Asanteni wana jamii forum,nimeshapata mpenzi wa maisha!

Asanteni wana jamii forum,nimeshapata mpenzi wa maisha!

Nakumbuka uliandika vigezo hivi ili kumpata mwenza:

habari kaka,natumai mwenye sifa tajwa hapo juu ndo unayesoma hapa'
mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 30,nipo serious na natafuta
mwanaume mwenye sifa hizo kwa kuwa mwenyewe nina sifa za mwanamke mrembo
shepu namba 8.yaani juu mwembaba chini Mungu nampa sifa zake,kwani kanijalia kusema
ukweli na ni original kabisa,rangi yangu ni maji ya kunde with Excelent Health!
Elimu ya chuo,na ni mwalimu wa Secondary hapa Dar na najitegemea na naendelea na masomo.
Swali,je kwa nini nimeamua kuchagua njia hii ya JF kumtafua mpenzi wa kweli?
ni kwa kuwa nimeona wengi wanaotumia FORUM HII wana upeo mzuri na waelewa
na si wahuni,na hawatachukulia suala hii kama joke ndo mana sijaenda kule kwenye
chit-chat so you have to be serious here! kama sio wewe mlengwa naomba upite tu nitakushukuru.
Jambo jingine ninalopenda kuweka wazi ni kwamba kabla ya kuchukua uamuzi huu mgumu
nilikuwa na mpenzi ambaye awali nilijidanganya kama nimepata kumbe sivyo,kwa kuwa hakuthamini
mapenzi yangu ya dhati kwa kunichukulia kiutani huku miaka ikiwa inapita pia nikatambua kwamba
hatuendani kwa mambo mengi,mfano ni mlevi wa kupindukia,hapendi kujituma nikiwa na maana
ya maendeleo hata ya kupiga hatua moja mbele ki- maisha,hakuwa anaonyesha Real love ya
kusema mimi naweza kujivunia hata kwa marafiki kama nina mpenzi muda mwingi nikawa lonely
yeye akiwa Busy na ulevi uliokithili.Ivyo tukielewana ukinipa sifa zako tutaonana live!
So if you are lonely out there you are welcome and just be realistic and affectionate!

Nilikujibu hivi "Ipo siku na mimi mtatangaza jambo hapa ndani. wewe dada unafiti kila idara kwangu kwa kuwa ninataman sana mwalimu.
Nataman mwalimu kwa sababu amesoma maadili na phychology automatically wanakuwa wastaarabu then kaz yenyewe inafanyika within 8 to 10 hours means kuna uwezekano wa mwalimu kuwepo nyumban kwa masaa 14 hadi 16 tofauti na mfanyabiashara wa masafa, madaktar au wauguz na askar hao siwataki na bora niwe bachela mpaka kufa SABABU NINAZO.

Sitatuma maombi kwako kwa kuwa nina 27 na bado sijatarajia mke hv karibuni ila nikiwa tayari ntahitaji mke mwenye wasifu kama wako.

Mungu akutangulie!"

Leo nimeamini kumbe JF hakuna lisilowezeka na namshukuru mwenyez Mungu kwa kukupa kile uliomba kwa sisi wakristo tunalijua neno hili "ni nani atamuomba baba ake mkate na apewe jiwe..."
Kwa kuwa ulitoa vigezo hivyo hapo juu na Bw. James amekupata na wewe umempata hivyo mmepatana.

Nawapenda sana waalimu kama nilivyosema siku ile na nikatoa mpaka sababu nategemea utakuwa zaidi ya maelezo yangu kwa James, tena mpole usiehamaki kujibu ukihojiwa jambo na mwenye kudadisi ukwazwapo. Wanawake wengi wamekaa Ki-beijing beijing mpaka inakera... Kuwa wa Mungu tena Mtanzania msomi ambaye naamin hata watoto ufundishao watakupenda sana kwa uadilifu kwao na ndoa uiendeayo.

Usiache kuja jamii forums ili uweze kuchangia michango hasa ya kimahusiano kama ulivyompata James kwa Cyber-love.

