Asili ya neno Mungu ni nini?

Asili ya neno Mungu ni nini?

Unataka kusema Allah, Mungu, Ruwa, Nguluvi, Kyala, God nk nk ni kitu kimoja?
Ikiwa hao wanaomuamini wanakiri kwamba ni wa vyote bila upendeleo na ndiye muumba wa vyote then in essence ni mmoja. Sema jina wanalotumia kukitaja hicho cheo ndio watatofautiana.

Halafu kakaa mbona ni kawaida tu kumtaja aliye mkubwa zaidi yako kwa cheo fresh tu bila jina; mfano kaka, baba, mbunge au mheshmiwa rais. Ni heshima tu.

Kikawaida jina tunavipa vitu na wadogo zetu mfano Adamu alivipa majina viwanyama vyoote. Au kitu ulichotengeneza unakiita jina unalotaka.
 
Tena mantiki ya kawaida tu inaonesha tunavipa majina vitu ili kuvitofautisha, na tunajaribu kuvitofautisha kwa sababu vinafanana in the first place! nitafafanua;

Ikiwa tupo jimboni na mbunge wetu ni mmoja ni kawaida tu watu wa halmashauri kusema mbunge atakuja leo, mbunge amesema tutoe ripoti etc etc. Au rais atatutembelea.

Lakini wakikaa kikundi cha wabunge utasikia - Mbunge wa jimbo la mashariki bwana JOHN XXX YYY ametoa hoja. Lakini kwa rais hata wakiendelea tu kusema mheshimiwa rais inatosha labda wawepo na marais wengine kumtofautisha na waliopita na wa nje basi jina linafaa.

Tukija kwa Mungu ambaye ni mmoja na hafananishwi niambie hapo kuna haja gani ya kumpa jina? kumtofautisha na nani?
 
Note: Mungu wa kweli ni mmoja Muumba wa vyote vyenye kuonekana na visivyoonekana, wa milele, mweza yote,mjua yote, afanyaye kila jambo kwa shauri la mapenzi yake pekee, mwenye uwezo wa kuua na kuhuisha hata roho (je Mungu wako ana fit hapo?) Kama hatoshani na sifa hizo tafakari kisha chukua hatua.
Naomba kuwasilisha.

NAKAZIA
 
Ungulubhi ni wa Mwalyego, Mwalyoyo na Mwalyoto😀😀😀. Haya ya kumuhamisha kumaanisha wa Yakobo ni upotoshaji.
 
Back
Top Bottom