Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Lazima tuwalaumu kwani wao hawakosi taarifa kuwa Selemani na Paulo wamejenga kwenye fukwe za mto msimbazi.Je, haina power ya kusema "Sele usijenge au bomoa kibanda chako hapo mtoni"

Na hiyo rushwa; TAKUKURU si ni ya serikali pia au haina meno mpaka watu wanatoa rushwa?
Ikumbukwe hujengi bila kuwa na kibali cha ujenzi ambacho kinatolewa serikalini.😕😕😕😕😕
 
Jiwe alibomoa nyumba, nyuzi zilijaa ndani humu za kulaumu, watu walipewa maeneo lakini wakauza wamerudi palepale.

Unataka wafanyeje sasa
 
Jiwe alibomoa nyumba, nyuzi zilijaa ndani humu za kulaumu, watu walipewa maeneo lakini wakauza wamerudi palepale.

Unataka wafanyeje sasa
Baada ya Nzilankende kulaumiwa alilegeza kamba?
Hebu angalia hii mkuu;
Baba: Hiki chakula kina sumu wanangu musile naomba mukakitupe
Watoto: Baba njaa kali tunaomba tule hivyo hivyo tu.
Baba: Musile wanangu mutadhurika nawaomba mule chakula hiki badala yake.
Jirani: Huyu baba ana roho mbaya mno anawanyima watoto chakula ili wafe njaa.

Watoto wanalazimisha kula kwa kuvizia na wakati mwingine baba anawapa maji ya kunawa ili wale chakula
Halafu watoto wanakula kisha wanakufa.
Hapo baba hana kosa mkuu?
 
Chakula chenye sumu unawaachia watoto wenye njaa waamue wale au wasile? Hapo baba atakuwa amepima DNA na kugundua sio watoto wake, maana wakiwa watoto wake atakitupa yeye na kuhakikisha anawaletea chakula kingine salama!
 
Majibu yako yanaendana na wazo langu kwamba huwezi kuacha watoto wako wadhurike eti kwa kuhofia watu au wanao watalalamika.Hili ni sawa na wananchi wako ukiwa kama Rais
 
Jiwe alibomoa nyumba, nyuzi zilijaa ndani humu za kulaumu, watu walipewa maeneo lakini wakauza wamerudi palepale.

Unataka wafanyeje sasa
Unajua sisi watu wa zamani enzi tukiangalia mpira, kina Jongo na Kipozi wakitangaza mpira, mchezaji akiwa offside walipenda kusema ni offside, Omari Hussein anaambiwa umejenga kibanda hapa bila idhini ya jiji!

Unafikiri alimaanisha nini? Serikali za enzi hizo hazikuruhusu huu ujinga wa kujenga bila vibali, ungebomolewa mara moja. Serikali zilizofuata zilikuwa na tatizo gani? Kwa nini zikaruhusu hili kushamiri?
 
Ukanda wote wa Pwani ya Bahari 50Km kutoka ufukweni itengenezwe Master plan yenye kufuata Topographic Survey ikijumuisha majengo gani yakae wapi lakini pia miundombinu gani inahitaji katika utunzaji mazingira.
Tatizo nilionalo kwa sasa ni uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa unaosababisha miundombinu ya kupitisha maji kuziba hivyo maji kuchukua mikondo mingine kupita.
Hata hivyo Ujenzi holela bila kufuata ushauri wa wataalamu ni tatizo lingine la kuifanyia kazi kwa haraka.
Ni vizuri bajeti za kujenga kingo za vijito na mito mikubwa inayopita katikati ya miji mikubwa ikatengwa kama ilivyo miundombinu mingine ili kutunza mazingira lakini pia kuzuia mafuriko ya mara kwa mara.
Ni vyema kwa Secretariate za Mikoa zikaunda timu za wataalamu ngazi ya Mkoa kwa kushirikisha wataalamu wa sekta binafsi walau kupata sanifu yakinifu ili Serikali kuu/Wizara husika zikatenga bajeti.
Mkuu tatizo jingine ni kwamba miundombinu iliyokuwapo haikukidhi mahitaji na pia mingi iliondolewa kupisha ujenji wa majengo mapya!
 
Stendi ya mwendokasi Zakiem imejaa maji, barabara ya mwendo kasi imejaa maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
1705934780067.png

Kuna watu wasio na uwezo wa kufikiri kwenye hii thread, labda tuwaulize kama hapa napo ni bondeni waliojenga wahame!
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Here we go again. Ndugu! Kazi ya serikali ni nini? Hivi unajua serikali ndiyo ina wajibu wa kusema hapa ni ruksa kujenga, na hapa siyo ruksa? Sheria zipo ili ziwe mapambo? Au hujui ni kwanini ulimwenguni wote watu alianzisha serikali au utawala wa aina fulani?
 
Magreda yakija kubomoa hawajahamisha vitu mseme Tena serikali Ina MAAMUZI ya kikatili?
Hiyo serikali inakuwa wapi mpaka watu wajenge nayo isubiri kuja na magreda kubomoa? Ndugu, nyumba inajengwa siku moja, au mbili? Sehemu zote atarishi zenye nyumba, zilijengwa kwa muda mrefu, huku serikali ikiwa inaangalia. Kazi ya serikali ni kuongoza na siyo kubomoa! Ilitakiwa iongoze watu pale ilipoona wanajenga!
 
Usimamizi mbovu wa serikali ndio umeafanya Dar ikafikia hapa. Kwa hili Samia sio wa kupewa lawama, maraisi karibu wote walilifumbia macho na leo tupo na kero hii kubwa sana.
Hili lawama iko kwa CCM.
 
Ni kweli maafa ya mafuriko yanaitwa natural disasters, lakini sio lazima natural disasters zilete maafa kwa raia na mali zao.

Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe, ubinafsi, kutojali, na uongozi mbovu kwa ujumla wa viongozi wa serikali. Si mara ya kwanza Dar es Salaam inapata mafuriko. Ni zaidi ya miaka 20 tunaishi kwa kudhani kwamba tatizo la mafuriko Dar dawa yake ni kumwomba Mungu atuepushe na vifo na upotevu wa mali, kutia ndani uharibifu wa miundombinu.

Mji wowote ulio pembezoni mwa bahari kuwa na tatizo la mafuriko yanayotokana na mvua kwa zaidi ya miaka 20 hakuna kingine zaidi ya uzembe. Serikali yetu imejisahau mno, hasa wakijua Watanzania sio rahisi kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kuwa tu inafanya uzembe, ufisadi, ubinafsi nk. Kwa hiyo wanajisahau sana.

Tatizo la mafuriko linahitaji suluhisho ambalo gharama yake huenda hata isifikie gharama ya kununua ndege mbili za dreamliner, au pesa tunayolipa makampuni yanayotushitaki kukiuka mikataba.
  1. Wakusanye wataalamu wa physical geography watengeneze topographical na contour maps za Dar es Salaam na ukanda wa pwani, wakionyesha ilikupata elevation na terrain ya ukanda wote wa Dar na contour lines zinavyokwenda
  2. Kwa kutumia topographical map na contour lines, wakusanye civil engineers wachore line kupitisha maji kwa kutumia channel za ukubwa wa kiasi na kupeleka kwenye channel kubwa ambazo zitaelekeza maji baharini
Sasa, katika kufanya design ya channel za maji, factor of safety isiwe tena historical data, bali iwe projection iliyo informed na modeling za climate change impact scenarios katika masuala ya mvua, na ipigwe factor kubwa zaidi ya standard factors (najua mainjinia tu ndio wataelewa hii paragraph)

Ikibidi, baadhi ya majengo itabidi yaondoke, yabomolewe, hata kama ni mazuri kiasi gani.
View attachment 2878486
Ninatamani sana nimpigie Samia simu nimwambia nipe hii kazi nisimamie huu mkakati. Raisi Samia nakuhakikishia kwamba mji wowote uliopo kando ya bahari haupaswi kuwa na mafuriko kama tunayoona Dar. Au mwambie Prof. Tibaijuka asimamie hili.

Tatizo lililop kwako Samia ni kuteua watu ambao wanaona kipao mbele cha Dar ni kushughulika na changudoa na maandamano ya Chadema badala ya matatizo yanayoathiri wananchi na taifa kwa ujumla kwa kiwango cha juu sana. Unapewa sifa kila siku katika mambo ambayo ni routine sana, usiridhike au kudanganywa na hizo sifa. Kutoa hela za kujenga Zahanati na nini sijui sio sifa za kuwa raisi mzuri. Kwanza wengine tunaona hilo ni uongozi mbovu tu, kwa sababau pesa hizo zinapaswa kutolewa kupitia mipango ya maendeleo na bajeti za maeneo hayo. Kwa nini unakubali kuleweshwa na sifa za mambo yanayotakiwa kufanywa na wakuu wa mikoa na wakurgenzi wa miji na majiji? Fanya kazi za kitaifa tukusifie, sio mambo ya vijijini, wilayani na mikoani. Hiyo sio ligi yako.

Bado hatuoni unayofanya katika mambo makubwa ambayo yataacha legacy yako, pamoja na hili la mafuriko Dar. Japo tunaelewa ni suala la majiji haya matatu, Ilala, Kindondoni na Temeke, lakini lichukue sura ya kitaifa ili kuwe na coordination rahisi.
Usidhani huko kusifiwa kwa mambo madogodogo ni bahati mbaya, huko ndiko anakostahili kuwepo, na ndio kunaendana na kiwango chake!
Kama mna kampuni ya ushauri wa haya masuala, mjaribu kuiingia serikali na mchanganuo wenu, kama watakuwa tayari kuwasikiliza na kufanyia kazi hizi kadhia.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Watu wameshatahadharishwa na mamlaka ya hali ya hewa wahame hawataki, kuna nabii akawaambia wahame wakasusa, sasa tuwasaidieje?.

Mtu unaona kabisa huu ni mkondo wa maji, unalazimisha kujenga, unataka nani apate uchungu wa uhai wako zaidi yako mwenyewe?.

Siipendi sisiemu na watu wake, lakini ktk hili la mafuriko niko na Samia.

Nyie kila mwaka maafa yanawakumba lakini hamkomi, hivi aliyewaambia maisha yanapatikana huko mitaroni ni nani?.

Huku bara ardhi imejaa tele, njooni huku.

Mvua ni baraka, acha iendelee kunyesha maana ni msimu wake.
Wahame waende wapi mkuu!! Viela vyenyewe vya kudunduliza, huwezi kuhama wakati huna pa kwenda, wakati mwingine hela ya msosi tu shida! Tuombe sana Mungu atuepushe na haya majanga kusema kweli [emoji1431][emoji1431]
 
Kwa hiyo waendelee kubaki !?
 
Back
Top Bottom