Asilimia kubwa ya Watanzania wanajua usafi wa mwili na mazingira yao ila wengi ni wachafu na wasio na kinyaa kabisa!

Wanaonishangaza zaidi ni wale wanaopigwa mswaki kwa kutumia maji ya kwenye ndoo ya kuogea ambayo hutumika pia kufulia nguo za ndani.
[emoji851] dah ila Kunaviumbe ni tatizo.Shule za bweni huu ndio mtindo wao hasa ukute boiz ndoo ya chooni,ya kuogea,ya kufulia soksi za kuchezea chandimu na mpaka boksa alafu mtu anaitumia kuifadhia maji ya kuswakia na kuoshea kolabo.Fangasi za mdomo aziishi
 
Umenena vema. Tunajenga vyoo mbali na nyumba kuu kwa kudhani kuwa choo ni dampo, maana hatuwezi kuvitunza kwa usafi. Kuna vyoo unaingia ukitoka harufu inakung'ang'ania kwenye nguo!
Kweli mkuu kuna bafu unaends kuoga unajiuliza nimekuja kuoga au kujipakaza uchafu wa bafuni
 
Hizo tabia wanatokanazo majumbani kwao na familia nyingi zinaishi hivi. Kikombe cha plastic kinaweza kabisa kutumika kwa kuswakia kama hakuna sinki bafuni ila watu hawajali na wanaona wako sahihi tu.
 
Binafsi najijua sio msafi na sina kinyaa.
Na hapo mengi sana umenigusa moja kwa moja, siku niliyokunywa supu ya utumbo pale mabibo sokoni ndio nikajua kudadeki zangu mm sio mdabliyusibii.

Ila nyie wenye kinyaa mna tabu sana hii nchi labda uwe na kibunda ila kama pangu pakavu utanuna kila siku.
 
Mkuu bora umeliona hili....! Mimi huwa napata tabu sana kuanzia nyumbani hadi mtaani nadhani watanzania tunaongoza kwa kutokua na kinyaa, hygiene iko chini sana...! Ila hilo tatizo sio tz pekee ni dunia nzima
 
Licha ya uchafu,Kuna watu Wana harufu za ajabu utafikiri kafungia panya kwenye shati.
 
Nlipokuwa advance karatu sec niliwahi kuwa domleader wa bweni linaitwa "MUONGOZO A"
Kuna tabia ilikithiri ya watu kuchafua vyoo hasa wanaokuja toka mabweninmengine tukafikia hatua bweni letu tukawa tunapiga kufuli then funguo moja wanakaa nao madogo wa form5 mwingine form6 na mwingn ninao mimi kiongozi...hivo kulikuwa na sehem wanatunza funguo zao ili uwe rahc mtu akija anachukua funguo anafungua hiyo iliongeza sana hali ya vyoo vya bweni letu kuwa safi sabb movement inakuwa ndogo na ustaarabu.

Sasa usiku kuanzia saa5 had saa1asubuhi muda wa usafi vyoo vinakuwa wazi maana wengi tunakuwa hostel haina haja ya kufunga mlango mkubwa.

Siku moja usiku naamka kwenda chooni namuona mshikaji tokea bweni la juu yetu ghorofan anakuja toilet nikajua kaja tu kukojoa asepe hakuwa na maji kwenye ndoo wala kichupa nikasem ngoja nimsikilizie sabb dumu letu la maji lilikuwa limeisha hivo ilitakiwa ukitak kujisaidia utoke nje ukachote maji na ndoo ndipo urudi.


Bas jamaa alikaa kam dakk5 hivi kaachia bonge la kimba alafu huyoo kasepa bas nikasem huyu simuachi bahati nzuri kuna madogo nao walikuwa wanatoka prepo wakanisapoti kumbananisha.

Jamaa alikuwa anasoma sayans form5 PCB alafu anafnya ujinga ule kutunza siri yake tukampa adhabu ya kutudekia vyoo vyetu na kujaza maji wiki nzima...

Putuuuuuuuu wabongo usafi bado sana yaan personal hygiene bado mnooo aseee yaan unakuta stend jengo zuri ila vyoo sifuri,unakuta mama ntilie anawateja kibao lakn hajali usafi kabisa yaan ni shida sana tunaishi kimazoea sana jaman.
 
Wabongo hawana kinyaa na malezi pia yanachangia.
 

Bado uchafu na uharibifu wao wanapojidhania hawaonekani mfano kwenye ma guest house, mabasi au kwenye maeneo ya umma.

Si nadra kukuta mtu kasokomeza ma big G, makamasi nk kusikopaswa kwa kuwa tu anadhani hayupo anayemwona.
 
Umenikumbusha.

Nimewahi kugundua uwepo wa kamasi katika maharage niliyoagiza na chapati kutoka kwa mama lishe. Nilimwambia na alimuuliza msichana wake ambaye alikiri kudondoshea kamasi lile kwenye maharage na hakulitoa.

Nimewahi kukuta mende mkubwa kwenye wali pale cafeteria ya ndani Mabibo Hostel.

Ila kuna hili: mama lishe wa Dar na Pwani huhifadhi ugali kwenye rambo, halafu lile rambo wanalidumbukiza kwenye ndoo ya plastiki, na ndoo ya plastiki inadumbukizwa kwenye sufuria yenye maji ndani kisha sufuria hiyo inawekwa jikoni kisha kuchochewa moto na kuchemka. Lengo ni kuufanya ugali usipoe.

Lingine, wakati wa kupika wali, badala ya kupalia mkaa, wanaweka mfuko wa rambo juu ya wali kisha wanafunika ili wali uive vizuri.

Wachemsha mahindi nao huyafunika mahindi yao na visalfeti(viroba) ili yaive vizuri.

Mifuko ya plastiki, ndoo na viroba huzalisha sumu pindi zinapopata moto, na sumu hii ni hatari kwa afya.

Lakini pia kuna mama lishe huweka panado kwenye nyama/kongoro ili nyama iive haraka na vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…