Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Ni kweli maafa ya mafuriko yanaitwa natural disasters, lakini sio lazima natural disasters zilete maafa kwa raia na mali zao.

Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe, ubinafsi, kutojali, na uongozi mbovu kwa ujumla wa viongozi wa serikali. Si mara ya kwanza Dar es Salaam inapata mafuriko. Ni zaidi ya miaka 20 tunaishi kwa kudhani kwamba tatizo la mafuriko Dar dawa yake ni kumwomba Mungu atuepushe na vifo na upotevu wa mali, kutia ndani uharibifu wa miundombinu.

Mji wowote ulio pembezoni mwa bahari kuwa na tatizo la mafuriko yanayotokana na mvua kwa zaidi ya miaka 20 hakuna kingine zaidi ya uzembe. Serikali yetu imejisahau mno, hasa wakijua Watanzania sio rahisi kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kuwa tu inafanya uzembe, ufisadi, ubinafsi nk. Kwa hiyo wanajisahau sana.

Tatizo la mafuriko linahitaji suluhisho ambalo gharama yake huenda hata isifikie gharama ya kununua ndege mbili za dreamliner, au pesa tunayolipa makampuni yanayotushitaki kukiuka mikataba.
  1. Wakusanye wataalamu wa physical geography watengeneze topographical na contour maps za Dar es Salaam na ukanda wa pwani, wakionyesha ilikupata elevation na terrain ya ukanda wote wa Dar na contour lines zinavyokwenda
  2. Kwa kutumia topographical map na contour lines, wakusanye civil engineers wachore line kupitisha maji kwa kutumia channel za ukubwa wa kiasi na kupeleka kwenye channel kubwa ambazo zitaelekeza maji baharini
Sasa, katika kufanya design ya channel za maji, factor of safety isiwe tena historical data, bali iwe projection iliyo informed na modeling za climate change impact scenarios katika masuala ya mvua, na ipigwe factor kubwa zaidi ya standard factors (najua mainjinia tu ndio wataelewa hii paragraph)

Ikibidi, baadhi ya majengo itabidi yaondoke, yabomolewe, hata kama ni mazuri kiasi gani.
View attachment 2878486
Ninatamani sana nimpigie Samia simu nimwambia nipe hii kazi nisimamie huu mkakati. Raisi Samia nakuhakikishia kwamba mji wowote uliopo kando ya bahari haupaswi kuwa na mafuriko kama tunayoona Dar. Au mwambie Prof. Tibaijuka asimamie hili.

Tatizo lililop kwako Samia ni kuteua watu ambao wanaona kipao mbele cha Dar ni kushughulika na changudoa na maandamano ya Chadema badala ya matatizo yanayoathiri wananchi na taifa kwa ujumla kwa kiwango cha juu sana. Unapewa sifa kila siku katika mambo ambayo ni routine sana, usiridhike au kudanganywa na hizo sifa. Kutoa hela za kujenga Zahanati na nini sijui sio sifa za kuwa raisi mzuri. Kwanza wengine tunaona hilo ni uongozi mbovu tu, kwa sababau pesa hizo zinapaswa kutolewa kupitia mipango ya maendeleo na bajeti za maeneo hayo. Kwa nini unakubali kuleweshwa na sifa za mambo yanayotakiwa kufanywa na wakuu wa mikoa na wakurgenzi wa miji na majiji? Fanya kazi za kitaifa tukusifie, sio mambo ya vijijini, wilayani na mikoani. Hiyo sio ligi yako.

Bado hatuoni unayofanya katika mambo makubwa ambayo yataacha legacy yako, pamoja na hili la mafuriko Dar. Japo tunaelewa ni suala la majiji haya matatu, Ilala, Kindondoni na Temeke, lakini lichukue sura ya kitaifa ili kuwe na coordination rahisi.
Ukanda wote wa Pwani ya Bahari 50Km kutoka ufukweni itengenezwe Master plan yenye kufuata Topographic Survey ikijumuisha majengo gani yakae wapi lakini pia miundombinu gani inahitaji katika utunzaji mazingira.
Tatizo nilionalo kwa sasa ni uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa unaosababisha miundombinu ya kupitisha maji kuziba hivyo maji kuchukua mikondo mingine kupita.
Hata hivyo Ujenzi holela bila kufuata ushauri wa wataalamu ni tatizo lingine la kuifanyia kazi kwa haraka.
Ni vizuri bajeti za kujenga kingo za vijito na mito mikubwa inayopita katikati ya miji mikubwa ikatengwa kama ilivyo miundombinu mingine ili kutunza mazingira lakini pia kuzuia mafuriko ya mara kwa mara.
Ni vyema kwa Secretariate za Mikoa zikaunda timu za wataalamu ngazi ya Mkoa kwa kushirikisha wataalamu wa sekta binafsi walau kupata sanifu yakinifu ili Serikali kuu/Wizara husika zikatenga bajeti.
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Ni nani wa kusimamia sheria za mazingira?
 
