Pale Barabara ya Msimbazi inapokutana na Barabara ya Nyerere, pamezoeleka kwa jina la "Kamata". Baadhi ya vijana, hawaelewi kwa nini panaitwa hivyo. Wengine mpaka wanajiuliza nani akamatwe?
Miaka ile ya zamani, serikali ilikusudia kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Na kufikia ndoto hiyo, ililazimu kukata "mirija" ya "makupe" wanyonyaji wote, yaani "mabepari". Na hivyo serikali kuanzisha biashara mbalimbali ili kufikisha huduma karibu kabisa na wananchi.
Mojawapo ya kampuni hizo ilikuwa ni kampuni za mabasi za mikoa, na lile baba lao, Kampuni ya Mabasi ya Taifa (KAMATA).
Hiyo kampuni ya KAMATA ilikuwa na makao makuu yake pale kwenye jengo lililo makutano ya Msimbazi/Nyerere.
Ndio kisa cha eneo hilo kujulikana kama KAMATA.
Umenifahamu?