Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Asili ya maneno 'Shikamoo' na 'Marahaba' ni utumwa, kwanini tunaendelea kuyatumia?

Unakataa nini wakati jibu huna? ndio yale Allah Yupo ukiuliza wapi hajui

Si unaona ulivyo punguani. Unashindwa kuelewa shikamoo utaelewa mengine?

Mimi nnakwambia maana ya shikamoo nnaijuwa na haihusiani na utumwa hata chembe.

Huo utumwa ulikuwa kwenu tu?
 
Mimi nadhani sisi waswahili hatujaibeba shikamoo kwa maana ya kitumwa wala kiudhalilishaji bali tumeichukua kama alama ya heshima kwa yule mtu aliyekuzidi umri.....ni kama zilivyo alama zingine za heshima kama ilivyo kupiga magoti kwa baadhi ya makabila pindi wasalimianapo hapa nchini....kwa hiyo sidhani kama ni ishara ya utumwa kwa wakati huu......
 
Si unaona ulivyo punguani. Unashindwa kuelewa shikamoo utaelewa mengine?

Mimi nnakwambia maana ya shikamoo nnaijuwa na haihusiani na utumwa hata chembe.

Huo utumwa ulikuwa kwenu tu?
Kwetu Ehiopia Hatujawahi Tawalaiwa wala Kutumwa... na tumekuja kuendup Germany East Africa Utumwa ushaisha...

Acha Kujishebendua weka Maana uijuayo hapa na sio Porojo
 
Kwetu Ehiopia Hatujawahi Tawalaiwa wala Kutumwa... na tumekuja kuendup Germany East Africa Utumwa ushaisha...

Acha Kujishebendua weka Maana uijuayo hapa na sio Porojo

Hata ardhi hii ya leo unayoiita Tanganyika iliwahi kuwa himaya ya Habash aka Ethiopia.

Kumbuka hilo kijana.

Shikamoo ni heshima tu, hakuna zaidi.

Utumwa ni ule wa wanawake kuwapigia magoti wanaume wanaposalimiana. Mpaka leo hii upo hata hapa kwetu.
 
MwanaFalsafa1 said: ↑

Nakubaliana wewe kwa 100% kwa sababu maana ya shikamoo haijabadilika Ni ile ile ya "niko chini ya miguu yako", lazima tuukubali ukweli kuwa shikamoo haina maana yoyote ya kiheshima.
Hili ni jukumu la wizara ya Utamaduni, bahati mbaya wapo wapo tu kupanga bajeti na kutayarisha majibu ya maswali bungeni.
 
Hata ardhi hii ya leo unayoiita Tanganyika iliwahi kuwa himaya ya Habash aka Ethiopia.

Kumbuka hilo kijana.

Shikamoo ni heshima tu, hakuna zaidi.

Utumwa ni ule wa wanawake kuwapigia magoti wanaume wanaposalimiana. Mpaka leo hii upo hata hapa kwetu.
Mkuu, umenikuna mno kuona una ufaham wa historia lakini umenifedhehesha sana kutoelewa maana halisi ya neno 'shikamoo'. Ninavojua mie neno hili ni la Kireno na lilitumiwa na hao jamaa wakati wa mapito yao nchi mwetu kwa kutoa msamaha kwa wazee wetu kwa makosa waliyotendewa kama adhabu. Kwa mfano mtoto wako (samahani kama unae) akikukosea badala ya kumuadhibu mathalan kwa kiboko au kupiga magoti basi unamwambia 'shikamoo' yaani akuguse unyayo wako wa mguu ili umsamehe. Sasa ajabu ni pale baba au mama anapomlazimisha mtoto atamke neno hilo kwa maana ya mtoto kumwambia baba au mama yake amshike unyayo wa mguu ili amsamehe. Neno 'marhaba' ni la kiarabu.
 
Tukishaitoa hiyo shikamoo,
Je tutakua tunawasalimia vipi wakubwa waliotuzidi umri?
Mbona salaam zipo nyingi tu mkuu? Habari ya asubuhi, habari ya mchana, umeamkaje n.k. Kwa hili ni mdogo kutangulia kumsalimu mkubwa.
 
Mbona salaam zipo nyingi tu mkuu? Habari ya asubuhi, habari ya mchana, umeamkaje n.k. Kwa hili ni mdogo kutangulia kumsalimu mkubwa.
Aah huo mtihani,
Bora wengine tushawazoesha 'Asalaam aleykum' yatosha,
Ila mswahili umwambie habari ya asubuhi bila shikamoo atakuelewa kweli?

Bora tuendelee tu,
Hatudhuriki kitu.
 
Aah huo mtihani,
Bora wengine tushawazoesha 'Asalaam aleykum' yatosha,
Ila mswahili umwambie habari ya asubuhi bila shikamoo atakuelewa kweli?

Bora tuendelee tu,
Hatudhuriki kitu.
Mkuu, hapo 'bolded' sikubaliani nawe asilan. Tunapaswa tuwe makini kwa kila jambo.
 
Je ni nan mwanzilishi ya hii salamu
Je lengo lake lilikua nin katika jamii
Je ni kweli ndo kipimo cha mtu mwenye nidhamu ndani ya jamii
Kwann kijana au mtoto mtoto usimpo mwambia mkubwa wako iy salamu waonekana huna nidhamu?
Kwann mdogo ndo aseme shikamoo halafu mkubwa ndo aitikie marahaba?
Na mbna dhamani wanafunzi tulisalimia kwa kusema Kauli ya Kulinda na kuendeleza Mapinduzi shikamoo Mwalimuu huku tumeweka dole gumba kwenye paji la uso?
Je mwanzilishi wake alikua amebase kwenye Siasa?
Yapo mengi kuhusu hii salamu ila leo tujuzane ayo machache kwanza...
 
Nakumbuka marehemu baba 'angu mkubwa aliwahi kunidokeza historia ya hii salamu lakini akili yangu iligoma kukubaliana nae.Aliniambia kwamba SHIKAMOO maana yake NIKO CHINI YA MIGUU YAKO.Ni salamu ya kumsalimia mfalme kipindi hicho.Mfalme atajibu MARAHABA akimaanisha ENDELEA KUWA HIVYO HIVYO;kwa maana aendelee kuwa dhalili mbele yake.Na akanieleza kuwa hii ni kwa sababu wafalme kipindi hicho walijiona kama Mungu kwa hiyo walijiona ni wa hadhi ya pekee.Hatimaye utamaduni huu 'wa hovyo' ukarithiwa na jamii zetu mpaka leo.
 
na huo ndo ukweli mkuu ni salamu ya kimwinyi hiyo
 
Back
Top Bottom