Wewe mzee ni vizuri kukubali tu kwamba umri umekwenda. Pokea shikamoo unazopewa na wadogo zako bila kujiuliza maana kwa umri wako 55+ ni mzee. Na hata shikamoo ikifa, uzee wako uko pale pale.
hivi na wewe umo kwenye orodha ya waliofuta ujinga? yaani umepost pumba kabisa badala ya kutoa mbadala unapost pumba. Kwa kadili nijuavyo mimi ni kuwa kuna watu hawjui maana ya shikamoo kwa sababu hawajawahi kanyaga hata darasa la kwanza. shikamoo ni salam ya heshima kwa wakubwa kama ilikuwa na utumwa ndani yake bac hiyo kwa leo haipo ila ni heshima kwa kizazi chetu, hutaki unaachashikamoo ni salamu ya wasio na hela kama watoto vile..! ndo'mana siajabu kukuta mzee anatoa shikamoo kwa kijana!!!
Kwahiyo unapendekeza salamu gani kwa wakubwa wenzako?
Salamu hii siipendi kabisa, ndio maana wadogo zangu hunisalimia salamu ya kidini (assalaam alaykm)
Heshima ni heshima tu shikamoo makelele. Tutafute salamu mbadala.
Wadau, labda ni vyema kushare nanyi suryey ambayo tuliifanya muda kidogo, nayo ni kuhusu salam ya 'Shikamoo'.
Katika suryey yetu tukagundua kuwa;
1. Watu wengi hawajui maana ya neno 'Shikamoo' zaidi ya kusema kuwa ni heshima, wengine wakasema ina maana ya 'nipo chini ya miguu yako'
2. Asili yake ni ya kitumwa,yaani walioinzisha hawaitumii kama salamu yao ya kawaida ila walioipokea ndio wanaitumia katika matumizi yao ya kila siku.
3. Ime simama katika kuangalia umri, kitu ambacho muda mwingine ni ngumu kujua au kukisia umri wa mtu sababu waweza muamkia mtu kumbe ni mdogo wako
4. Imejengwa katika nidhamu ya uoga, ndio maana ni rahisi kumkuta mtu mkubwa kiumri ana msalimu mtu mdogo kiumri sababu tu anayeamkiwa ana nguvu kubwa kifedha au kimadaraka.
5. Imepitwa na wakati, yaani wengine hawataki kabisa kuisikia ama wanajishusha umri, ndio maana mtu anaamkiwa anasema poa, au salama.
6.Imesababisha ugomvi au wengine kutosalimiana kwa sababu tu hakuna anayependa kuwa mdogo.
Wadau toeni mapendekezo yenu juu ya kile mliona na mnavyodhani juu ya suala hili...
Salamu hii siipendi kabisa, ndio maana wadogo zangu hunisalimia salamu ya kidini (assalaam alaykm) Heshima ni heshima tu shikamoo makelele. Tutafute salamu mbadala.
Tunajua na kukubali chanzo cha hii salamu ilikuwa ni utumwa, je kuna aina salamu gani inayoweza kutumika badala ya hii? kusema kweli nilichogundua Baba yangu tangu nikiwa mdogo huwa hataki kupokea shikamoo badala yake anataka tuwe tunamsalimia kilugha.
shikamoo ni salamu ya wasio na hela kama watoto vile..! ndo'mana siajabu kukuta mzee anatoa shikamoo kwa kijana!!!
Shikamoo ni xalamu ambayo haina maana ya heshima ilitumiwa wakati wa utumwa ikiwa na maana ya nko chini ya miguu yako lakin waswahili wakalichukulia kama neno linaloweka heshima kati ya mkubwa mdogo ndo maana hili neno halina tafsiri katika lugha zetu za kikabila ninavyoona hili neno lanakufa kwa xababu za utandawazi tu na hivyo bac hata baadhi ya wazee wetu hawaithamini tena!itafika sehemu hili neno litakuwa historia tu