Asilimia kubwa ya watu wanaosali katika Kanisa hili naamini watakwenda mbinguni

Sasa, mkuu, kama unaona wazi matendo ya mapepo na ya mashetani kwanini unapata kigugumizi kuamini kwamba mbingu ipo? Shetani alikuwa malaika mkuu mbinguni. Alivyoasi akatupwa duniani pamoja na malaika walioasi. Hao ndio wanaoitwa mapepo.
Hakuna mapepo Wala mashetani je una ushahidi gani kuwa malaika waliasi mbinguni au umetoa kwenye vitabu vilivyo chapishwa na binadamu kama wewe
 
Leta andiko linaloonyesha yesu aliwahi kusali kanisani
Hujui kwamba Yesu yuko nasi hata ukamilifu wa dahari? Soma Mathayo 28:20.
Tunaposali Kanisani na Yesu yuko nasi. Ndio sababu kwa Jina lake mapepo yanatimka!
 
Maisha ya Waumini yakoje?
Kimwili,Maana kiroho umenena vyema.
 
Luk 10:25 .... "Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?" Kuisoma Biblia na kuiga mwenendo wa mitume haitoshi kukupa tiketi ya kuuona uso wa Baba, japo kufanya kinyume chake yaweza kukunyima nafasi hiyo.
Sura hii ina swali ambalo huwa nalipenda sana kulisikia "And who is my neighbour?"

Math: 6:1 na kuendelea, inatutahadharisha tusiwe kama Mafarisayo na wanafiki wengine, matendo yetu katika jamii ndo kila kitu, tusijilinganishe na hao, "Amini nawaambia, wamekwishakupata thawabu yao".

Kwahiyo hayo yote wanayafanya kwa kuzingatia maandiko, ni vema na haki. Lakini je, wanazingatia yale maelezo ya Mtakatifu Yakobo kuhusu dini safi? Je wanaishi vipi na jamii inayowazunguka, ama ndio wamekwishajiona wao wa mbinguni wanajihadhari wasienenda na wale wa mataifa.

Mat 5:46 "Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru je, nao hawafanyi hayohayo?". Katika sifa zote za hao waumini nimeona unazungumzia wanavyoshirikiana na washarika wenzao tu, inamaana jamii nzima wanayoishi ni ya waamini wenzao tu?
 
Hakuna mapepo Wala mashetani je una ushahidi gani kuwa malaika waliasi mbinguni au umetoa kwenye vitabu vilivyo chapishwa na binadamu kama wewe
Ukiacha Biblia unayoikataa, kuna ushahidi wa kihistoria (by secular historians kama Tacitus (AD 56 – 120) kuwa Yesu alikuwepo duniani.
Yesu mwenyewe alisema alimuona shetani akianguka kutoka mbinguni.
 
Ukiacha Biblia unayoikataa, kuna ushahidi wa kihistoria (by secular historians kama Tacitus (AD 56 – 120) kuwa Yesu alikuwepo duniani.
Yesu mwenyewe alisema alimuona shetani akianguka kutoka mbinguni.
Sio kweli 😀 😀 umeenda kule kule kwenye story za uwongo
 
Usiwe mwepesi wa kusema na kuhukumu. Sijasema kila kitu wanachofanya watu hao. Hayo uliyoyataja wanayafanya pia. Wanawajali hata watu ambao hawajaokoka ndio sababu wana ibada za maombezi kwa watu wote na hawawaambii wagonjwa na wenye shida kutoa kwanza sadaka kabla ya maombezi. Wanawajali pia yatima na wajane.
 
Sio kweli 😀 😀 umeenda kule kule kwenye story za uwongo
Duh, pole kama hukusoma somo la historia. Huyo Tacitus alikuwa mpagani kabisa. Aliandika historia ya Israeli bila msukumo wowote wa kidini.
 
Asante, basi tunawaombea wasimame imara katika imani, 1 Kor 16:13. Kama ulivyoelekeza ujumbe wa Kwaresma 2025 kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
 
Nimekata mtumishi, tuzidi kuombeana tuingie wote maana kubaki ni hasara sana.!
Amen. Tutaingia kwa neema yake.
Watakaobaki kwakweli nawahurumia. Hiyo dhiki kuu inayotajwa katika Ufunuo, loo, ni mapigo ya kutisha.
 
Hoja yako hasa ni Nini?
Hoja yangu ni kwamba huyo secular historian alithibitisha kwamba Yesu alikuwepo duniani. Na Yesu alipokuwa duniani alitaja habari za shetani na mbinguni. Kwahiyo ni kweli kwamba mbingu ipo.
 
Leta andiko linaloonyesha kuwa yesu aliwahi kusali kanisani
Mkuu, hujui historia ya Kanisa? Kanisa la kwanza lilianza wakati Yesu ameishapaa! Kabla ya hapo Yesu alikuwa akienda kwenye masinagogi.
 
Leta andiko linaloonyesha kuwa yesu aliwahi kusali kanisani
Kabla hajapaa aliweka msingi wa Kanisa
Mathayo 16:18
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
 
Maisha ya Waumini yakoje?
Kimwili,Maana kiroho umenena vyema.
Mbona nimesema pia ya kimwili, kwamba wanashirikiana kwa upendo katika misiba, arusi...
Au unamaanisha nini maisha ya kimwili
 
Mbona nimesema pia ya kimwili, kwamba wanashirikiana kwa upendo katika misiba, arusi...
Au unamaanisha nini maisha ya kimwili
Zaburi 1:3
[3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
Watu wengi waliookoka,wanafeli pakubwa kwenye kumiliki na kutawala,wanaridhika
1) Vitu vinyonge, kusomesha Watoto shule za kata, maono madogo katika kushiriki shughuli za uongozi wa Nchi/ maamuzi.biashara kubwa kubwa/ huduma kumilikiwa na wasioamini Kuliko walokole.( Kushirikiana katika Misiba/ harusi hata wasioamini wanafanya)
2) Umaskini Wana SEMA,Duniani tunapita tu.
3) Magonjwa wanasema mapenzi ya Mungu
 
Kwa hiyo wewe unafuatlia maisha yao hadi wanapotoka hapo kanisani!? Na mioyo yao unauwezo wa kuisoma!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…