Pale jangwani mvua kidogo unakuta magred yanatoa tope kila mwaka wameridhika ...Ile barabara kutokea magomeni hata uendeshe gari unaona kabisa unashuka kama kweny shimo.


Wanashindwa vip pale kujaza enzi za kutengeneza kituo cha mwendo kasi pale level mpaka mapipa hapa
hayo madude mradi wa mtu, hayatoi pale. anaombea mvua tu
 
Serikali yake au ya watangulizi wake ndio waliacha watu wajenge, au hata walitoa hivyo vibali vya kujenga. Kwa hiyo tumlaumu nani sasa?

Au kwa lojiki zako za chekechea, watu wanapomlilia Samia atoe msaada wa fedha za wodi ya wazazi, yeye ndio anakuwa kawapa mimba na kawazalisha?
Huyo popoma kichwani uji hawezi elewa ulicho shauri
 
Machapisho kama adhimu hupata wachangiaji wachache kuliko ya Uchumba wa Manara.
Kiukweli hatutaki tuu kushughulikia changamoto zetu kikamilifu... Data base tokea Enzi za ukoloni 1957 ambazo tayari zilikuwa zinaonyesha maeneo ya maji, mikondo mpaka mapito ya maji... Swali sasa kwa nini havifuatiliwi? Je hii nchi haina planners?? Mwisho niseme pia mfumo wa uongozi, hasa huko mikoani na mawilayani, ambako kila kitu kidogo unamuona DC, mara RC badala ya kuona wataalam husika wakiwajibika ndiyo kabisa limeuwa ubunifu na utaalamu... Sasa hivi huko mawilayani eti unakuta afisa mifugo au kilimo anasimamia ujenzi wa madarasa au nyumba za walimu???
Screenshot_20240121-225649.jpg
 
Sio kila kitu unalaumu serikali kijana maeneo yote yenye changamoto ya mafuriko wananchi waliambiwa wahame kwa hiari ila hawakufanya hvyo na wengine walipewa maeneo wameuza wamerudi tena mabondeni serikali inahusikaje na wananchi sikio la kufa kiufupi watanzania hatuamini kitu mpaka kitokee hata kule hanang eneo liliathiriwa walishapewa maeneo mengine wakauza wakarudi tena karibu na milima sasa unataka serikali iwachape viboko mkibolewa mnataka fidia nani atabeba huo mzigo ni kweli serikali ina changamoto zake lakini kuna vitu vingine wananchi wanajitakia.
Hivi umemuelewa mtoa mada? Hajazungumzia mtu mmoja mmoja, anazungumzia jiji lililopakana na bahari kuwa na mafuriko wapi na wapi?

Okay, watu watahama, je madaraja yanayokatika nayo yatahama?
Je barabara ya jangwani nayo itahama?
 
Sio kila kitu unalaumu serikali kijana maeneo yote yenye changamoto ya mafuriko wananchi waliambiwa wahame kwa hiari ila hawakufanya hvyo na wengine walipewa maeneo wameuza wamerudi tena mabondeni serikali inahusikaje na wananchi sikio la kufa kiufupi watanzania hatuamini kitu mpaka kitokee hata kule hanang eneo liliathiriwa walishapewa maeneo mengine wakauza wakarudi tena karibu na milima sasa unataka serikali iwachape viboko mkibolewa mnataka fidia nani atabeba huo mzigo ni kweli serikali ina changamoto zake lakini kuna vitu vingine wananchi wanajitakia.
Hivi umemuelewa mtoa mada? Hajazungumzia mtu mmoja mmoja, anazungumzia jiji lililopakana na bahari kuwa na mafuriko wapi na wapi?

Okay, watu watahama, je madaraja yanayokatika nayo yatahama?
Je barabara ya jangwani nayo itahama?
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Hivi unaelewa ulichoandika!?
 
