Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akifanya mahojiano na Salim Kikeke, Crown Media
Asha-Rose Migiro: "...kuhusu vyombo vya ulinzi na usalama. Ndugu Kikeke, unafahamu kwamba katika nchi yoyote na Tanzania haina tofauti, vyombo vya ulinzi na usalama vina kazi zake, vina majukumu. Tukizungumzia polisi, tuseme mojawapo ya majukumu yake makubwa ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Jeshi la wananchi la Tanzania lina usala– lina kazi kubwa ya kulinda mipaka ya nchi yetu."
Salim Kikeke: "Lakini sio kuuawa wananchi."
Asha-Rose Migiro: "Sio kuuawa wananchi. Kwa hiyo majukumu yake ya msingi ndio hayo, sio kuuawa wananchi. Na utafahamu kwamba tarehe 29 Oktoba, nchi nzima tulikuwa na vituo vya kupigia kura takriban 99,000. Na kwa kuwa tuliamka katika hali ya kawaida, wenzetu wanaolinda usalama wa raia walikuwa tayari wamekaa kwenye maeneo ya kupigia kura kwa sababu wananchi walio wengi walikuwa wamejitayarisha kutoka kwenda kupiga kura na kurejea nyumbani.
Sasa ilipotokea kadhia ile, vyombo hivi na hasa polisi walilazimika sasa kujigawa, huku usalama uendelee kuwepo kwenye maeneo ya kupigia kura na huku waje katika yale maeneo ambayo yalikuwa na fujo. Na pia itakumbukwa kwamba fujo hii ilikuwa kama moto wa nyikani; pale fujo, huku fujo, sio Dar es Salaam pekee yake, na katika nchi nzima kwa ujumla wake. Kwa hiyo, hawa walikuwa ni kama wana jambo kubwa la kufanya. Kuhakikisha kura zinaendelea kupigwa na vilevile usalama katika maeneo mengine.
Hilo lilikuwa ni jukumu lao kubwa na walilifanya, na tunaamini kama wasingefanya vile, labda madhara yangekuwa makubwa zaidi katika taifa letu.
Na la pili ambalo tunaweza kuliunganisha hapo kwa nini pia Chama cha Mapinduzi kupitia Halmashauri Kuu tulizipongeza, kwa sababu kazi waliyoifanya ndio imefanya taifa letu liwe imara mpaka leo hii, pamoja na ile fujo ambayo kwanza hatukuitegemea lakini pili haijawahi kutokea, kwa hiyo ilitushangaza wote tukapigwa na butwaa.
Na kitu ambacho ningependa tutenganishe hapa ni kwamba inawezekana katika utendaji wa kazi zao kukawa na dosari, hiyo hiyo inatokea. Sasa tusichanganye majukumu yao ya msingi, kazi nzuri waliyoifanya ya kutunza amani kwa kiwango kile ambacho kilihitajika kwa wakati ule, na dosari mojamoja zinazoweza kujitokeza. Na hapa sisemi kwamba vifo ni dosari ndogo, sio dosari ndogo, ni dosari kubwa. Lakini ndio sababu kuna haja sasa ya kuangalia mazingira ya vifo vile, lakini hii haiondoi ukweli kwamba kazi waliyoifanya ni kazi ya kutukuka katika taifa letu."