Asilimia 90 ya watanzania tumeshagundua kwamba hawa viongozi wamehongwa kwa ajili ya bandari

Rushwa ni kitu kibaya sana na ndo kitu kinachoumiza hii nchi. Rushwa haifai hata kidogo.
 
Rushwa ni kitu kibaya sana na ndo kitu kinachoumiza hii nchi. Rushwa haifai hata kidogo.
Kwa kweli rushwa haifai. Si unaona baada ya kuwa Mbowe, NSHALLA, Lissu, Mwabukusi na Kitima wamepewa rushwa si waliharibu mjadala wa bandari na kuanza kuongelea uzanzibar wa rais na waziri Mbarawa na Uarabu wa akina DP WORLD mpaka watu wakahamia kwenye hayo mambo na hoja ya msingi ikaachwa? Rushwa ina madhara makubwa sana.
 
Tatizo kubwa la afrika na la miaka mingi ni wananchi wa kawaida kabisa kuwaamini wanasiasa na kuwapa kila chembe ya uelewa wao.

Wanawaamini kwa kutumia uzoefu wao walioupata kwa wachache kati yao na kudhani kwamba wanasiasa wote wana hulka moja ya ukweli mioyoni mwao.

Mpaka siku wakija kugundua kwamba wametapeliwa tayari wameshaumizwa. Suala la bandari haswa hiyo mikataba ni danganya toto ya wanasiasa, huwa wanavisoma vifungu viwili vitatu bila ya kuusoma mkataba mzima wenye vifungu 30.

Na hii ni janja ya hao hao wapigaji wa bandarini, kuwatumia watu wenye ushawishi na heshima miongoni mwetu ili eti tukizipinga hoja za hao wanazuoni ionekane kama vile ni dhambi ya mauti kwa nafasi zao mbele ya jamii!.

Hii ni vita nzito ya kiuchumi, wale wenye kuelewa nini anakuja kufanya DPW pale bandarini na katika uchumi kwa ujumla na tusikae kimya tukaacha upotoshaji wenye lengo la kuwalinda wapigaji ukaendelea kuheshimiwa na kukubalika.
 
Tumeshawashtukia hivyo kushindwa kwa hoja zao ni suala la muda tu.
 
wewe ndo unaakili au umeshikiwa
2008 Enyi misukule yetu tunawambieni Lowasa ni fisadi sasa andamaneni ili ajiuzulu, misukule mkaandamana kweli hadi Lowasa akajiuzulu.

2015 Lowasa akamwaga pesa...
Lowasa ni msafi na kamwe hakuwahi kuwa fisadi. Kwahiyo misukule yetu tunawaamrisha mumchague ili awe raisi wetu, na kweli siku ya kupiga kura ukamchagua Lowasa.

Sasa mpaka hapo unaweza kuona ni jinsi gani ulivyoshikiwa akili na wanasiasa uchwara. Unakubali vipi wanasiasa uchwara wakifanye kichwa chako ni chaka la kudanganyia na bado unaendelea kuwaona ni wakombozi kwako!!
 
Bora Mbowe na lisu wanajulikana wazi kuwa ni wanasiasa uchwara wanaoishi kwa njia za uongo uongo, rushwa nk.

Sasa Mwabukusi na wenzake si wanajiaibisha tu bure na hadhi yao inashuka.
 
Natamani wanaodanganywa na wanasiasa ili kuupinga mkataba wangepita hapa ili wajifunze kitu kupitia comment yako yenye hekima.
 
Huyo Mwabukusi ni mtu wa hovyo sana ndomana kadharauliwa na kila mwenye akili
WaTanganyika sio wajinga kama mnavyodhania! Waarabu wameshtuka hawataki tena kuja kupora Bandari zetu na sasa wanataka warudishiwe $$$ zao walizowahonga Samia na genge lake!!
Huo ndio mtihani alionao Samia kwani fedha walizohongwa wamezogawagawa kwa machawa wao hivyo hawajui watazirudishaje!
Ndio maana wanahangaika kuzunguka nchi nzima kuwarubuni wananchi ili hali waarabu wameshtuka wanataka warudishiwe hela zao!
 
Endelea kujitekenya na kuruka mwenyewe, wenye akili tunasubiri dp world waje kuanza kazi na wale wote waliokuwa wanatumia bandari yetu kupitishia madawa ya kulevya na kuja kuharibu nguvu kazi ya vijana wa kitanzania sasa watafute biashara zingine za halali wafanye.

Pia wale waliokuwa wanapitisha mizigo bandarini bila kulipa ushuru na kodi sasa kwisha habari zao. Wamejaribu kuwatumia wanasiasa uchwara na mawakili njaa wakifikiri labda serikali itawasikiliza. Kwa bahati serikali haina muda wa kuwasikiliza na wananchi ndo kabisa hatutaki kusikia porojo zao.

Wao waendelee kula hela za wakwepa kodi wa bandari ila wasifikiri kwamba serikali itaacha kuendelea na mipango yake na ukizingatia raisi Samia akiamua jambo huwa habadilishi. I hope unakumbuka swala la Loliondo ambapo Wakenya walitumia mamluki wao humu ila raisi hakurudi nyuma, operation ikaendelea kama kawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…