Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!

Tumuulize P kama alishakuwa mwanasiasa , hasa siasa ambazo ccm yupo🤔Mbona ameigopa kusema jibu alilopewa alipopata fursa kuuliza swali
Sijaogopa ni sikumbuki nilijibiwaje!. Mtu kuuliza swali, ukajibiwa halafu hukumbuki ulijibiwaje, ndizo siasa zenyewe!.
P
 
Ajabu sana miaka yote hiyo mikutano ya kisiasa ipo kisheria, sheria imevunjwa waTanzania wanajionea sawa tu kama majuha vile. Wamerogwa au inakuaje
 
Tatizo kubwa la pascal ni kuwa ukisoma post zake zote na ref zote anazofanya kupitia maandiko yake yote! Unapata mistar miwil tu ya kuabudu na kutukuza kijani! Tena kwa malengo ya kupata teuzi! Ushauri wangu "mkono mtupu haulambwi" ongeza jitihada kidogo hata kufunga kamba za viatu wenye ccm yao! Vinginevyo utaishia kuandika insha tu humu jf na kwenye magazeti! Kwa kifupi unazunguruka mno kumpresent hoja zako za mista mi2 tu
Mkuu MTENGETI , mimi ni mwandishi na mtangazaji, kazi yangu ni kuandika na kutangaza. Siandiki kusaka uteuzi Je, wajua Sio Kila Kumpongeza, ni Kujikomba/Kusaka Teuzi? Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
P
 
Hakika Rais Dkt. Samia ni zawadi pekee kutoka kwa Mungu kwa watanzania.
Tumshukuru sana Mungu kwa ukuu wake na uwezo wake usio na upeo.
Mungu azidi kumlinda Rais wetu.
 
Chawa ni chawa tu kwa kweli, wakati mwendazake anapindua pindua nchi atakavyo yeye mbona hizi makala ndefu tulikuwa hatuzioni?

Wakati wa siku 100 za kwanza za mama Samia mbona makala hizi ndefu tulikuwa hatuzioni?
 
Ajabu sana miaka yote hiyo mikutano ya kisiasa ipo kisheria, sheria imevunjwa waTanzania wanajionea sawa tu kama majuha vile. Wamerogwa au inakuaje
Watanzania wengi ni watu wa kawaida sana hawajui haki zao, ila katika utetezi wa haki, ukimuondoa Zitto na ACT yake, Chadema sio lolote sio chochote na hili tumewalaumu sana humu Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele! na CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.

Mikutano ya siasa ni haki ya vyama vya siasa, haki inapoporwa, haiombwi!, hii sio hisani, inapaswa idaiwe, na ikibidi ipiganiwe!.

Watanzania tumezoea haki zetu kugeuzwa ni hisani, favours, hivyo tunapiga magoti kunyenýeea tupewe kwa kuhisaniwa kama zawadi, na tukipewa tunashukùru kwa shangwe na mapambio!. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
P
 
Chawa ni chawa tu kwa kweli, wakati mwendazake anapindua pindua nchi atakavyo yeye mbona hizi makala ndefu tulikuwa hatuzioni?

Wakati wa siku 100 za kwanza za mama Samia mbona makala hizi ndefu tulikuwa hatuzioni?
Mkuu FUSO, nimejiunga jf 2006 hivyo ndani ya miaka 10 ya JK, nimeandika humu, ila amini usiamini, ndani ya miaka 5 ya JPM, nimeandika Makala nyingi za ukosoaji kuliko miaka yote 10 ya JK. Nina Makala zaidi ya 100!.
P
 
Hapa nilimtaka Pascal anijibu kwenye mada yake ameongea mengi ila hakuthubutu kusema majibu aliyopewa na mwana sisiemu mwenzie
Japo mimi niliuliza swali, ila nina mambo mengi kichwani, hivyo sikumbuki niijibiwa nini, ila kwa sasa swali lile na jibu lake it's immaterial maana limeisha tekelezwa na Ma mkombozi Samia!.
P
 
P anatamani kupata nafasi mzuri ya kurejesha Kwa jamiii kweli kweli Tena kupitia ccm, ila kiuhalisia P hayupo pamoja na ccm, ila kwa maana TU ya kufikia malengo anaambatana nao . Amua moja P, kuambatana na ccm mwanzo mwisho au uamue kuachana nao kabisa na uamue kurejesha Kwa jamii Kwa jasho na damu kama wafanyavyo chadema, usihofie matokeo , kama lengo ni kurejesha Kwa jamii🤔
Amen,

Amen na asante, Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
Niombee niweze
P
 
Hakika Rais Dkt. Samia ni zawadi pekee kutoka kwa Mungu kwa watanzania.
Tumshukuru sana Mungu kwa ukuu wake na uwezo wake usio na upeo.
Mungu azidi kumlinda Rais wetu.
Amen asante, na sisi watu wa shukrani, hatuishii kuchagia tuu posts, tunamuanzishia kabisa threads za kumtolea Mungu shukrani kwa Samia. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania na Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
P
 
Kuna vitu watu tulivisema humu, sasa vinaanza kutekelezwa, hivi hapa ukimpongeza Samia, utaonekana chawa?.
P

mama keshasema amewashtukia nyie ni CHAWA mlikuwa mnampoteza

Fls4GeCXgAAPjDL
 
Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya wiki iliyopita
View attachment 2141741View attachment 2141742
Wanabodi,

Kitendo cha kuachiwa kwa Freeman Mbowe ni the biggest political milestone ya rais Samia.
Asante sana Rais Samia, Big Up Sana.

