Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Moshi = ni Kijerumani Moschee = Msikiti. Huenda wajerumani waliukuta msikiti hapo. Ndiyo maana
kuna Old Moshi au kwa kijerumani "Alt moschee"

Arusha = Kimaasai La rusa = ng'ombe kijivu

Karatu = Kiyunani (the name of settler) (kratoo maana yake kutamalaki, kutawala)

una uhakika larusa ni ngombe wa kijivu???
 
Tanzania imejawa na majina ya mitaa, Mikoa na maeneo mbalimbali ambayo majina hayo yanavutia sana kwa kweli.

Mfano wa sehemu/mtaa na inapopatikana:

Msasani - DSM

Mwenge - DSM

Nyamagana - MWANZA

Mtwivila - IRINGA

Kihonda - MOROGORO

Tuendeleeni kupeana hazina ya majina haya ambayo hatujui maana yake
 
Samahani, kwa wale wenye kujua historia ya uanzishwaji wa majina ya maeneo, HIVI essence ya neno Gongo la Mboto ni nini? Ni nini historia ya jina hilo? Walikuwa wanakunywa sana gongo au?
 
Huyu huenda ndio wale samaki wanaoitwa "eel" kwa Kiingereza, ana umeme mkali sana huyu.
Asante kwa historia hii mkuu.
Kwa historia niliyoisoma, Jina Dar Es Salaam limebadilishwa ile "EL" na kuwekwa "ES". Jina halisi laKiarabu lilikuwa Dar El Salaam, likiwa na maana ya Bandari salama.
Kimaandishi katika kiarabu inaandikwa El salaam,lakini kimatamshi,inakuwa Es,L haitamkwi,zinakuja Es na S tena.
 
Chekelei - Check the Railway
Chekereni - Check the Train
Kariakoo - Carrier Crops (?)
Kilimanjaro - Kilima Kyaro (?)
Lugalo - Alipopigwa Jerumani Emily Von Zelewisky na Jeshi la Mkwawa
Same - Mzungu kila akienda hapo alikuwa anaona kile kitu kiko vilevile (?)
Simba - Kuna mtu aliliwa na simba katika hiyo barabara pale Chuo Kikuu

Mmmhh Kuna wajomba waongoo kinomaaa duuu. Umesoma chuo cha sound ww uongooo?
 
Kariakoo ni carriers call yaani wapagazi walopokuwa wanapatikana ili kwenda kubeba mizigo kwenye meli bandarini
 
Ni nini asili ya maneno haya na kipi kiliwashawishi au kuwatuma wayaite hivi?
  • Kawe.
  • Mchambawima.
  • Makunduchi.
  • Mikocheni.
  • Mwananyamala.
  • Goba
  • Kiboroloni.
  • Kiembe samaki.
  • Kijitonyama.
  • Nyegezi.
  • Butiama.
Nitashukuru kwa michango yenu na hasa majibu yenu.
 
Mwananyamala ni kizaramo maana yake mwana nyamaza......
niliwahi simulia chanzo nimesahau
 
Mikocheni kulikuwa na miti miingi aina ya mikoche........
 
Kiembe samaki ninahisi ulikuwa mwembe wanauoza samaki
 
Kiboriloni....>> kibo alone
Mwananyamala wanadai ilikua ni mbuga simba walikuwamo sasa kuna siku simba alipita na hao wakaaji wakwanza walikua na mtoto akaanza kulia wakawa wanambeleza MWANANYAMAlA dat mwananyamaza!! Sijui kams ni kweli ila ni story za primary.
 
majibu yote katika replies za awali kabla yangu ni ya kweli kabisa kama kuhusu mwananyamala,kawe,mikocheni
 
Back
Top Bottom