramu nyingi (nakufulia kofia). Siamini kama akina Msukuma biashara wanazotamba nazo zitakuwa za kwao tu bali yaliyojificha yapo na yawezekana wanatumwa kuwashambulia maprofesa (wasomi). Ninyi Maprofesa unganeni mkatae ujinga na uzandiki huu wa kina msukuma, Erick shigong, Lusinde na kishimba. Ni ajabu Lusinde kumshambulia Profesa Muhongo halafu kesho yakeProfesa Muhongo anasimama kumuomba msamaha Lusinde; hii ni ajabu sana na mambo kama haya bila shaka yanafanyika Tanzania tu!

3. TCU ilifanya kosa kubwa tena sana kuruhusu vilaza kuchezea elimu yetu. Siwezi kuteseka kwa zaidi ya miaka 16 kuzotea digrii (shahada) ya kwanza halafu kilaza wa darasa la 7 anapewa shahada hiyo kwa njia ya mkato. Asante sana profesa Joyce Ndalichako (distinguished professor) kwa kutuambia chanzo cha uozo huo.

4. Ni wakati wa katiba yetu hasa ibara ya 67 kufanyiwa marekebisho ili kuongeza sifa ya mtu kuwa mbunge bali ya kujua kusoma na kuandika ili kuziba mianya ya vilaza na vihiyo kuingia bungeni. Hapa namfulia KOFIA Hayati John Pombe Joseph Magufuli Rais wa awamu ya 5 ya JMT kwa namna alivyowaondoa wale vilaza na vihiyo wa kidato cha NNE waliokuwa wameandikishwa pale chuo kikuu cha dodoma kwa minajiri ya kusoma na hatimaye kutunukiwa shahada ya kwanza.

5. Dr. Tulia Akson yupo makini kwa namna alivyomjibu msukuma kuwa elimu si ya kurukiarukia bila kufata utaratibu na vigezo muhimu.

Ni kosa kubwa sana tena sana tena tena sana kuwaruhusu vilaza na vihiyo kuchezea elimu yetu.
 
Kama elimu haina umuhimu mbona mtoto wake yuko China anasoma udaktari. Arudi akae nae Kongwa achunge ng'ombe
Mbaya zaidi mtu kama Ndugai naye ameanza kuucheza mziki wa akina Musukuma,stupid.Kila mtu anakosolewa pindi atendapo makosa fulani.Makosa hayo yapo kwa wasomi tu hata wanangwe vile?Ndugai naye yupo yupo tu kama msukule akishadadia kauli za akina Musukuma.
H
 
Hawa viongozi wanakera sana, ila hawajui tyuuuuuh.
Ila kiukweli hadi sasa hivi siamini kama Shigongo ni hewa kiasi hiki.... nilikuwa naonaga kama watu wanamwonea kumbe hewa. Aisee elimu ni kitu ingine kabisa
 
Naomba kujuzwa maana ya kuchomoa shilingi
 
Maelezo mazuri halafu katikati umejaribu kwa kumshambulia mtu binafsi badala ya hoja
Hoja imetolewa na shigongo,we unashambulia wengine ambao wameponda vyeti
Sijamshambulia. Kila nilichoandika source ni yeye mwenyewe Shigongo. Amekua akisema mara nyingi hayo kwenye mikutano yake ya ujasiriamali.
 
Back
Top Bottom