Nasikitika, jifunze kuishi maisha mapya na uombe Mungu ndoa yenu kamwe isijevunjika hata ukimfumania James kaa nae na akuambie na akiri kutothubutu nina imani na penz lenu kwa kuwa limepita kwa mchakato wa mchujo japo si wa muda mrefu.

Keep it on prayers ili kati ya wale waliokuja PM kama James wasipate nafasi tena ya kukusumbua kwa kuwa umeshatangaza tayari umefunga maombi please endapo utarusu hili means utakuwa una tatizo.

Binafsi ntataman kuwepo katika harusi yenu na kama ntabanwa na majukumu yangu basi hapa kwa kifuta jasho cha mbali ntapenda nishiri.

Napenda sana cyber-life na ni iman yangu njia yangu itakuja kuwa kama hii kumpata Mchuchuu wangu hapo badae!

God bless u always and ur family to be.
 
it is not over until it is over.... it's good to be optimistic, though
 
hongera sana, mimi wangu pia nilimpata humuhumu jukwaa la jokes tukajifanya kutaniana taniana sasa tumextend utani wetu, tunanunuliana vocha, tunaenda snema kila mwisho wa mwezi, na samtaimu tunataniana yeye ananiita Invisible mimi namwita RussianRoulette.
 
Last edited by a moderator:
When dog turn an bite u plz njoo tena!
 
hongera sana, mimi wangu pia nilimpata humuhumu jukwaa la jokes tukajifanya kutaniana taniana sasa tumextend utani wetu, tunanunuliana vocha, tunaenda snema kila mwisho wa mwezi, na samtaimu tunataniana yeye ananiita Invisible mimi namwita RussianRoulette.

Hahahah......dah!! We hata ban hautokaa upewe aisee!
 
Last edited by a moderator:
Yaani... nimechoka hapa, nimekaa kwanza nasoma mara ya pili. hahahahaha klorokwini simuwezi. Sasa huyo mchumba wako hana jina? Halafu kwa nini uchague kumpanga Russian Roulette na isiwe Husninyo au sweetlady?

We acha tu, mi mwenyewe nimecheka kweli!! Maybe wanajifananisha na couple ya moderators kwenye meli yao lol!!
 
Last edited by a moderator:
RussianRoulette wako hajambo? Halafu kama nilikuona unaimba kwaya kwenye muungano!
Yuko poa, muda si mrefu tulkuwa tunabishana nani akate simu mwanzo, mapenzi bana, jana tu alisema kaniota namlisha keroti. Aaah Nakonda jamani

Kwaya za muunggano kaimba @Uporoto na kundi lake
 
Saint Ivuga
poa jibaba, wewe hauko serious bana mbona niliweka mambo hazarani kulekule. Kuna halfu price offer linaisha kesho, fanya fasta jibaba.

nilishindwa kuingia humu ndani.nilimsindikiza jamaa yangu ukweni kwake tukakuta jamaa za mke wake ni walevi kinoma ili kuua soo ikabidi tujiunge nao kupiga moja moto moja baridi,pombe zenyewe wanazokunywa ni kama ile ya Kanumba imagine na sisi sio walevu halafu tulikuwa ukweni tukachanganya na johnwalker kwa nini jamaa asimkumbatie mama mkwe arifu. pombe mbaya inabidi ninywe kila siku ili kuizoea na kuepuka aibu kama hizi arifu .
 
Last edited by a moderator:
Mzima kabisa Saint Ivuga. Sijui umenikumbukia wapi. Ni leo tu nilikua nikisoma ile thread yako ya Simba VS Mazembe, kuna kitu nilikua natafuta, nimecheka kweli. Kuna watu machizi humu ndani... lol
 
Mzima kabisa Saint Ivuga. Sijui umenikumbukia wapi. Ni leo tu nilikua nikisoma ile thread yako ya Simba VS Mazembe, kuna kitu nilikua natafuta, nimecheka kweli. Kuna watu machizi humu ndani... lol

Nimekukumbuka niliingia mida flan hivi nikashindwa kukusabahi kuna mtu alianza kunipigisha stori kuhusu gemu ya kesho kutwa ya simba..nawaombea sana washinde hii gemu dhidi ya waarabu wa sudan hapo. in other way kila kitu kiko poa.
 
Back
Top Bottom