Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe wa serikali, Raisi Samia akubali ukweli huu

Usimamizi mbovu wa serikali ndio umeafanya Dar ikafikia hapa. Kwa hili Samia sio wa kupewa lawama, maraisi karibu wote walilifumbia macho na leo tupo na kero hii kubwa sana.
Kwa hiyo huo usimamizi mbovu umeanzia Kwa Samia au ndio kasababisha mkajenga mabondeni?
 
Sometimes hii nch tunalaumu mno serikali,
Watu wanajenga kwenye mikondo ya maji, wengine hadi wanatoa rushwa ili wajenge, then yakija mafuriko wanakimbilia kusema serikali, hahah
Sidhani au sikumbuki kama dar ilishawahi pata mafuriko, watu wameenda kujenga kwenye njia za maji mnaita mafuriko, sidhani aisee
 
Watu wameshatahadharishwa na mamlaka ya hali ya hewa wahame hawataki, kuna nabii akawaambia wahame wakasusa, sasa tuwasaidieje?.
Ni serikali ya kijinga sana na kipumbavu itakayotoa tamko kama hilo na itarajie wananchi watekeleze kwa hiari. Serikali inawajibika kuhamisha na kufidia watu kwa kuwa walipojenga hawakujenga ndani ya siku moja, na serikali ilikuwapo ikiona wakifanya hivyo.

Wewe nenda leo kajenge kibanda nyuma ya ikulu uone kama utaanza hata kuchimba huo msingi.

Katika hali hi serikali lazima ikubali kulipia gharama za kuhamisha watu, kwa sababu ni kwa uzembe wa serikali watu wapo sehemu wazizotakiwa kujenga. Na zaidi, cummukatively, serikali inaingia gharama kubwa zaidi kusaidia watu maafa yanapotokea kuliko gharama ambayo ingetumika ikiwa wangekubali kuingia gharama ya kuwahamisha.

Mbona kama serikali tunakubali kulipia ujinga wa kuwalipa watu tuliowakatia mikataba yao? Lazima katika mausha uelewe kuna gharama za upumbavu na uzembe. Serikali ikubali kwamba watu kujenga maeneo hayo ni kwa sababu ya upumbavu na uzembe wake, na hivyi ina wajibu wa kuingia gharama kurekebisha hilo
 
Hizo ni semantics. Kutoa rushwa kwa daktari ili akutibu wa kulaumiwa ni wewe, sivyo? Na trafiki kuomba rushwa wa kulaumiwa ni wewe? Na tuoa rushwa polisi wamfutie mashataka mtuhumiwa wa kulaumiwa ni mtoa rushwa? Hebu jaribu kujifanya una uwezo wa kuchambua mambo angalau kidogo
Serikali ni watu kama ulivyo wewe, hivyo si kila kitu lazima usubiri mwongozo wa binadamu mwenzio ili uchukue hatua.

Janga unaliona hilo linakuja, unasubiri nini kuchukua hatua kwa ajili ya usalama wako mwenyewe?

Tusipende kulaumu kila kitu, hakuna namna nyingine zaidi ya kuhama ili kuwa salama wewe na mali zako.

Watu wamegoma kuhama pamoja na kuhamasishwa wahame, sasa unataka nani aache kuhangaika na maisha ya familia yake aje ahangaikie familia za wengine?.

Miaka nenda rudi wimbo ni uleule ikifika msimu wa mvua, kwani nyie ni kenge kuwa hamsikii hadi damu iwatoke masikioni?.

Endeleeni kupambana na hiyo hali ya kujitakia.
 
Alaumiwe aliyejipeleka machinjioni wakati sehemu salama zipo nyingi hapa Tanzania.

Hao waliotoa vibali wana makosa yao lakini mwenye kosa zaidi ni yule aliyetoa rushwa ili apate kibali cha kujenga kwenye njia za maji.
Na ukiona mwanao kachukua kamba anaenda kujiny'onga utasema mwacheni, anajua madhara ya kujinyonga, wewe sio wa kulaumiwa, sivyo?
 
