Asikuzuge mtu, jezi zote za timu zetu ni fulana na bukta za kawaida tu

Asikuzuge mtu, jezi zote za timu zetu ni fulana na bukta za kawaida tu

Nilijua TU itakuwa ni vuluvulu ileile, kama itavaliwa na kufuliwa kila siku kwa miezi 3 hamna kitu hapo. Angalia na bei yake kama Yanga vile vile kasolo yake Yanga wamezindulia Ikulu ya Malawi.
Zikitenezwa jezi za quality kubwa ni washabiki wangapi watakuwa na uwezo wa kuzinunua?
 
Sasa ndugu yangu jezi ikiuzwa 100,000 watanzania wanagapi watakua na uwezo kumudu hiyo gharama? Kumbuka Tu hata hiyo 40k wengi hawanunui wanasubiri zile za juakali za elfu 10..

Sasa ikiwa laki huoni vilabu zitapoteza kabisa mapato na kuwanufaisha wajanja...

Kwanza mi naona bei iko Sawa kulingana na Hali halisi ya Maisha wa Watanzania
Kakaaa!! Toa jezi original kwa wanaomudu original na hafifu kwa wanaomudu hafifu Hata pale uwanjani viingilio vinatofautiana. Toyota anatengeneza magari ya watu na bei tofauti. Haingii akilini timu inasajili mchezaji kwa mamilioni ya hela halafu unamvakisha jezi ya 20,000
 
Back
Top Bottom