Wakuu bila shaka uzima upo. Basi nashukuru pia poleni kwa wale uzima unapelea.
Leo nimeamua kuja mbele yenu kuuliza kwa nini Wazungu tu? Naamu hii inamaana ya kuomba msaada wa majibu kwenu.
Ukifuatilia Asili au Maana ya Maneno ya majina ya maeneo mengi hapa nchini utakuta na majina hayo asili yake au maana mzungu kuhusika ndani yake.
Mifano;
1-
Asili ya Neno Geita.
Geita imetokana na neno la kisubwa(kwa nadharia moja) yenye maana ya neno
Keita yaani kuuwa (kwa kisubwa). Hivyo hapo zamani watu waliokuwa wakipita milimani kuingia Geita walikuwa wakifia njiani hivyo wenyeji wakawa wanasema
Akabanga Keita Abhantu yenye maana
Mlima unauwa wafu (kwa kisubwa). Hivyo Neno Keita wazungu walishindwa kuita wakaita Geita na ndiyo ikawa mwanzo wa neno Geita.
2-
Asili ya neno Kilimanjaro
Zamani ilikuwa ikiitwa (
kilima kyar'yu)kwa kabila la kichaga yaani kilima chetu. Wazungu wakashindwa kutamka (kyar'yu)yaani chetu ndo wakaanza kuita kilimanjaro mpaka likazoeleka hivyo na hapo ikawa mwanzo wa neno Kilimanjaro.
3-
Asili ya neno Lukuledi mkoani Ruvuma
Lukuledi ni moja ya eneo lililopo mkoani Ruvuma asili yake ni kwamba maeneo hayo kulikuwa na mto hivyo wanawake walipenda kuoga maeneo ya mto, sasa wazungu wakipita pale wanaanza kuongea
Look Ladies hivyo na sisi Wabongo tukajua Hilo eneo bila shaka ni Look Ladies hivyo kwa vile kizungu hakikueleweka wao walijua ni Lukuladi sawa na Look Ladies na hapo ikawa mwanzo wa jina hilo.
4-
Asili ya Jina kolomije- Mkoani Mwanza
Kuna mzungu alikuwa anaitwa J. Hivyo kwa jinsi alivyokuwa alijitambulisha akawa anawambia
call me J akimaanisha niite J(kw kiswahili), basi hilo eneo likaitwa
kolomije na wenyeji walio Kuwa wakijua mzungu huyo anasema eneo hilo ni Kolomije yaani call me J.
Pia kuna maeneo mengine ambayo uwepo wake ni chanzo cha wazungu.
Je, bila wazungu tusingekuwa na majina ya maeneo yetu au kabla ya mzungu sisi hatukutambua umuhimu wa majina ya maeneo.
Wenu
Kasomi naomba majibu pia unaweza share stori ya chanzo cha eneo.