Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Lazima tuwalaumu kwani wao hawakosi taarifa kuwa Selemani na Paulo wamejenga kwenye fukwe za mto msimbazi.Je, haina power ya kusema "Sele usijenge au bomoa kibanda chako hapo mtoni"

Na hiyo rushwa; TAKUKURU si ni ya serikali pia au haina meno mpaka watu wanatoa rushwa?
Ikumbukwe hujengi bila kuwa na kibali cha ujenzi ambacho kinatolewa serikalini.😕😕😕😕😕
 
Jiwe alibomoa nyumba, nyuzi zilijaa ndani humu za kulaumu, watu walipewa maeneo lakini wakauza wamerudi palepale.

Unataka wafanyeje sasa
 
Jiwe alibomoa nyumba, nyuzi zilijaa ndani humu za kulaumu, watu walipewa maeneo lakini wakauza wamerudi palepale.

Unataka wafanyeje sasa
Baada ya Nzilankende kulaumiwa alilegeza kamba?
Hebu angalia hii mkuu;
Baba: Hiki chakula kina sumu wanangu musile naomba mukakitupe
Watoto: Baba njaa kali tunaomba tule hivyo hivyo tu.
Baba: Musile wanangu mutadhurika nawaomba mule chakula hiki badala yake.
Jirani: Huyu baba ana roho mbaya mno anawanyima watoto chakula ili wafe njaa.

Watoto wanalazimisha kula kwa kuvizia na wakati mwingine baba anawapa maji ya kunawa ili wale chakula
Halafu watoto wanakula kisha wanakufa.
Hapo baba hana kosa mkuu?
 
utamu na uzuri wa dar ni kwamba mvua ikikatika na maji ata yawe mengi kiasi gani after 30 yanaisha shughuli zinaendelea kama kawaida mathalani apo zhakiem....
Halafu serikali inasahau hadi mvua za mwakani tena!
 
Chakula chenye sumu unawaachia watoto wenye njaa waamue wale au wasile? Hapo baba atakuwa amepima DNA na kugundua sio watoto wake, maana wakiwa watoto wake atakitupa yeye na kuhakikisha anawaletea chakula kingine salama!
 
Majibu yako yanaendana na wazo langu kwamba huwezi kuacha watoto wako wadhurike eti kwa kuhofia watu au wanao watalalamika.Hili ni sawa na wananchi wako ukiwa kama Rais
 
Jiwe alibomoa nyumba, nyuzi zilijaa ndani humu za kulaumu, watu walipewa maeneo lakini wakauza wamerudi palepale.

Unataka wafanyeje sasa
Unajua sisi watu wa zamani enzi tukiangalia mpira, kina Jongo na Kipozi wakitangaza mpira, mchezaji akiwa offside walipenda kusema ni offside, Omari Hussein anaambiwa umejenga kibanda hapa bila idhini ya jiji!

Unafikiri alimaanisha nini? Serikali za enzi hizo hazikuruhusu huu ujinga wa kujenga bila vibali, ungebomolewa mara moja. Serikali zilizofuata zilikuwa na tatizo gani? Kwa nini zikaruhusu hili kushamiri?
 
Mkuu tatizo jingine ni kwamba miundombinu iliyokuwapo haikukidhi mahitaji na pia mingi iliondolewa kupisha ujenji wa majengo mapya!
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Here we go again. Ndugu! Kazi ya serikali ni nini? Hivi unajua serikali ndiyo ina wajibu wa kusema hapa ni ruksa kujenga, na hapa siyo ruksa? Sheria zipo ili ziwe mapambo? Au hujui ni kwanini ulimwenguni wote watu alianzisha serikali au utawala wa aina fulani?
 
Magreda yakija kubomoa hawajahamisha vitu mseme Tena serikali Ina MAAMUZI ya kikatili?
Hiyo serikali inakuwa wapi mpaka watu wajenge nayo isubiri kuja na magreda kubomoa? Ndugu, nyumba inajengwa siku moja, au mbili? Sehemu zote atarishi zenye nyumba, zilijengwa kwa muda mrefu, huku serikali ikiwa inaangalia. Kazi ya serikali ni kuongoza na siyo kubomoa! Ilitakiwa iongoze watu pale ilipoona wanajenga!
 
Usimamizi mbovu wa serikali ndio umeafanya Dar ikafikia hapa. Kwa hili Samia sio wa kupewa lawama, maraisi karibu wote walilifumbia macho na leo tupo na kero hii kubwa sana.
Hili lawama iko kwa CCM.
 
Usidhani huko kusifiwa kwa mambo madogodogo ni bahati mbaya, huko ndiko anakostahili kuwepo, na ndio kunaendana na kiwango chake!
Kama mna kampuni ya ushauri wa haya masuala, mjaribu kuiingia serikali na mchanganuo wenu, kama watakuwa tayari kuwasikiliza na kufanyia kazi hizi kadhia.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Wahame waende wapi mkuu!! Viela vyenyewe vya kudunduliza, huwezi kuhama wakati huna pa kwenda, wakati mwingine hela ya msosi tu shida! Tuombe sana Mungu atuepushe na haya majanga kusema kweli [emoji1431][emoji1431]
 
Kwa hiyo waendelee kubaki !?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…