Asilimia kubwa ya Watanzania wanajua usafi wa mwili na mazingira yao ila wengi ni wachafu na wasio na kinyaa kabisa!

Asilimia kubwa ya Watanzania wanajua usafi wa mwili na mazingira yao ila wengi ni wachafu na wasio na kinyaa kabisa!

Kuna tabia ya kuchokonoa pua halafu anakupa mkono za saizi bwana kitambo sana wapi hivi upo saizi🤣🤣
Uchafu mtupu na hapo katoka toilet labda hakunawa mikono, au kapenga kwa mikono aaargh ndio maana sisalimii mtu kwa mkono aisee...
 
Nimewahi kufanya Kazi na waturuki nao wachafu Sana, kwanza hawaflashi uchafu wao, pili wanakula bila kunawa mikono

Kuna hii ishu ya kufunga vitafunio au samaki wa kukaanga ktk magazeti huu nao ni uchafu mwingine, watu wanshikashika magazeti na chafya zinapigwa humo kisha tunafungiwa vitu ambavyo tunaenda kula moja Kwa moja

Juzi nilienda kunywa chai kwa Mama lishe, daah anapiga chafya huku anasukuma chapati tena bila kujizuia Kwa namna yoyote ile, ikitokea hitajio la kula kwa mama lishe nimeapa sitoenda kwa yule madam mchafu
 
Kuchokonoa meno kwa njiti mbele ya watu ni uchafu mkubwa.
Mimi hata hamu ya kula huwa inakata mtu akichokonoa sehemu ya kula

[emoji817][emoji817]
Ustaarabu ni kuziba kwa kiganja.
 

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengi usafi wanaojua ni ule wa kuoga, kufua, kudeki na kufagia mazingira yanayozunguka nyumba zao na usipofanya haya jamii itakuwa mchafu na utasemwa tena sana lakini ni jamii hio hio isiyojali kabisa usafi wa kile kinachoingia mdomoni wala kuwa na kinyaa zaidi ya kinyaa cha kuona kinyesi tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kifupi asilimia kubwa ya watanzania hawajastaarabika kabisa.

Hivi mtu mzima unaanzaje kuchokonoa pua zako na vidole hadharani Kisha unaendelea tu mambo mengine bila kunawa mikono?? Hayo mambo kama ni lazima yalitakiwa yafanyike chooni kisha unawe mikono na sabuni. Kuna sababu kwanini kuna kioo pale kwenye sink la kunawia mkono.

Kutonawa mikono na sabuni baada ya kutumia bathroom iwe haja ndogo au kubwa.

Kutumia maji yanayokaa kwenye ndoo vyooni badala ya maji tiririka
 
Wanaonishangaza zaidi ni wale wanaopigwa mswaki kwa kutumia maji ya kwenye ndoo ya kuogea ambayo hutumika pia kufulia nguo za ndani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaa sana.
 
[emoji851] dah ila Kunaviumbe ni tatizo.Shule za bweni huu ndio mtindo wao hasa ukute boiz ndoo ya chooni,ya kuogea,ya kufulia soksi za kuchezea chandimu na mpaka boksa alafu mtu anaitumia kuifadhia maji ya kuswakia na kuoshea kolabo.Fangasi za mdomo aziishi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nlipokuwa advance karatu sec niliwahi kuwa domleader wa bweni linaitwa "MUONGOZO A"
Kuna tabia ilikithiri ya watu kuchafua vyoo hasa wanaokuja toka mabweninmengine tukafikia hatua bweni letu tukawa tunapiga kufuli then funguo moja wanakaa nao madogo wa form5 mwingine form6 na mwingn ninao mimi kiongozi...hivo kulikuwa na sehem wanatunza funguo zao ili uwe rahc mtu akija anachukua funguo anafungua hiyo iliongeza sana hali ya vyoo vya bweni letu kuwa safi sabb movement inakuwa ndogo na ustaarabu.

