Asili ya Msemo "Underdog"

Asili ya Msemo "Underdog"

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Tanzania, kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Afrika na duniani, tunapenda sana mpira wa miguu. Mchezo huu umekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wetu, ukijumuisha shangwe, mazungumzo na matumaini ya kila siku.

Miongoni mwa misemo maarufu inayotumiwa na mashabiki, wachambuzi wa soka, wataalamu, na makocha ni neno "underdog."

Mfano ni sledi hii Kwa jinsi AFCON inavyokwenda, sitashangaa underdog team kunyakua taji hilo la Afrika mwaka huu.

Asili ya Msemo "Underdog"​

Asili ya msemo huu inarudi nyuma kwenye karne ya 17 hadi ya 19 huko Marekani na Uingereza, wakati wa ujenzi wa majahazi na Meli kubwa yaliyotumika kusafiri duniani kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na usafirishaji. Ujenzi wa meli na majahazi hayo ulihitaji mbao ngumu zilizokatwa kwa usanifu mkubwa.

Katika zama hizo, kulikuwa na kundi la wafanyakazi waliokuwa wakipasua mbao kwa kutumia misumeno ya mikono. Kazi hii ilihitaji watu wawili – mmoja alikuwa juu ya mbao akivuta msumeno kwenda juu na chini, huku mwenzake akiwa chini ya mti mkubwa uliokatwa, akivumilia vumbi, uchafu, na ugumu wa kazi.

Yule aliyekuwa chini, ambaye alijulikana kama "underdog," alichukuliwa kuwa yupo kwenye nafasi ngumu zaidi na alikuwa ndo mnyonge wa game ya kuchana mbao.

Kwa wale mliowahi au ambao mnaishi maeneo kama Mufindi, Rungwe, Makete, au Muheza, mtakumbuka jinsi kazi ya kupasua mbao kwa njia hii ya jadi ilivyokuwa ngumu hasa kabla ya kuenea kwa mashine za kisasa kama zile za Amec za Kichina. Jamaa huwa wanakula ugali mgumu kama jiwe na maharage chukuchuku.

Katika miaka ya 90 kurudi nyuma, kazi hiyo ilikuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa wengi wanaojihusisha na kazi za mbao.

Maana ya "Underdog"​

Kwa muktadha wa sasa, msemo huu umetafsiriwa kumaanisha mtu au kundi linalodharauliwa au kutarajiwa kushindwa lakini linaweza kushangaza na kufanikiwa dhidi ya matarajio.

Kinyume chake ni "top dog," anayehesabiwa kuwa na nafasi bora zaidi. Kwa mfano unaweza kusema "Yanga ni top dog".

Kwa hivyo, msemo wa "underdog" umeendelea kuwa kipenzi cha mashabiki wa michezo, hasa mpira wa miguu, tunaposhuhudia timu zisizotegemewa zikifanya maajabu uwanjani kama alivyofanya Yanga jana kumchapa Fountain Gates 5 - 0 bila mtu yeyote kutarajia.

images (1).jpeg
 
View attachment 3188602
Okay elimu nzur
 
Back
Top Bottom