mkuu
story yako inafanana na tukio lililowahi tokea kule kwetu mbinga-songea ambako bila shaka yeyote 99.9% ya wenyeji ni wakristo.
naambiwa kuna mwaka mmoja hivi karibuni aliibuka muislamu mmoja toka dar na pesa kibao alizopewa na waarabu ili ausambaze uislamu mwambao wa lake nyasa sambamba na kujenga misikiti.
basi alipo wasili tu,akapokelewa na wenyeji baada ya kueleza lengo lake,aka itisha mhadhara na vijana walihudhuria.wale vijana wakamwabia kama issue ni kupata tu waislamu ili upeleke report kwa waliokutuma,kwanza tupe chetu.
basi jamaa akatoa pesa,kanzu na barakashia kwa wale vijana. na kweli kwa zile wiki mbili ambazo yule msambaza uislamu alizoshinda nao,walijifanya kama wamesilimu.
story ni ndefu,ila mpaka wakati huu,wale vijana wote wamebaki na ukristo wao.hakuna hata mmoja aliye silimu.wana subiri neema itokee aibuke tena muislamu mwingine ili wapige pesa.imekuwa ni kama mradi wa pesa za uchaguzi.hahaha