Wasalaam

Paskali
Kitendo cha Rais Samia kumuachia Mbowe was the biggest milestone wakati ule. Rais Samia kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, ikawa bigger than the previous biggest!, sasa kitendo cha jana Rais Samia kuwa Mgeni rasmi event ya Chadema ni the biggest milestone ambayo imezika rasmi the politics of confrontations and replace them with the politics of reconciliation.
Hongera sana Rais Samia, hongera sana Freeman Mbowe.
Poleni sana wahafidhina wa pande zote kwa maumivu!, both manyumbu na magamba.

Reconciliation hii isiishie kwa Ccm na Chadema bali ifike na kwa wale hawana Chama chochote lakini wana maumivu makali yaliyosababishwa na Ccm !!
 
Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya wiki iliyopita
View attachment 2141741View attachment 2141742
Wanabodi,
Hili ni bandiko la Pongezi kwa Rais wetu, Mama Samia.
Kama mtu uliwahi kuandika kuhusu jambo fulani, halafu hilo jambo likafanyika, kwa jinsi ile ile ulivyoandika na ulivyoshauri, hata kama halikufanyika kwasababu ya andiko lako au ushauri wako, lakini limefanyika, hauna budi kupongeza.

Kitendo cha kuachiwa kwa Freeman Mbowe ni the biggest political milestone ya rais Samia, mikutano ya hadhara itaruhusiwa, Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi itaundwa, Sheria ya Uchaguzi itarekebishwa na mwisho kabisa ni Rais Samia atakwenda kutupatia katiba mpya!.

Asante sana Rais Samia, Big Up Sana.

Mungu Mbariki Rais Samia ili ayaweze yote katika YEYE,

Mungu ibariki Tanzania.

Wasalaam

Paskali
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, huku tukielekea mwaka wa uchaguzi, nafanya tathmini ndogo ya expectations zangu na awamu hii ya Rais Samia, nili expect nini, nini kimefanyika, nini bado hakijafanyika, na nini kinaweza kufanyika kabla ya 2025 ili Watanzania tufanye Uchaguzi Mkuu huru na wa haki unaosimamiwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.

Katika bandiko hili, nilikuwa na the following expectations
1. Mikutano ya hadhara itaruhusiwa,
2. Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi itaundwa,
3. Sheria ya Uchaguzi itarekebishwa
4. na mwisho kabisa ni Rais Samia atakwenda kutupatia katiba mpya!.

Expectation number 1, imetekelezwa.
Expectation number 2 na number 3, imo on a pipeline mwezi February 2014.
Expectation number 4, bado, na kwa muda uliobakia kabla ya uchaguzi, the time is too little too late, hatuwezi kupata katiba mpya!, ila sasa tumuombe Rais Samia, hata kama muda uliobakia hauwezi kutupatia katiba mpya, muda huu unatosha kufanya mabadiliko madogo ya katiba, tukafanya uchaguzi Mkuu huru na wa haki.
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Wanabodi
Hatimaye kesi ya Mbowe imefutwa!.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Ukiaminiwa, Jiaminishe", Tanzania ni nchi ya wote, Watanzania wote, binadamu wote ni sawa, CCM na Wapinzani wote ni sawa, na wote tuna lengo moja la kuijenga Tanzania yetu ambayo ni moja hivyo tunajenga nchi moja, tunajenga nyumba moja hatuna sababu ya kugombea fito.

Wiki iliyopita DPP kaifuta kwa Nolle kesi ya Mbowe, na Mbowe na washtakiwa wenzake kuachiwa huru, japo kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu ni DPP ndie pekee mwenye mamlaka ya Nolle, lakini watu wote wenye jicho la tatu wanamjua ni nani aliyeifuta kesi ya Mbowe na aliyemuachia Mbowe awe huru!.

Mbowe mwenyewe mara tuu baada ya kuachiwa huru, siku hiyo hiyo alikwenda Ikulu kuzungumza na Rais Samia, kila mtu mwenye akili, alijua Mbowe, alikwenda Ikulu kuzungumza nini na Samia,

Kitendo cha kuachiwa kwa Freeman Mbowe ni the biggest political milestone ya rais Samia, mikutano ya hadhara itaruhusiwa, Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi itaundwa, Sheria ya Uchaguzi itarekebishwa na mwisho kabisa ni Rais Samia atakwenda kutupatia katiba mpya!.

Paskali
Mkuu Lax karibu pande hii ushuhudie.
P
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom