Asilimia 60 chali matokeo ya kidato cha nne

Habarin wanajamvi,

Baada ya matokeo kuwa mabaya serikali imeanza kukubaliana na madai ya walimu.

Rafiki yangu mwalimu wilaya ya Bagamoyo na alipata ajira February 2012, Amepeta taarifa jana pesa za malimbikizo ya mishahara miezi mitatu majina yametoka.

Leo anasema kuwa wanatakiwa wapeleke TSD namba kwa ajili ya kupandishwa madaraja.

Je huko kwingine imekaaje?
 
Mitaala je????

Mitaala hiyo hiyo mibovu lakini kuna waliofanya vizuri tu,kwa hiyo sidhani kama mitaala itakuwa sababu kubwa japo inaweza kufhangia,ila mwaka huu hali ni mbaya sana haijawahi kutokea,labda kwingine tuangalie upya elimu yetu,maana mtu akipata 4 ndio anakwenda kusomea uwalimu sasa hapo sidhani kama kuna jipya,yeye mwalimu kapata 4 unadhani mwanafunzi wake atapata nini kama sio ziro?
 
Kama ni kweli basi pia waliondaa marking scheme nao wana upungufu flani hivi
 
Warudi darasani kwa gharama zipi,
mishahara tu ya watumishi inaielemea nchi,
la maana wahusika wajivue madaraka wakianzia ngazi ya juu hadi ya chini.
Mkuu sikuamini pale Waziri alipotokeza mbele ya waandishi wa habari huku anatabasmu kama vile hakuna baya lilotokea. Kiongozi wanamna hii hafai kabisa. Hoja ya Mbatia ilikuwa na mshiko na hivi sasa atajizolea umaarufu mkubwa. Haishangazi kama naibu waziri aliwahi kusema Tanzania ni muunganiko wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe unategemea nini kwa watoto wetu? Kama ile presentation ingekuwa ni mtihani waziri siku ile angekuwa kwenye hili kundi la 60%.:A S 39:
 
Kashfa Nzito
MATOKEOya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambaoni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisemawatahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa68,806.

"Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana nahali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hilitatizo," alisema Dk Kawambwa.
DkKawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 katiyao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa naasilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44,wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.

Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa naasilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihanihuo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.

Ufaulu kwa madaraja
Kwamujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641,wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulanawakiwa 4,456 na wasichana 1,997. Waliopata daraja la tatu ni 15,426, wavulana 10,813 na wasichana 4,613,waliopata wa daraja la nne 103,327, wavulana 64,344 na wasichana 38,983 hukuwaliopata sifuri wakiwa 240,903, wavulana 120,664 na wasichana 120,239.

Shule 20 bora
Katikahali isiyokuwa ya kawaida, wizara ilitaja shule 20 zilizofanya vizuri badala ya10 kama ilivyozoeleka, kati yake 18 zilikuwa za watu binafsi na mashirika yadini na mbili za Serikali.Shule hizo ni pamoja na St.Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, FezaBoys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Rosmini ya Tanga, Canossa ya Dares Salaam, Jude Moshono ya Arusha, St. Mar's Mazinde Juu ya Tanga, AnwariteGirls ya Kilimanjaro na Kifungilo Girls ya Tanga.

Nyingine ni Feza Girls ya Dar es Salaam, Kandoro Sayansi Girls ya Kilimanjaro,Don Bosco Seminary ya Iringa, St. Joseph Millenium ya Dar es Salaam, St.Iterambogo ya Kigoma, St. James Seminary ya Kilimanjaro, Mzumbe ya Morogoro,Kibaha ya Pwani, Nyegezi Seminary ya Mwanza na Tengeru Boys ya Arusha.

Shule 10 za Mwisho
Kwaupande wa shule 10 za mwisho, iliyofanya vibaya zaidi ni Mibuyuni ya Lindi,Ndame ya Unguja, Namndimkongo ya Pwani, Chitekete ya Mtwara, Maendeleo ya Dares Salaam, Kwamndolwa Tanga, Ungulu Morogoro, Kikale ya Pwani, Mkumba naTongoni za Tanga.

Matokeo yaliyofutwa
Jumlaya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja naudanganyifu na kuandika matusi.
Baadhi ya udanganyifu huo ni karatasi za majibu kuwa na mfanano usio wakawaida, kukamatwa na simu za mkononi kwenye chumba cha mtihani, kukutwa nakaratasi au madaftari pamoja na kubadilishana karatasi za majibu.
Dk Kawambwa alisema matokeo ya watahiniwa 28,582 yamezuiwa kwa sababu yakutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja.

