Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Wakuu katika pitapita zangu nimekutana na historia ya majina ya sehemu ambayo yanatumika hivi sasa kutoka kwenye maneo ya kiingereza;
Do me Love = Dumila (Morogoro)
Mind You = Mindu (Morogoro)
Kill bad Guy = Kibaigwa (Dodoma)
Guy Love = Gairo ( Moro)
Man and Tom Boy = Matombo (Morogoro)
If I care her = Ifakara (Moro)
New Alert = Newala (Mtwara)
Carrier Corps = Kariakoo (Dsm)
Kill it Off Site = Kilosa (Moro)
Kill it on Bed or Down = Kilombero (Moro)

Wakuu mnaweza ongezea karibuni.....
hii fix
 
Tabata ilitokana kuwepo kwa duka moja tu eneo hiko lililokuwa la mwarabu, wateja walikuwa wengi sana folen, na kila mtu alikuwa anataka bidhaa so mwarab akawa anawaambia 'subiri tabata' yan ' subiri utapata'.
 
Na Kundichi? Eti wazungu walikuwa wanaogelea baharini uchi hivo waswahili wakawa wanawnda kuangalia, kwa kuhamasishana walisema "twende tukaangalie mkundu uchi" hivo wazungu kwa kushindwa kutamka vile wakaishia kusema "kundichi". Ndomana panaitwa kunduchi
 
mkumbuke mbagala limetokana na Lumbambala huyu alikuwa ni mfanyakaz ktk mashamba ya wajeruman co wajeruman walishundwa kuita jina lake wakawa wanamuita mbagala.
 
Kuna sehemu mtoni kijichi inaitwa kwa BURUDA, ambayo ilitokana na wajenz wasaidizi wa majengo yaani '' BUILDERS) ila waswahili wakashindwa kutamka hivyo kisahii hivyo kuiita kama buruda...
 
Hili lilitokana na Ng'ombe maarufu aliyejulikana kama Charles. Walikua wanamwita Charles Ng'ombe, lakini kutokana na kufupisha ikatokea Cha-Ng'ombe ... Ndo adi leo pakawa Chang'ombe
 
Na haya je;-
Kwa Tumbo-
Mchamba wima-
Kiembe Mbuzi-
Bi Nyau-
Nauliza Makunduchi ilikuwaje historian yake??? Mwenye habari tufahamishane wakuu😃😃😃😃 yalikiwa mangapi hayo Makunduchi?
 
Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?

Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.

Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).

Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.

Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.

Umenifahamu?
 
Mule ndani ya jengo la kamata kulikua na ofisi ya scandinavia na mpaka leo kuna basi zake....
 
Back
Top Bottom