Ashura Masoud: Tuhuma za Heche kula pesa hazina ukweli, hahusiki na fedha za CHADEMA

Ashura Masoud: Tuhuma za Heche kula pesa hazina ukweli, hahusiki na fedha za CHADEMA

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Masoud, amesema kuwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zinazomkabili Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, hazina ukweli wowote kwani kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, kiongozi huyo hahusiki na usimamizi wa masuala ya fedha za chama.

Masoud amefafanua kuwa sekta ya fedha ipo chini ya sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu, hivyo kama kuna upotevu wa rasilimali, lawama hizo hazipaswi kuelekezwa kwa Mwenyekiti wala Makamu Mwenyekiti.

Amebainisha kuwa shutuma hizo ni muendelezo wa mbinu za kisiasa zinazolenga kudhoofisha msimamo thabiti wa chama, baada ya jitihada za awali zilizohusisha uchochezi wa kidini na mashambulizi dhidi ya viongozi wa kiroho kushindwa kufanikiwa.

 
Na hata kama amekula fedha nje ya mfumo rasmi wa chama. Hana makosa,watu wasiokoteze makosa ya kumwadhibu CDM kuweni macho.
 
Back
Top Bottom