Wanapojenga serikali inakuwa wapi, imelala? Na utakuta wengi wana vibali vya serikali. Ndio maana tunasema bottom-line yote haya ni uzembe wa serikali, japo kuna 20% ya lawama kwa hao watu, na 20% kwa natural disasters
Yani Kuna watu sio Huwa vichwa vinawaza nn !!!Yani anaiondoa serikali eti
 
Iyo yote inatokana na poor infrastructure inayochangiwa na poor sewage system ambayo inachangia maji kutuama kwenye eneo moja
 
Ni serikali ya kijinga sana na kipumbavu itakayotoa tamko kama hilo na itarajie wananchi watekeleze kwa hiari. Serikali inawajibika kuhamisha na kufidia watu kwa kuwa walipojenga hawakujenga ndani ya siku moja, na serikali ilikuwapo ikiona wakifanya hivyo.

Wewe nenda leo kajenge kibanda nyuma ya ikulu uone kama utaanza hata kuchimba huo msingi.

Katika hali hi serikali lazima ikubali kulipia gharama za kuhamisha watu, kwa sababu ni kwa uzembe wa serikali watu wapo sehemu wazizotakiwa kujenga. Na zaidi, cummukatively, serikali inaingia gharama kubwa zaidi kusaidia watu maafa yanapotokea kuliko gharama ambayo ingetumika ikiwa wangekubali kuingia gharama ya kuwahamisha.

Mbona kama serikali tunakubali kulipia ujinga wa kuwalipa watu tuliowakatia mikataba yao? Lazima katika mausha uelewe kuna gharama za upumbavu na uzembe. Serikali ikubali kwamba watu kujenga maeneo hayo ni kwa sababu ya upumbavu na uzembe wake, na hivyi ina wajibu wa kuingia gharama kurekebisha hilo
Serikali inaongoza vilaza wa namna gani wasiojua wajibu wao wala kujali usalama wao hata kidogo??

Kuna vitu sio vya kuilaumu serikali mkuu, japo ni kweli ina makosa lakini uhai wako wa kuulinda ni wewe kwanza kabla ya hiyo serikali.

Wakati huu unasema ina kosa hili na hile tayari vyombo vimesombwa na maji, nyumba nzima ina maji na sio kua hukua unajua. Unajua kabisa na sio mara ya kwanza .

Ni december tu hapo, mvua imepiga nyumba zimejaa maji lakini watu hawachukui tahadhari hata kidogo.

Mzee kabla ya serikali ni wewe kwanza, Dar hamna ushirikiano kabisa, barabara za mtaani au hata nje ya nyumba nyingi za watu ni chafu, barabara za mitaa hazipitiki, uchafu unarundwa sehemu yoyote, madimbwi yanayoweza kufukiwa hata na watu wachache hayafukiwi, wapuuzi wanaongeza tu ukubwa wa dimbwo kwa kupita na magri yao vioo juu, wanasubiri serikali.
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Mpaka wajenge na serikali inaona mpaka wanahamia maana yake nn
 
Na sahv serikali wala hawahangaiki
Na watu wa mabondeni huko

Ova
 
Unapotaka haki wajibika kwanza beba jukumu la usalama wako wewe mwenyewe kama kichaa anaona moto na anakwepa sisi tulio timamu tunakwama wapi kuyatambua maeneo hatarishi kuishi kuna watu walihamishwa wakapewa na maeneo ya kujenga wakazunguka wakarudi palepale walipoambiwa si salama now mnataka serikali yaleyale ya mwanzo?Tusiwe wasahaulifu kiasi hicho
NB:KUSIKIA KWA KENGE NI MPAKA ATOKE DAMU
 
Wengine hujibu kwa fahari kuwa wameshazowea mafuriko na hawahami. Wanasema ni tatizo la siku moja baadaye wanasafisha nyumba zao na maisha yanaendelea.
 
Wanapojenga serikali inakuwa wapi, imelala? Na utakuta wengi wana vibali vya serikali. Ndio maana tunasema bottom-line yote haya ni uzembe wa serikali, japo kuna 20% ya lawama kwa hao watu, na 20% kwa natural disasters
Shida akili zetu pia haziko sawa. Wakisema tusijenge tunalaumu, wakisema tuhame tunalalama kila kitu sisi tunaonewa
Tunataka kuishi kwa kuonewa huruma
 
Back
Top Bottom