Sasa usiku kuanzia saa5 had saa1asubuhi muda wa usafi vyoo vinakuwa wazi maana wengi tunakuwa hostel haina haja ya kufunga mlango mkubwa.

Siku moja usiku naamka kwenda chooni namuona mshikaji tokea bweni la juu yetu ghorofan anakuja toilet nikajua kaja tu kukojoa asepe hakuwa na maji kwenye ndoo wala kichupa nikasem ngoja nimsikilizie sabb dumu letu la maji lilikuwa limeisha hivo ilitakiwa ukitak kujisaidia utoke nje ukachote maji na ndoo ndipo urudi.


Bas jamaa alikaa kam dakk5 hivi kaachia bonge la kimba alafu huyoo kasepa bas nikasem huyu simuachi bahati nzuri kuna madogo nao walikuwa wanatoka prepo wakanisapoti kumbananisha.

Jamaa alikuwa anasoma sayans form5 PCB alafu anafnya ujinga ule kutunza siri yake tukampa adhabu ya kutudekia vyoo vyetu na kujaza maji wiki nzima...

Putuuuuuuuu wabongo usafi bado sana yaan personal hygiene bado mnooo aseee yaan unakuta stend jengo zuri ila vyoo sifuri,unakuta mama ntilie anawateja kibao lakn hajali usafi kabisa yaan ni shida sana tunaishi kimazoea sana jaman.
"Putuuuuuuu" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haihitaji kufanya utafiti bali kutazama tu jinsi jamii inayokuzunguka inavyoishi katika suala zima la usafi hasa usafi wa kitu kinachoingia mdomoni mwako na jinsi jamii isivyojali kabisa.

Watanzania wengi usafi wanaojua ni ule wa kuoga, kufua, kudeki na kufagia mazingira yanayozunguka nyumba zao na usipofanya haya jamii itakuwa mchafu na utasemwa tena sana lakini ni jamii hio hio isiyojali kabisa usafi wa kile kinachoingia mdomoni wala kuwa na kinyaa zaidi ya kinyaa cha kuona kinyesi tu.

Nitaeleza hapa kwa kutaja mifano kadhaa na ambayo hata wewe msomaji ni shahidi mzuri tena bila shaka na wewe ukiwa ni mmoja wa watu wenye tabia hizo.

Table manners
Ukiacha mambo mengine yanayohusiana table manners kama kusali kabla ya kuanza kula, kukaa mezani, n.k, kuna hii tabia mbaya ya kuongea wakati wa kula. Hapa ndio watu hulisha mata huku hakuna anaejali kabisa. Mtu mdomoni umejaza chakula huku mnaongea na tena mmekaa karibu karibu na huoni hata watu wakishituka.

Kwenye mabaa wanakokula nyama choma na bia au kitimioto na bia, hawa ndio kabisa hulishana mate kuliko fisi wanaogombania mzogo poroni. Yaani mtu mdomni anatafuna nyama halafu anatupia kinywaji huku anaongea basi ni mnvua ya mate kwenda mbele ila cha ajabu watu wanafurahia tu kama hakuna kinachotokea.

Binafsi kama naenda bar, napenda kukaa meza ya peke yangu na wakija watu natafuta sababu nahama nawachia meza hasa nikiona ni kundi la wanywa pombe(walevi) maana mambo ya kurushiana mate mimi siyawezi.

Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni
Hili ndio tatizo kubwa miongoni mwa watanzania wengi na hii ni kwasababu hawana kinyaa. Unaweza kumuona mwanaume yuko smart kwelikweli au mwanadada mrembo sio kidogo ila akitoka chooni hana habari ya kunawa mikono na akinawa, basi ni mazingira yamemlazimisha kwa maana ya kuwa choo kipo sehemu ya public na akiingia au kutoka, anaonekana huku maji ya kunawa yakiwa nje ya choo hapo anakuwa hana ujanja vinginevyo hanawi.

