Bila shaka ni binadamu wachache sana katika ulimwengu wa leo ambao hawakupitia mikononi mwa mwalimu. Mwalimu ni mlezi, tabibu, afisa wa afya, hakimu, mnasihi, kasisi, askari polisi, mtetezi wa haki za wanafunzi na mambo mengine yote mazuri ambayo kimsingi hutakiwa kuyarithisha kwa kizazi kilichopo na kijacho.
Fikiria mtoto wa chekechea na (nursery and Kindergatten) akiwa na miaka mitatu anakabidhiwa kwa mwalimu: mwalimu ndiye anayetakiwa kumhudumia anapojisaidia, akiugua, au apatwapo na madhila yoyote wakati mzazi akiwa anaendelea na shughuli zake. Fikiria kwa mwalimu anayemlea mtoto hadi anafikia shule ya msingi, sekondari mpaka vyuo endapo atakengeuka kimaadili akaamua kutema sumu kwa watoto hawa tangu wakiwa wadogo matokeo yake nini.
Namshukuru Mungu kuwa mimi mwenyewe ni mwalimu na ninaipenda kazi hii kwa dhati. Hata hivyo, kutokana na utafiti wangu (action research) kazini nimegundua kwamba moyo wa walimu waliowengi kujituma kwa ajili ya kazi hii umepotea. Waulize walimu wanaoajiliwa leo mtazamo wao kuhusu kazi hii! Ukiwasikia hutatamani kuwauliza tena na utagundua kuwa inahitajika hatua zichukuliwe ili kunusuru hali hii. Wengi hujilinganisha na wenzao waliosoma fani nyingine na kujikuta wako nyuma kimaendeleo na jamii inawabagua. Kwa walio wengi ukijilinganisha fani kama benki, tra, ardhi, kilimo, afya, bandari n.k. Hadhi ya mwalimu ni duni mno katika jamii ya kitanzania na wengine hawapendi kujitambulisha kama walimu. Ukiangalia vigezo vinavyoleta tofauti havieleweki. Kwa mfano: mtu anafaulu darasa la saba vizuri, kidato cha 4 anatoka na division anazoziheshimu kawambwa (i, ii au iii) sawa na fani nyingine. kidato cha vi hivyohivyo isipokuwa kosa ni kuchagua kusomea ualimu iwe ni masomo ya sayansi ama sanaa maana yake atakuwa amepoteza mwelekeo. Yule atayepata four akaenda Nursing, chuo cha sheria Lushoto ameula au kujiunga na jeshi la mganbo kisha akaajiriwa tanesco, bandari, benki, tanapa, huyo kaula. Ila mwalimu na digrii yake ya mathematics na phisics ni cha mtoto mbele ya mwenye credit moja iliyompeleka unesi au ukarani wa mahakama! Hata atm card alishakabidhi kwa mkopeshaji mwenye riba kubwa ambalo ni dili la wakubwa.
Ole wa nchi hii ambayo inakausha maeneo oevu kwa mazoea ya umangimeza maana itavuna sawasawa na matendo yake. Unawezaje kuwadharau watu wanaoshikilia amali za nchi ili kuzirithisha kwa watanzania wa sasa na kizazi kijacho? Nenda Cuba, China, Japan na nchi nyingine zisizoruhusu usanii! Ualimu ni title! Mwalimu akikuta mahali huduma fulani ya kungojea kwa kujipanga utasikia anahimizwa apate kwanza ili awahi kwenye kazi yake. Kama hatutajifunza kwa hili, tukafikiri mahakama, ukatili wa mwajiri, mifumo ya kiutawala kama OPRAS ndilo jawabu basi tutarajie maajabu mengine KWA MAANA KUDHULUMU WALIMU NI SAWA NA KUKAUSHA VYANZO VYA MAJI KWANI CHEMICHEMI ZIKIKOMA NDIO MWISHO WA MAVUNO BORA.