Ni kweli,Niliwahi kufanya kazi taasisi fulani wakaajiriwa mabinti wawili ndio wamemaliza chuo wakaletwa pale,Wakapata nyumba mmoja wakawa wanaishi,haikupita miezi miwili vurugu zikaanza,kuna siku wamepigana mpaka kupelekana polisi,baada ya hapo wakatengana kila mtu akaishi kivyake nyumba tofauti.
Baada ya muda wakaletwa tena mabinti wawili wapya kwahio mle ofisini wakawa wanne,ilikuwa ni shida.
Ukikaa na na huyu labda mnakunywa chai akapita mwenzake utasiki 'huyu nae simpendi kama nini' ukiuliza vipi kwani hujibiwi anaishia kubinu mdomo tu.
Haya ukikaa kupiga stori mbili tatu na huyu,ikatokea mwingine akawa anashida na wewe halafu ukachelewa kuitika aisee utaitwa sauti ya juu kama mtu anakufokea hivi,yaani ni vurugu tupu
Yule Boss wetu alipata shida sana,kesi za kila mara.