Ni serikali ya kijinga sana na kipumbavu itakayotoa tamko kama hilo na itarajie wananchi watekeleze kwa hiari. Serikali inawajibika kuhamisha na kufidia watu kwa kuwa walipojenga hawakujenga ndani ya siku moja, na serikali ilikuwapo ikiona wakifanya hivyo.

Wewe nenda leo kajenge kibanda nyuma ya ikulu uone kama utaanza hata kuchimba huo msingi.

Katika hali hi serikali lazima ikubali kulipia gharama za kuhamisha watu, kwa sababu ni kwa uzembe wa serikali watu wapo sehemu wazizotakiwa kujenga. Na zaidi, cummukatively, serikali inaingia gharama kubwa zaidi kusaidia watu maafa yanapotokea kuliko gharama ambayo ingetumika ikiwa wangekubali kuingia gharama ya kuwahamisha.

Mbona kama serikali tunakubali kulipia ujinga wa kuwalipa watu tuliowakatia mikataba yao? Lazima katika mausha uelewe kuna gharama za upumbavu na uzembe. Serikali ikubali kwamba watu kujenga maeneo hayo ni kwa sababu ya upumbavu na uzembe wake, na hivyi ina wajibu wa kuingia gharama kurekebisha hilo
Hameni, acheni kuongea kwa sauti.

Suluhisho ni moja tu, KUHAMA au kubaki kusubiri maafa zaidi.
Siku zote mchuma janga hula na wakwao.
 
Sijawahi kumkubali Hangaya hata kwa jambo moja lakini hili la miundombinu ya Dar mnamsingizia tatizo liko kwa wakaazi wenyewe maana ubishi na ubabe na ujuaji ndio vimetawala , haiwezekani watu wanauza viwanja mpaka kwenye maporomoko na mabonde na mito pamoja na vijito , unadhani maji unapoambiwa hufuata mkondo wake unadhani ni maji ya bahari? kiukweli mji umepangika kiholela sana na watu wameziba vichochoro vyooote mabonde na mito unataka kusiwe na mafuriko? kama akili zenyewe hizi za kujenga mtoni kisha wananyanyua misingi iwe mikubwa wakitegemea mvua haitaharibu sahau. Hangaya asilaumiwe kwenye hili mjitafakari wenyewe , haiwezekani watu wanauziana mito na mabonde kisha lawama zielekee kizimkazi, NO.
 
Ushauri tu; Ukitoa mada usianze kulaumu watu
Uki address tatizo vizuri, anaye laumiwa ataonekana
Mfano: kwa majibu wa post yako naona makosa yapo pande mbili hapa
1. Raia kwenda kujenga maeneo ya karibu na mito na mabondeni
2. Serikali kuwaacha wajenge hadi kuhamia bila kuwachukulia hatua
3. Kama kwenye hii Nchi bado kuna Kitengo cha mipango miji, nashauri wafute kabisa hicho kitengo.....
 
Tatizo lipo pande zote wala Rais asilaumiwe kwani haya nae kayakuta.
Walishindwa waliopita yeye nani wa kuweza?
Kuna watu wabishi wanataka tu mradi waishi kwa mazoea wamefunga mikondo yote yaliyokuwa yanapitisha maji na wengine wamevunja drainage systems zote na kujenga majumba juu yake

Hao wahandisi mnaowasema ni kina nani umeona madaraja wanayojenga utafikiri sio yale malori makubwa yatapita na maji yatapita mengi
Yaani daraja utafikiri la mbele ya duka la mangi
Hao ndio civil engineer unaowasema?

Hebu angalia madaraja yetu na wenzetu tofauti yake, hili kweli ni daraja au
Screenshot_20240121_075912_Instagram~2.png
 
Wanapojenga serikali inakuwa wapi, imelala? Na utakuta wengi wana vibali vya serikali. Ndio maana tunasema bottom-line yote haya ni uzembe wa serikali, japo kuna 20% ya lawama kwa hao watu, na 20% kwa natural disasters
Nitoe mfano mdogo WA uzembe WA watendaji WA Serekali, Kuna barabara wanajipambanua wanajenga kutoka kimara mwisho kupitia kinyerezi Bonyokwa, hii barabara inafahamika siku nyingi itajengwa, Watu wanaruhusiwa waendelee kujenga, Kuna Watu wanajenga Kuta Za gharama, nyumba na vitu vingi ili wafidiwe, na ujenzi unaendelea, juzi wamekuja Watu sijajua wametumwa na Nani ila pia hawatumii utaalamu wapo kama wameokotwa njiani Kwani wanaweka tape kati kati na kupima mita kadhaa kulia na kushoto, ila hii kazi ni ya surveyor, Land surveyor Kwa nini wizara ya Ardhi, Tarura au Kama ni Tanroads Kwa nini wanaturudisha kwenye ujima!? Niwashauri waje na michoro ya usanifu WA hiyo barabara na land surveyor ambaye ataweka beacons za hiyo design na waweze kufidia kulingana na uhitaji na Sio walichokifanya!! Madness, Tunasomesha watu ili iweje!? Upigaji upigaji upigaji Kila Kona
 
Na ukiona mwanao kachukua kamba anaenda kujiny'onga utasema mwacheni, anajua madhara ya kujinyonga, wewe sio wa kulaumiwa, sivyo?
Kuna mifano haina uhalisia, anayejenga ni binadamu mtu mzima mwenye utashi wa kung'amua jema na baya sio mtoto.

Kila siku Serikali inawaambia hameni hamtaki, wewe unataka nini zaidi ya maafa?.
 
Mleta mada unaeleweka vizuri sana. nawashangaa ambao hawajakwelewa. tena umeongea kisomi hasa.
 
Ni kweli maafa ya mafuriko yanaitwa natural disasters, lakini sio lazima natural disasters zilete maafa kwa raia na mali zao.

Asilimia 60 ya maafa ya mafuriko Dar es Salaam yanatokana na uzembe, ubinafsi, kutojali, na uongozi mbovu kwa ujumla wa viongozi wa serikali. Si mara ya kwanza Dar es Salaam inapata mafuriko. Ni zaidi ya miaka 20 tunaishi kwa kudhani kwamba tatizo la mafuriko Dar dawa yake ni kumwomba Mungu atuepushe na vifo na upotevu wa mali, kutia ndani uharibifu wa miundombinu.

Mji wowote ulio pembezoni mwa bahari kuwa na tatizo la mafuriko yanayotokana na mvua kwa zaidi ya miaka 20 hakuna kingine zaidi ya uzembe. Serikali yetu imejisahau mno, hasa wakijua Watanzania sio rahisi kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kuwa tu inafanya uzembe, ufisadi, ubinafsi nk. Kwa hiyo wanajisahau sana.

Tatizo la mafuriko linahitaji suluhisho ambalo gharama yake huenda hata isifikie gharama ya kununua ndege mbili za dreamliner, au pesa tunayolipa makampuni yanayotushitaki kukiuka mikataba.
  1. Wakusanye wataalamu wa physical geography watengeneze topographical na contour maps za Dar es Salaam na ukanda wa pwani, wakionyesha ilikupata elevation na terrain ya ukanda wote wa Dar na contour lines zinavyokwenda
  2. Kwa kutumia topographical map na contuoar lines, wakusanye civil engineers wachore line kupitisha maji kwa kutumia channel za ukubwa wa kiasi na kupeleka kwenye channel kubwa ambazo zitaelekeza maji baharini
Sasa, katika kufanya design ya channel za maji, factor of safety isiwe tena historical data, bali iwe projection iliyo informed na modeling za climate change impact scenarios katika masuala ya mvua, na ipigwe factor kubwa zaidi ya standard factors (najua mainjinia tu ndio wataelewa hii paragraph)

Ikibidi, baadhi ya majengo itabidi yaondoke, yabomolewe, hata kama ni mazuri kiasi gani.
View attachment 2878486
Ninatamani sana nimpigie Samia simu nimwambia nipe hii kazi nisimamie huu mkakati. Raisi Samia nakuhakikishia kwamba mji wowote uliopo kando ya bahari haupaswi kuwa na mafuriko kama tunayoona Dar. Au mwambie Prof. Tibaijuka asimamie hili.

