Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania


una uhakika larusa ni ngombe wa kijivu???
 
Tanzania imejawa na majina ya mitaa, Mikoa na maeneo mbalimbali ambayo majina hayo yanavutia sana kwa kweli.

Mfano wa sehemu/mtaa na inapopatikana:

Msasani - DSM

Mwenge - DSM

Nyamagana - MWANZA

Mtwivila - IRINGA

Kihonda - MOROGORO

Tuendeleeni kupeana hazina ya majina haya ambayo hatujui maana yake
 
Samahani, kwa wale wenye kujua historia ya uanzishwaji wa majina ya maeneo, HIVI essence ya neno Gongo la Mboto ni nini? Ni nini historia ya jina hilo? Walikuwa wanakunywa sana gongo au?
 
Kimaandishi katika kiarabu inaandikwa El salaam,lakini kimatamshi,inakuwa Es,L haitamkwi,zinakuja Es na S tena.
 

Mmmhh Kuna wajomba waongoo kinomaaa duuu. Umesoma chuo cha sound ww uongooo?
 
Kariakoo ni carriers call yaani wapagazi walopokuwa wanapatikana ili kwenda kubeba mizigo kwenye meli bandarini
 
Ni nini asili ya maneno haya na kipi kiliwashawishi au kuwatuma wayaite hivi?
  • Kawe.
  • Mchambawima.
  • Makunduchi.
  • Mikocheni.
  • Mwananyamala.
  • Goba
  • Kiboroloni.
  • Kiembe samaki.
  • Kijitonyama.
  • Nyegezi.
  • Butiama.
Nitashukuru kwa michango yenu na hasa majibu yenu.
 
Mwananyamala ni kizaramo maana yake mwana nyamaza......
niliwahi simulia chanzo nimesahau
 
Mikocheni kulikuwa na miti miingi aina ya mikoche........
 
Kiembe samaki ninahisi ulikuwa mwembe wanauoza samaki
 
Kiboriloni....>> kibo alone
Mwananyamala wanadai ilikua ni mbuga simba walikuwamo sasa kuna siku simba alipita na hao wakaaji wakwanza walikua na mtoto akaanza kulia wakawa wanambeleza MWANANYAMAlA dat mwananyamaza!! Sijui kams ni kweli ila ni story za primary.
 
majibu yote katika replies za awali kabla yangu ni ya kweli kabisa kama kuhusu mwananyamala,kawe,mikocheni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…