Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Wewe mzee ni vizuri kukubali tu kwamba umri umekwenda. Pokea shikamoo unazopewa na wadogo zako bila kujiuliza maana kwa umri wako 55+ ni mzee. Na hata shikamoo ikifa, uzee wako uko pale pale.

Shikamoo ni kuonesha heshima kwa wakubwa tangu jadi. Utamaduni wa kizungu usituharibu.
 
shikamoo ni salamu ya wasio na hela kama watoto vile..! ndo'mana siajabu kukuta mzee anatoa shikamoo kwa kijana!!!
hivi na wewe umo kwenye orodha ya waliofuta ujinga? yaani umepost pumba kabisa badala ya kutoa mbadala unapost pumba. Kwa kadili nijuavyo mimi ni kuwa kuna watu hawjui maana ya shikamoo kwa sababu hawajawahi kanyaga hata darasa la kwanza. shikamoo ni salam ya heshima kwa wakubwa kama ilikuwa na utumwa ndani yake bac hiyo kwa leo haipo ila ni heshima kwa kizazi chetu, hutaki unaacha
 
Salamu hii siipendi kabisa, ndio maana wadogo zangu hunisalimia salamu ya kidini (assalaam alaykm)
Heshima ni heshima tu shikamoo makelele. Tutafute salamu mbadala.
 
Salamu hii siipendi kabisa, ndio maana wadogo zangu hunisalimia salamu ya kidini (assalaam alaykm)
Heshima ni heshima tu shikamoo makelele. Tutafute salamu mbadala.

Mbona hizo salam zote zimeletwa na Wenye dini yako... Waarabu
 
Nilipata msemo mmoja kuwa "heshima ni pesa shikamoo kelele tu".
 
vijana wa siku hizi hawataki kabisa kusikia wala kuambiwa mambo mazuri....ndio hawa waendao na wakati hadi wanaupita wakati wenyewe....... turudi ktk tamaduni zetu....shikamoo..mtu akija kuniambia maana ya niko chini ya miguu yako alipoitoa na asili ya neno hili ntamuelewa
 
Wadau, labda ni vyema kushare nanyi suryey ambayo tuliifanya muda kidogo, nayo ni kuhusu salam ya 'Shikamoo'.

Katika suryey yetu tukagundua kuwa;

1. Watu wengi hawajui maana ya neno 'Shikamoo' zaidi ya kusema kuwa ni heshima, wengine wakasema ina maana ya 'nipo chini ya miguu yako'

2. Asili yake ni ya kitumwa,yaani walioinzisha hawaitumii kama salamu yao ya kawaida ila walioipokea ndio wanaitumia katika matumizi yao ya kila siku.

3. Ime simama katika kuangalia umri, kitu ambacho muda mwingine ni ngumu kujua au kukisia umri wa mtu sababu waweza muamkia mtu kumbe ni mdogo wako

4. Imejengwa katika nidhamu ya uoga, ndio maana ni rahisi kumkuta mtu mkubwa kiumri ana msalimu mtu mdogo kiumri sababu tu anayeamkiwa ana nguvu kubwa kifedha au kimadaraka.

5. Imepitwa na wakati, yaani wengine hawataki kabisa kuisikia ama wanajishusha umri, ndio maana mtu anaamkiwa anasema poa, au salama.

6.Imesababisha ugomvi au wengine kutosalimiana kwa sababu tu hakuna anayependa kuwa mdogo.

Wadau toeni mapendekezo yenu juu ya kile mliona na mnavyodhani juu ya suala hili...

