Asilimia 60 chali matokeo ya kidato cha nne

Kama aongozae chombo cha elimu anashindwa kutofautisha kati ya Zanzibar na Zimbabwe....sembuse wanafunzi wake kufaulu ????

Tafakari....................chukua hatua.................chagua CHADEMA 2015

Hivi ndivo watanzania wataendelea kujidanganya. badala ya kuwamasisha watoto wao kujenga tabia ya kujisomea, wanakaa na kufkiri siasa. Hivi Chadema ya akina SUGU, NYERERE, WENJE itafanya nini katika ulimwengu huu wa utandawazi. Mwarobaini wa elimu nzuri kamwe hauwezi kuwa serikali kama, tutawaacha watoto wachore katuni wakiwa kwenye vyumba vya mitihani, kama hatutajenga tabia ya kukagua madaftari ya watoto wetu kila watokapo shule, kama hatutapiga marufuku watoto wetu kushinda kwenye internet cafe na kuwapa simu za mikononi na kuwasiliana kimapenzi wawapo madarasani. Tutarushia mawe hawa CDM kwa tunafikiri tatizo ni CCM, hawa wakishika nchi tukiwa bado na mawazo ya kuwa mwarobaini wa elimu ni serikali hakika hata mwaka mmoja hawatamaliza
 
Kama aongozae chombo cha elimu anashindwa kutofautisha kati ya Zanzibar na Zimbabwe....sembuse wanafunzi wake kufaulu ????

Tafakari....................chukua hatua.................chagua CHADEMA 2015

Kwa hiyo hii imekuwa sera kujipatia kura 2015? kazi ipo watu wanalala wanaota uongozi.
 
Nadhani wewe ni miongoni mwa wanafunzi waliochora katuni wakiwa kwenye chumba cha mtihani na hapa ndiyo mwisho wako wa kufikiri.

Ungejua mimi nimesoma shule enzi gani (miaka ya zamani) na wapi (kijijini Katavi) usingehangaika kwenda fikia huo upeo wa kuwaza. Kwa kukuelimisha tu ni kuwa, hii katuni ya Mheshiwa Naibu Waziri iliwekwa kwenye media za Tanzania mara tu alipoborongonga huko South Africa. Tanzania is a Union of Tanganyika and the Islands of Pemba and Zimbabwe in 11964. Cheka unenepe!!!
 
........Mjomba nakushukuru sana... zemakopolo ujumbe ameupata!!!
 
Mfumo wetu wa elimu inabidi ufumuliwe upya Tume ya Makweta (RIP) inahitajika zaidi sasa kuliko hata wakati ilipofanya kazi yake
 
Bila shaka ni binadamu wachache sana katika ulimwengu wa leo ambao hawakupitia mikononi mwa mwalimu. Mwalimu ni mlezi, tabibu, afisa wa afya, hakimu, mnasihi, kasisi, askari polisi, mtetezi wa haki za wanafunzi na mambo mengine yote mazuri ambayo kimsingi hutakiwa kuyarithisha kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Fikiria mtoto wa chekechea na (nursery and Kindergatten) akiwa na miaka mitatu anakabidhiwa kwa mwalimu: mwalimu ndiye anayetakiwa kumhudumia anapojisaidia, akiugua, au apatwapo na madhila yoyote wakati mzazi akiwa anaendelea na shughuli zake. Fikiria kwa mwalimu anayemlea mtoto hadi anafikia shule ya msingi, sekondari mpaka vyuo endapo atakengeuka kimaadili akaamua kutema sumu kwa watoto hawa tangu wakiwa wadogo matokeo yake nini.

Namshukuru Mungu kuwa mimi mwenyewe ni mwalimu na ninaipenda kazi hii kwa dhati. Hata hivyo, kutokana na utafiti wangu (action research) kazini nimegundua kwamba moyo wa walimu waliowengi kujituma kwa ajili ya kazi hii umepotea. Waulize walimu wanaoajiliwa leo mtazamo wao kuhusu kazi hii! Ukiwasikia hutatamani kuwauliza tena na utagundua kuwa inahitajika hatua zichukuliwe ili kunusuru hali hii. Wengi hujilinganisha na wenzao waliosoma fani nyingine na kujikuta wako nyuma kimaendeleo na jamii inawabagua. Kwa walio wengi ukijilinganisha fani kama benki, tra, ardhi, kilimo, afya, bandari n.k. Hadhi ya mwalimu ni duni mno katika jamii ya kitanzania na wengine hawapendi kujitambulisha kama walimu. Ukiangalia vigezo vinavyoleta tofauti havieleweki. Kwa mfano: mtu anafaulu darasa la saba vizuri, kidato cha 4 anatoka na division anazoziheshimu kawambwa (i, ii au iii) sawa na fani nyingine. kidato cha vi hivyohivyo isipokuwa kosa ni kuchagua kusomea ualimu iwe ni masomo ya sayansi ama sanaa maana yake atakuwa amepoteza mwelekeo. Yule atayepata four akaenda Nursing, chuo cha sheria Lushoto ameula au kujiunga na jeshi la mganbo kisha akaajiriwa tanesco, bandari, benki, tanapa, huyo kaula. Ila mwalimu na digrii yake ya mathematics na phisics ni cha mtoto mbele ya mwenye credit moja iliyompeleka unesi au ukarani wa mahakama! Hata atm card alishakabidhi kwa mkopeshaji mwenye riba kubwa ambalo ni dili la wakubwa.

