Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Kusema kweli mimi nilifanya kazi nyingi ktk wilaya za mkoa wa Pwani (sijui upande wa Zbar) kwa zaidi ya miaka 6 sasa. Na nilifanya kazi na walimu na wanafunzi wa shule za misingi na sekondary.
Sishangai na matokeo haya kwa upande wa mkoa wa Pwani kwa sababu wanafunzi wengi sana kuanzia kidato cha pili wanaanza kufikiri kuolewa kuliko kuendelea na shule. Hii pia inatokana na utamaduni wa kucheza watoto wa kike /kumtoa mwali (mkoleni) ambao kisaikolojia unamfanya afikirie masuala ya Ndoa kuliko Shule baada ya kutolewa mwali.
Niliwahi kufanya kazi na Diwani mmoja msomi kidogo mzaliwa na wa Pwani (mzaramo) akawa anapinga ngoma hizi za asili kwa hoja kwamba inaharibu watoto wa kike. Matokeo ya msimamo wa Diwani huyo kuangushwa ktk hatua za kura ya maoni ya chama chake 2010.
Japokuwa ukizungumzo na watu wazima wanapinga kwamba wanahamasisha tabia mbaya kwa watoto wao lakini ukweli utabaki pale pale kwamba Mkoleni au kutoa mwali ni utamaduni unaohitaji kubadilishwa ili kuboresha mfumo wa Elimu. Watoto wa kike baada ya kutolewa mwali matokeo yao yanabadilika darasani na hili hata waalimu wanashuhudia kabisa. Matokeo yake sasa naona hata waalimu wanaanza kukata tamaa.
Sikubaliani na madai ya hujuma ktk baraza la mitihani kama alivyodokeza mleta mada.
Hivi hao 7% waliopata div 1-3 tanzania nzima ni wa kutoka mikoa ipi? Kuna tatizo kubwa sana na lazima lijadiliwe kwa kina na sio kutupia mikoa fulani.
Mtu yeyote anayetoka na kushangilia kuwa waislam ndio waliofeli kwa hii 7% ya div 1-3 huenda amefungwa na kiakili.

