Asilimia 88 ya vijana (umri 30 - 35) hutegemea wazazi na mashemeji

Asilimia 88 ya vijana (umri 30 - 35) hutegemea wazazi na mashemeji

Katika kutathimini namna ambavyo kama taifa linapaswa kuwekeza kwenye elimu ya biashara (ujasiriamali) na ubunifu badala ya vijana kutegemea ajira za serikali, uchunguzi uliofanywa katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Mwanza & Kagera umegundua 88% ya vijana kati ya umri wa miaka 30 na 35 bado hutegemea kwa matumizi yao yote toka kwa wazazi ama Mashemeji zao.

Hii si dalili nzuri tunapoelekea kwenye nchi ya viwanda na kutimiza dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025 (Tanzania Vision 2025). Vijana amkeni fanyeni kazi, biashara, kilimo, acheni kubweteka na ku-bet kutwa nzima, kushangilia mipira ya ulaya na siasa za Marekani huku hamna namna ya kuingiza kipato binafsi zaid ya kutegemea mashemeji na wazazi kuwapa pesa ya matumizi.
========

Maoni ya WanaJF yamesomwa kwenye kipindi hiki cha JAMII LEO


*vijana acheni uvivuuuu

Vijana wa mikoa mitano hiyo katu haiwezi kutusemea vijana wa nchi hii, mkuu tutake radhi
 
Hao hao vijana ndio wanatajirisha makampuni ya Betting
 
Wanaambia wakajiajiri watoto wao wanawekwa kwenye vitengo nyeti, Tutafanyaje tutawalea mpaka tupate mafao tuwape mtaji.
 
Hongera Mkuu. Mm 2016/17 nilianzisha mahusiano na Divorced woman flan baada ya kunieleza matatizo yake pia nilivutiwa na umbo lake (wezere kama lote japo alikua na smell ya ajabu sana ila nilivumilia) basi akaomba nimlipie kodi nikaona why nilipe kodi wakati nina kwangu akahamia kwangu mwanae wa kiume alikuwa SAUT-Mwanza final year basi alipomaliza mqsomo Julia 2016 nikamtafuta kazi ofisini akawa analipwa 35,000 per day. Na hapo ofisi inatoa chakula na usafiri na home anakaa bure halipii chochote. Kafanya week 2 tu kaacha. Aisee kumuambia Mama yake anadai namnyanyasa mwanae kwa sababu mm si baba yake nilicholifanya nilienda kukodi kirikuu wakabeba vilivyo vyao hasa nguo na mapazia mm nikabaki huru nikihitaji nanunua tu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] khaaaaaaah weeeeeh hukuona hata aibu uwiiiiiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I'm 36yo bado niko kwa bimkubwa&mzee,and i'm proud of it,wengi wenu mnaongea hivyo 7bu ugumu maisha,hamna pa kwenda,nimejenga kwetu,naendelea kuishi kwetu....
 
Back
Top Bottom