Hata hivyo, unawaji wenyewe unaweza kuwa ni kichekeso kingine, kwani anafungua tu bomba ushahidi na kupitisha maji juu juu tena haraka haraka na sababuni anaweza asitumie kabisa hasa akiona hakuna anaemfuatilia halafu mkikutana mtaani anakupa mkono eti tusalimiane kumbe anakusambazai uchafu.

Ukitaka kuyaona haya,tembelea vyuoni (vyuo vikuu vikiwemo), nyumba za kupanga, kwenye nyumba za kupanga, vyoo vya njiani muwapo safarini, n.k.

Maajabu zaidi ni pale mtu huyo anatoka chooni anasuhuza mikono kisha anakamata tunda anakula na kama ni msichana wa kazi anaingia jikoni kwenda kupika au hata mama nyumbani anamtawaza mtoto kisha anasuhuza tu mikono na kuingia jikoni kuendelea na shughuli zake kama hakuna kilichotokea.

Kupiga chafya hadharani bila kuziba pua na mdomo
Hii tabia nayo ni moja ya kero kubwa sana miongoni mwa watanzania wengi. Mtu yuko sehemu ya public na amezungukwa na wenzake mfano ofisini, darasani, mezani,n.k ila anapiga chafya kama vile yuko pekee yake na wala hazibi pua wala mdomo. Cha kushangaza zaidi, katika watu kumi, unaweza kujikuta uko peke yako unaekereka wenzio wanaona sawa tu utadhani sio binadamu bali ni kikundi cha mifugo kama vile mbuzi, kondoo .n.k mmoja wao ndio kapiga chafya.

Kingine kinachokera ni tabia ya kupiga chafya kwa kutumia kiganja cha mkono badala ya kiwiko hivyo kusambaza uchafu kwa kila unaempa mkono au kwa kila anaetumia kifaa cha ku-share kama mouse, pen, n.k. Katika hili, pengine wa kulaumiwa zaidi ni yule mtu alieleta utamaduni wa kupiga chafya na kuziba pua na mdomo kwa kutumia kiganja na bila shaka hii tabia ilichangia sana kwenye kusambaza ugonjwa wa corona.

Kwa Mama Ntile na kwenye mighahawa

Hayo niliyoyaeleza hapo juu unaweza kuyaona na kuyadhibitisha katika sehemu wanzouza chakula kama vile kwa Mama Nile na kwenye mighahawa kwa ujumla.

Kwa mfano, ni kawaida kuona Mama Ntile anasukuma chapati kisha anapokea hela halafu anachukua chapati anakupatia au anasukuma chapati huko anakohoa (hakohilii pembeni) huku anaendelea kuhudumia huku wateja nao wakipiga nae strory wakiwa comfortable kabisa kama hakuna kinachotokea na wewe utaehoji, ukiondoka tu unapigwa jungu kwa unajifanya msafi, n.k.

Kwa kifupi, haya ni machache na hawa ndio watanzania ambao usipofua, usipofagia mazingira au kudeki nyumba hata kwa siku moja au mbili, watakusema kuwa wewe ni mchafu, ila hayo mengine kwao ni sehemu ya maisha na ukihoji utaambiwa unajifanya msafi (alietuloga kwa hakika alikuwa fundi).

Katika hili, tusisingizie umasikini au mazingira magumu wakati wengi hii ni hulka tu na ndio maana hata vyuo vikuu utayaona mambo kama haya hata kama mazingira kwenye mabweni, vyuoni na sehemu za kula ni rafiki kwa watu kunawa mikono kabla ya kula, baada ya kula na hata watokapo chooni.

Wasanii acheni kuimba nyimbo za mapenzi tu bali imbeni nyimbo za kukemea hizi tabia ila sijui itawezekana vipi kwa hili kutokea wakati wasanii wenyewe ni sehemu ya hiyo jamii.

Tuna safari ndefu sana.
CC: Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom