Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

MAANA ASILI YA JINA - “SINGIDA”
Mkoa wa Singida unapata jina
lake hilo kutoka katika jamii ya
Kabila la Wanyaturu –
“Masingida” ikimaanisha Urembo
asilia wa heleni unaotengenezwa
kutokana na zao la miti ya
mapori au misitu ambao
huvaliwa masikioni na vile vile
hutengenezwa na Wanyaturu
ambao ni moja ya jamii ya
 
Sea breeze= Chibirizi (Kigoma)

Ila samahani mleta mada kuna majina huku Manyara yanaishia na consonant sijui chanzo chake mf. Katesh, Hanang, Endabash, Endasaq,
 
Chekelei Korogwe na sehemu nyingine pia IPO kama Moshi. Ilitokana na neno Check Rail ndio maana Iko pale kwenye kivuko cha treni
 
Ziginali maeneo ya ifakara Original yake ni neno SIGNAL alama iliyokuwa ina maanisha Railway crossing
 
Sea breeze= Chibirizi (Kigoma)

Ila samahani mleta mada kuna majina huku Manyara yanaishia na consonant sijui chanzo chake mf. Katesh, Hanang, Endabash, Endasaq,
Mkuu Wairaq sidhani kama ni wabantu wenzetu[Mimi siyo mbaguzi] wao pamoja na jamii mbalimbali za wafugaji wana asili tofauti na ya watu wengine.

Ndio maana Lugha zao hazijachangia neno lolote kwenye lugha ya Kiswahili[pia sina uhakika] hivyo kuziondoa miongoni mwa lugha za kibantu na ndio sababu iliyonifanya niseme siyo wabantu......Kuna neno linatamkwa Haidom nalo lina niacha hoi sana.
 
simu 2000
nilivo sikia ni kwamba apo simu 2000 kulikuwa na wizi mkubwa wa simu na ilibiwa kwa muda huo na kuuzwa muda huo kwa bei ya chini kabisa 2000 ndo leo panaitwa ivo simu 2000
 
Naskia hata ISIMANI(IRINGA) watu wanasema ni IS MONEY. Sijui ni kweli?!
Huenda ikawa kweli, kumbuka hizi ni Hearsay story.....Ila hili eneo lingekuwa uchagani pasingekuwa na haja ya kuuliza kama ni kweli😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom