Asilimia 13 fixed bank Vs UTT - kwa sasa wapi bora?

13 fixed account? Tena 45m peke yake?

Kwa Sasa ilitotangaza riba kubwa ni TCB 11% sasa hiyo ya kwako ni bank gani?
 
ni kweli lakini kama unamtaji mkubwa kwanini usiende BOT ambapo na hao UTT wanawekeza? na bado unaweza kukopa benk dhamana hiyo ukanunua hisa zingine za thamani labda 30mil na instalment yake ikawa inalipa deni kila baada ya miezi sita na riba yake haitakuwa sawa na mikopo mingine ya biashara.
 
BOT si ni mpaka watangaze lakini? Ukitaka kununua sasa hivi bila kutangazwa inabidi ununue kwenye secondary market ambapo ni kama bank kawaida tu
 
ni kazi sana kuwasaidia maskini na tatizo lao wanaangalia hela ya leo tu
 
Sawa lakini siyo primary market ,hiyo inakuwa secondary market
issue za Primary na Secondary Market hazipo BOT hizo zipo DSE. Huku ni serikali inauza hati fungani iliiweze kufinance activitiy zake au wakati mwingine inaweza kufanya hivyo kupunguza mzunguko wa hela mtaani.
ingia web ya BOT
 
Kama umeajiriwa na bado kijana pia bado hujajua ufanye nini nje ya kazi yako basi nenda UTT fungua akaunti anza kuweka
Pesa kidogo kidogo baada ya 3-5 yrs utapata mtaji mzuri sana. UTT wana mifuko mbalimbali na watakuelekeza.
Je UTT wana matawi mikoa gani?
 
wewe mtoa ushauri unazo hizo 45m ngapi ..au ndo nawewe unamuita huko Pm ukamvune hio pesa kwa jina la consultancy fee .?
Huitaji kuwa na nyumba ili uitwe fundi na si kila mtu anahitaji taarifa zilizo kitaalam zaidi na baadhi ya taarifa zinaweza kuwa hazitakiwi kuonekana na wengi.
hivyo akienda huko anaweza kumsaidia zaidi swala la fee ni maelewano lakini utakuwa mtu wa ajabu unayetaka kuwekeza mil45 halafu huwezi kulipia gharama za ushauri pale unahitaji
 
Mkuu wewe UTT inakufaa.. Kama una 40m inatosha sana kwa kuanzia Bond Fund, utakuwa unapata dividend kila mwisho wa mwezi na hiyo pesa waweza itumia kama collateral bank kupata mkopo
Ukiweka hiyo 40M unapata kiasi gani kila mwezi kama dividend? Tuanzie hapo kwanza ndugu, ili nione kama kuna faida ya KUITELEKEZA hiyo milioni 40 huko UTT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…