Ole wa nchi hii ambayo inakausha maeneo oevu kwa mazoea ya umangimeza maana itavuna sawasawa na matendo yake. Unawezaje kuwadharau watu wanaoshikilia amali za nchi ili kuzirithisha kwa watanzania wa sasa na kizazi kijacho? Nenda Cuba, China, Japan na nchi nyingine zisizoruhusu usanii! Ualimu ni title! Mwalimu akikuta mahali huduma fulani ya kungojea kwa kujipanga utasikia anahimizwa apate kwanza ili awahi kwenye kazi yake. Kama hatutajifunza kwa hili, tukafikiri mahakama, ukatili wa mwajiri, mifumo ya kiutawala kama OPRAS ndilo jawabu basi tutarajie maajabu mengine KWA MAANA KUDHULUMU WALIMU NI SAWA NA KUKAUSHA VYANZO VYA MAJI KWANI CHEMICHEMI ZIKIKOMA NDIO MWISHO WA MAVUNO BORA.
 
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.
Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva).

“Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.
“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema.

Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.

Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.

Sababu za kufeli
Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa.

Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu.

“Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.”

Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea.

“Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli,” alisema Dk Ndalichako.
 
mleta mada, hiyo sio ishu ndugu. tumo ndani ya janga kubwa, na tunaelewa hivyo.
Ishu ni kwanini kijana wa form 4, aliyesoma miaka 4, afikie hatua ya kufanya madudu hayo. ishu ni MSINGI WA TATIZO. Tumefikaje hapo? kwa hiyo usijaribu kututoa kwenye reli, au kupotoshwa mwelekeo na huyo mtu wa Baraza. Tunajua pa kulenga.samahani lakini.
 
Lowassa kasema ana kipaji.Ndo Rais wetu huyo wa kesho
 
Awali ya yote napenda kutoa pole kwa vijana wetu wale ambao walikuwa wamejitosa kwa lengo moja tu la kupanda ngazi ki-elimu, lakini ghafla wamejikuta wakirudi nyuma kwa kasi ya ajabu sana na wengine hata kuwaghalimu maisha yao kupotea hivi hivi!!

Ninapotoa tahadhari ya kuliangalia suala hili kwa macho ya zianda, ni baada ya mikanganyiko kuanza kujitokeza mara baada ya matokeo hayo kutangazwa?!
1. Watoto zaidi ya 60% kuferi haijawahi kutokea tangu zama za ukoloni, leo inatokana na nini?

2. Inakuwaje watoto ambao hawakufanya baadhi ya mitihani, na mitihani hiyohiyo ndiyo wapewe maksi za kufaulu wakati ile waliyoifanya wameshindwa??

3. Je, taarifa za watoto waliofukuzwa shule kuonekana kwenye matokeo hayo wakati wao wenyewe hawakuingia darasani tuliiteje?

4. Kumekuwa na shinikizo la kutaka Dr. Ndarichako ang'oke kwenye nafasi hiyo, Je, tuaminishwe kuwa hizo ni moja ya mbinu ambazo zimetumika kuwa kishinikizio?

5. Je tuamini kuwa huu ni moja wa mkakati wa watawala kuendelea kuwafanya wapumbavu waendelee kuwa wapumbavu, wajinga waendelee kuwa wajinga, na wale wachache wenye mamlaka waendelee kututawala hadi miaka ya dahali?!!

Maswali yapo mengi ya kujiuliza juu ya sakata hili, naomba wenzangu muendelee kujazilizia ikiwezekana hata Ndarichako mwenyewe.

Tusikurupuke kulaumu: Tutafakari kwanza.
 
