kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kama jezi ya timu yako haina logo ya Nike, puma, umbro au adidas badala yake ina logo ya vunja bei, sandaland, sijui kindoki, gsm na akina aden rage, hiyo ni fulana na bukta tu, sio jezi ya kupandisha sijui mlima gani na kuunajisi.
Tufike mahali tuwaambie watu wetu ukweli kuhusu hizi jezi badala ya kuwaaminisha kuwa tunaleta jezi/uzi bomba na hadaa mbalimbali za kuwaibia wadau wa mpira.
Kuna jezi ya timu ukiifua tu mara moja inapauka au inaongezeka ukubwa lakini inasifiwa kupita maelezo ili watu waibiwe. Lete jezi bora hata kama bei yake ikiwa sh. 100,000 lakini ni jezz kweli. Kumsajili mchezaji ghali na kumvakisha tambara sio poa. TBS ingilieni kati utapeli huu ili ubora wa jezi ulingane na thamani ya pesa.
Ni heri zikaletwa jezi 150000, 100000, 40,000 na 30,000 ili anaemudu jezi avae na anaemudu jezi hafifu avae kama ilivyo kwenye viingilio vya mlangoni viwanjani.