Asikudanganye mtu! Rafiki wa kweli katika dunia hii ni hela (pesa/money)!

Mwanamke anaweza mvumilia baba mzazi asiye na pesa muda wote hawezi mvumilia mume wake akose pesa miezi mitatu
 
Ndiyo unajua sasa? Wenzako walijua tangu wakiwa chekechea.
 
Kupata pesa sio kazi KAZI ni kuifanya pesa ikae nawe milele.
Nimepoteza jumla ya million 400 kwa miaka 18 ya utafutaji lkn nishagundua makosa yangu sasa hivi ikija haitoki
Mkuu tunaomba tujifunze kutoka kwako...
 
Mtu pekee anaeweza kukupenda hauna hela ni mama yako mzazi pekee.
Lakini ni upendo wa kinafiki na kimasikini. Mama ukiwa unajitafuta stakuonyesha upendo kama wooote! Lakini ikifika umri usomeki na yeye anakumwaga! Ogopa kukosa hela broh!
 
Ukiwa huna Hela unaweza ona pesa ni kila kitu ninachoshukuru pesa ninazo na marafiki wa kweli ambao ni ndugu zangu ninao
 
Hapa nipo home mama kapita na kajukuu, jirani kamtania "naona huko na mme wako" kajibu "nampeleka huko kwa mama yake mme gani hana hela? πŸ˜€πŸ˜„πŸ˜„
 
Mkuu.. Yote usemayo ni sawa kabisa.. Ila kuna muda hayana maana.. Yan kuna muda pesa haina maana kabisaa kama hauna amani.. Haswaa ni amani ya moyo ambayo inaweza kukufanya uthubutu kufanya chochote..
Weeeeweee! Hiyo amani utaitoa wapi bila hela?
 
"tukusaidie nini?" Hili ndilo swali la msingi, wewe ulitakaje? Mimi nikifika sehemu ya huduma natulia, muhumu akija nataka aniulize short and clear kama ulivyoulizwa, sihitaji mambo mengi. Nikiona wahudumu hawaji nawafuata huko huko bila hata salamu na kuwaeleza "nataka hiki"

Mwanzoni nilikuwa najifanya muungwana, nikienda dukani naanza na salamu lakino unakuta wauzaji wanajivuta hata salamu yako wanaiona haina maana kwa sababu wameishakushusha thamani.

Nikaona isiwe kesi. Sasa hivi nikute mhudumu awe mzee au kijana, nikifika hiyo sehemu sisalimii ni kusema tu "nataka hiki, kipo?" nikimuonea aibu kidogo kama ni mzee, ndio nasema "Samahani mzee nahitaji hiki" Lakini huyo mzee hapati salamu pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…