Tatizo lililop kwako Samia ni kuteua watu ambao wanaona kipao mbele cha Dar ni kushughulika na changudoa na maandamano ya Chadema badala ya matatizo yanayoathiri wananchi na taifa kwa ujumla kwa kiwango cha juu sana. Unapewa sifa kila siku katika mambo ambayo ni routine sana, usiridhike au kudanganywa na hizo sifa. Kutoa hela za kujenga Zahanati na nini sijui sio sifa za kuwa raisi mzuri. Kwanza wengine tunaona hilo ni uongozi mbovu tu, kwa sababau pesa hizo zinapaswa kutolewa kupitia mipango ya maendeleo na bajeti za maeneo hayo. Kwa nini unakubali kuleweshwa na sifa za mambo yanayotakiwa kufanywa na wakuu wa mikoa na wakurgenzi wa miji na majiji? Fanya kazi za kitaifa tukusifie, sio mambo ya vijijini, wilayani na mikoani. Hiyo sio ligi yako.

Bado hatuoni unayofanya katika mambo makubwa ambayo yataacha legacy yako, pamoja na hili la mafuriko Dar. Japo tunaelewa ni suala la majiji haya matatu, Ilala, Kindondoni na Temeke, lakini lichukue sura ya kitaifa ili kuwe na coordination rahisi.
Haya ondokeni mara Moja,msije kusema sijawaambia.

View: https://twitter.com/eastafricatv/status/1749039265562902695?t=o9basEQ1rdLdu2xWTPd6qA&s=19
 
Ni serikali ya kijinga sana na kipumbavu itakayotoa tamko kama hilo na itarajie wananchi watekeleze kwa hiari. Serikali inawajibika kuhamisha na kufidia watu kwa kuwa walipojenga hawakujenga ndani ya siku moja, na serikali ilikuwapo ikiona wakifanya hivyo.

Wewe nenda leo kajenge kibanda nyuma ya ikulu uone kama utaanza hata kuchimba huo msingi.

Katika hali hi serikali lazima ikubali kulipia gharama za kuhamisha watu, kwa sababu ni kwa uzembe wa serikali watu wapo sehemu wazizotakiwa kujenga. Na zaidi, cummukatively, serikali inaingia gharama kubwa zaidi kusaidia watu maafa yanapotokea kuliko gharama ambayo ingetumika ikiwa wangekubali kuingia gharama ya kuwahamisha.

Mbona kama serikali tunakubali kulipia ujinga wa kuwalipa watu tuliowakatia mikataba yao? Lazima katika mausha uelewe kuna gharama za upumbavu na uzembe. Serikali ikubali kwamba watu kujenga maeneo hayo ni kwa sababu ya upumbavu na uzembe wake, na hivyi ina wajibu wa kuingia gharama kurekebisha hilo
Ndo ushenz ninaosema wa kuyaacha maisha yako mikononi mwa serikali,
Unaona kila mwaka unapata mafuriko, ila unaendelea kujenga huko huko,

Et unataka serikali ikulipe fidia, walai ningekua mm sikulipi,
Kingine unataka serikali itumie nguvu kuwahamisha, hao watu ni machizi hawaoni kinachotokea ?
Kipind cha mwanzon JK alikuwa analipa fidia watu wakawa wanachukulia kama mtaji, baadae akaacha
 
Wanapojenga serikali inakuwa wapi, imelala? Na utakuta wengi wana vibali vya serikali. Ndio maana tunasema bottom-line yote haya ni uzembe wa serikali, japo kuna 20% ya lawama kwa hao watu, na 20% kwa natural disasters
100% lawama kwa hao watu, kwa hio wao serikali ikisema kitu hawatumii akili ?
 
Back
Top Bottom