Matokeo ya QT
DkKawambwa alisema waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) walikuwa 21,310,wasichana 13,134 na wavulana 8,176 na waliofanya ni 17,137 sawa na asilimia80.42... "Watahiniwa 5,984 kati ya 17,132 waliofanya mtihani huo wamefaulu."

Source: Mwananchi
 
Spika na naibu wake pamoja na uongozi wa bunge kwa ujumla, kama hata vijana wetu wa miaka 19 hadi 20 wanaliona Bunge letu kama ni kijiwe ni hatari sana.

Watoto wanalalamikia mfumo wa elimu, wananchi wanalalamika, waalimu wanalalamika, wadau wa elimu wanalalamika, wasomi wanalalamika wazazi wanalalamika. Mbunge anajitokeza kwa nia njema kuleta hoja bungeni tuujadili mfumo wetu kwa ujumla wetu, Bunge linaungana na serikali kusema hakuna haja.

Mtahiniwa badala ya kujibu maswali kumpima uelewa wake kwa miaka 4 aliyokaa darasani yeye anaandika hivi, tunakwenda wapi as a nation?

nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…"
"
 


Kuna mengi mno yanayochangia, hati kutengamaa ipo kazi. Kwa mwendo huu wanafunzi wanaenda darasani.
 
pinochet,
waalim waliandamana wakiomba kanyongeza ka mshahara wakatishiwa usalama wa kazi zao,
waziri nae ni cheti cha kuunga unga,
mwenye nchi watoto wake wanasoma shule gani sijui (Feza)


 
Last edited by a moderator:
Matokeo haya ni msiba wa taifa, kwanini bendera haipepei nusu mlingoti, maana kila familia yenye mtoto aliyemaliza kidato cha nne mwaka 2012 wanalia na haya matokeo! Halafu Mulugo na Kawambwa wapo tu wanavinjari na mashangingi ya Umma!
 
Kijana zermarcopolo ni msomi mzuri tu DR kwa proffessional lakini hana akii kabisa siku hizi nae kaingia kwenye peyroll ya nape inatia huzuni sana.Elimu yake haijamsaidia chochote yeye anafikiria kwa kutumia tumbo.Nape mwaka huu lazima atawaoa wee ngojeni kama mwanaume unalipwa kuandika utumbo kwenye internet siku si nyingi utalipwa kuinamishwa coco beach na kupigwa nao
 
Matokeo haya ni msiba wa taifa, kwanini bendera haipepei nusu mlingoti, maana kila familia yenye mtoto aliyemaliza kidato cha nne mwaka 2012 wanalia na haya matokeo! Halafu Mulugo na Kawambwa wapo tu wanavinjari na mashangingi ya Umma!

Mkuu umenena kweli, hili ni janga la kitaifa, lakini bendera nusu mlingoti haitobadili chochote......cha msingi ni serikali kupitia wizara kuwajibika. Kawambwa na wenzake waachie ofisi na kama wanakaidi basi after two weeks alizowapa Mbowe, tuingie barabarani tuwatoe kwa nguvu.
 
Matokeo haya ni msiba wa taifa, kwanini bendera haipepei nusu mlingoti, maana kila familia yenye mtoto aliyemaliza kidato cha nne mwaka 2012 wanalia na haya matokeo! Halafu Mulugo na Kawambwa wapo tu wanavinjari na mashangingi ya Umma!
mbaya zaidi waliofeli ni watoto wa walala hoi kwenye zile shule za kata.
 
Kama huku ni balaa hivi. Huko kutakuwaje?? Kazi kweli kweli..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne, yaliyotangazwa na Baraza la Mtihani NECTA!! yanaonyesha kuwa shule hizi kumi ndizo zinazo vuta Mkia!

(1) MIBUYUNI, ya ZANZIBAR, (2)NDAME YA UNGUJA (3)NAMNDIMKONGO YA PWANI. (4)CHITETEKETE YA MTWARA. (5)MAENDELEO YA DAR. (6)KWA MNDOLWA TANGA. (7)UNGULU MOROGORO. (8)KIKALE YA PWANI. (9)MKUMBO YA TANGA. (10)TANGONI TANGA!

Nacho jiuliza je ni kwanini shule hizi ndizo zimekuwa za Mwishoni, je ni kwa ajili ya kwamba watu wengi wa Mikoa hii,huthamini zaidi wanachokiita ELIMU AKHERA, na sio ELIMU DUNIA? ,Au baraza la Mitihani taifa NECTA wamehujumu hizi shule?

NB :
Mikoa hii ndio Ngome za Ccm,na kwamba watu wa mikoa hii bado hawana uelewa wa kutosha na ndio,maana Mkoa kama Tanga Pwani na Morogoro, hazijawahi kuchagua Mbunge wa Upinzani, tangia kuanzishwa kwa Mfumo wa vyama Vingi 1992!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…