Fani ya elimu ni muhimu sana kwa maendeleo ya kila mmoja wetu. Ili tupate matinda mazuri hatuna budi kuzingatia na kuwekeza katika mambo makuu Matatu
1.Mfundishaji
2.Mfundihwaji na
3.Zana za kufundishia
Mfundishaji lazima ajengwe katika hali inayofaa kufundisha kwa kuzingatia mfumo bora utakao mfanya aipende kazi. Apewe stahiki zake kwawakati, athaminiwe na kushilikishwa kwa kila namna katika mipango kazi ya kuboresha kazi yake. Chukulia mfano mfundishaji anaelekezwa kufundisha jambo ambalo nigeni kwake tena bila hata semina. Mambo yanaongezwa na kupunguzwa pasi ushilikishwaji wake. Hapa lazima mtu asifaulu. Kama tutaamua kumjali mfundishaji kwa kumpa mazingira ya kuwa na furaha kazini basi naye atafanya makubwa.
Nikigeukia mfundishwaji, nae lazima apewe mazingira mazuri yatakayochochea utayari wake wa kusoma. Kwa mfano pana baadhi ya wafundiswaji wanatoka umbali wa zaidi ya km 10 hadi huduma inapopatikana. Anafika shule tena kwa farasi wa chuma ama magurudumu ya kuzaliwa nayo. Anafika hana hamu hata ya kusoma. Mfundishaji hasa wa saa za karibu na kuondoka hataeleweka maana huyu anaanza kuwaza safari ya kurudi huku akiwa hana talajio la kupata lunch!
Kwa upande wa zana za kufundishia mama weeeee! Huku kila mtu na "uniform" yake. Hakuna muelekeo. Shule hazina vitabu wala chaki. Nani ataelewa kwa hali hii? Je matokeo ya aina hii tutayakwepa?
Kama wenye mamlaka wasipobadili fikra katika duals hili hakika hatuenei. Maana matokeo hayo yamepikwa na Fikira zao. Mwisho, Hatafundi cherrhani asipopewa kiwango cha kuridhisha ataongea na asiposikilizwa atakaa kimya na kimya chake kitaonekana katika nguo atayo shona,.
 
Habari za usiku huu wamajamvi!

Pamoja na sababu kadha wa kadha juu ya kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha Nne,mimi leo nakuja na sababu kuu inayochangia kushuka kwa ufaulu huo.Mpango wa kushusha madaraka ya kuendesha elimu ya sekondari hadi halmashauri za wilaya umechangia kwa kiasi kikubwa mno kuharibu mfumo wa usimamizi wa utoaji elimu bora katika shule za sekondari[The instructional supervision of secondary education in schools].Moja ya matatizo ni pale wanasiasa hususani wabunge na madiwani wanapowachanganya vichwa wakuu wa shule,walimu na Board za shule katika usimamizi wa shule hizi.

Imefikia waheshimiwa hawa kushinikiza uhamisho kwa wakuu wa shule na walimu kwa hisia za misimamo tofauti ya kisiasa,hali hupelekea kuyumba kwa strategies za kiutawala na hivyo wanafunzi kujikuta wakiyumba pia.Kadhalika mfumo huu umeleta mkanganyiko katika utekelezaji wa sera ya Elimu ya taifa[NATIONAL EDUCATION POLICY] kwa maana kwamba msimamizi wa elimu na washika dau wanauelewa tofauti juu ya sera yenyewe hivyo kupelekea double standards katika kufikia malengo ya sera ya Elimu.

Pamoja na decentralisation kuna sababu sambamba na hilo nayo ni rushwa,mathalani maafisa Elimu wa sekondari[huenda baadhi]wametumia mwanya huo kuendekeza Rushwa kutoka kwa wakuu wa shule na walimu hivyo kupelekea poor instructional supervision in secondary schools.Nimeweka sababu hii japo kwa uchache ili pamoja na sababu nyingine tupendekeze suluhu kabla ya zahama ama ghalika haijazoa umma wa watoto ambao hawajachakachuliwa.Kwangu mimi suluhu ni Iundwe kamisheni ya elimu ya taifa[The National Education Commission-NECo]ambayo kazi yake ni pamoja na kudeal na kero zinazoikabili sector ya elimu na kupendekeza needs za ku-transform mtaala wa elimu ya taifa. ALAMSIKI.
 
Wanacheza na moto maofisi haikaliki sas hivi chezea mwalimu wewe? na bado kama 5% ni div1,2 na 3 alafu 95% div 4 and 0. Nchi imeanguka kwa hakika.
 
Commission hii unayotaka iundwe ni ya muda au ya kudumu na je inayatoa wapi madaraka yake na inawajibika kwa nani? Pamoja na janga hili hatuhitaji maamuzi ya kukurupuka.
 
Tatiza linaanzia kwenye mtaala na vipaumbele vya Taifa letu. Mara kilimo kwanza, mkukuta nk ukweli ni kwamba ili tusonge mbelelazima tuamue kuwa sasa ni ''elimu kwanza na siyo kilimo kwanza. Elimu kwanza ni walimu kwanza, vitabu kwanza, maabara kwanza na siyo majengo kwanza. Ukishampata mwl aliyehamasika na competent we mpe ubao na chaki chini ya mwembe tu uone kazi yake. Kwani ilikuwaje enzi za elimu ya Ndumbaro miaka ile ya 1970s'? Ujinga unatumaliza. Na ujinga ni kipaji kwa wengine.
 
Jamani kweli matokeo yalikuwa siyo mazuri Hatimaye shule inayoongozaga kila mwaka haina Div one ya single Digit? Aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…