Shikamoo haina matatizo,Ni salamu imara ktk taifa letu.Hoja zako no.1-6 hazina mshiko,Zimebeba UJINGA tu,.Namaanisha kama mtu amepatwa na hisia au hali mojawapo ya hizo pointi zako uelewa wake ni mdogo [anatakiwa ajifunze na awe anafanya mambo ki uelewa]:

1.Kutokujua maana=Ujinga
2.Utumwa=Tumerithi vitu vingi kutoka kwa wakoloni,.kama shikamoo ilipitishwa na kukubaliwa kuiwekea maana bora ya kujenga heshima ktk jamii yetu na tukaikubali,hakuna kosa.
3.Kuangalia umri,Hiyo ni nzuri ndio maana zipo salam tofauti tofauti ktk umri tofauti,au unaolingana.
4.Nidhamu ya uoga ni Ujinga wa mtu binafsi.
5.Kupitwa na wakati:Mtu akiwaza hivyo ni mjinga,.Kujishusha umri kukwepa/kutoitikia shikamoo ni upumbavu!!Sio hoja ya kuibeza shikamoo.
6.Kuleta ugomvi;huo nao ni ujinga,watu tunatakiwa tuishi ktk uhalisia



Salamu hii siipendi kabisa, ndio maana wadogo zangu hunisalimia salamu ya kidini (assalaam alaykm) Heshima ni heshima tu shikamoo makelele. Tutafute salamu mbadala.

Gandias,Hapa linazungumziwa suala la kitaifa na sio la kifamilia wala dini,Hizo salam zako za kidini ambazo unazitumia zina mipaka na hazina nguvu ktk jamii yote,hazitofautiani na zile za kilugha cha makabila!!.Tuijadili 'Shikamoo" ambayo ni kiswahili ambacho hakibagui wala hakichagui kwa wa TZ wote.
 
Tunajua na kukubali chanzo cha hii salamu ilikuwa ni utumwa, je kuna aina salamu gani inayoweza kutumika badala ya hii? kusema kweli nilichogundua Baba yangu tangu nikiwa mdogo huwa hataki kupokea shikamoo badala yake anataka tuwe tunamsalimia kilugha.

Kwa nyie wanae ana nguvu ya kuwafanya mumsalimie kwa kilugha cha kabila lenu,.Ila huko mitaani anakubali na anaitikia hiyo salamu ya Shikamoo.Na kama huwa haitikii huko mtaani heshima yake mbele ya jamii itakua imeshuka sana,Ni nyie wanae tu ndo mnaemuheshimu.[Naomba uchunguze tena,waweza kugundua kitu]
 
Shikamoo ni xalamu ambayo haina maana ya heshima ilitumiwa wakati wa utumwa ikiwa na maana ya nko chini ya miguu yako lakin waswahili wakalichukulia kama neno linaloweka heshima kati ya mkubwa mdogo ndo maana hili neno halina tafsiri katika lugha zetu za kikabila ninavyoona hili neno lanakufa kwa xababu za utandawazi tu na hivyo bac hata baadhi ya wazee wetu hawaithamini tena!itafika sehemu hili neno litakuwa historia tu
 
Heshima yako ndio salam inayochukua nafasi ya shikamoo ckuhizi.
 
Sote tunakiavwatu watatu. Aliyekuzidi cheo. Unaye mhofu na Unayempenda.Basi ukikuta mtu anasalimia mtu tofauti ha hao, basi utarajie kuwa kasoro kubwa iko kichwani mwa mtu huyo na hasa hasa tarajia uchizi siku zijazo kwa mtu huyo.

Hivi ni nani anayempa shikamoo kila mpita njia kama si wehu? Basi ukiona mtu humpa shikamoo huyu na humwacha kumpa yule ujue mtu huyu anajitambua na anajua maana ya kuamkia.
 
Shikamoo ni xalamu ambayo haina maana ya heshima ilitumiwa wakati wa utumwa ikiwa na maana ya nko chini ya miguu yako lakin waswahili wakalichukulia kama neno linaloweka heshima kati ya mkubwa mdogo ndo maana hili neno halina tafsiri katika lugha zetu za kikabila ninavyoona hili neno lanakufa kwa xababu za utandawazi tu na hivyo bac hata baadhi ya wazee wetu hawaithamini tena!itafika sehemu hili neno litakuwa historia tu

Good point. Umejibu vizuri na umeeleweka. Ila kwa sababu zisizo na msingi kwenye S umeweka X nimekupuuza.
 
Shkamoo salamu ya wototo ya kuombea Pesa, unakutana na mtoto wa shule anakupa shkamoo ya nguvu hujakaa sawa unaombwa shs mia hahhahaha
 
Back
Top Bottom