Luk 10:25 .... "Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?" Kuisoma Biblia na kuiga mwenendo wa mitume haitoshi kukupa tiketi ya kuuona uso wa Baba, japo kufanya kinyume chake yaweza kukunyima nafasi hiyo.
Sura hii ina swali ambalo huwa nalipenda sana kulisikia "And who is my neighbour?"
Math: 6:1 na kuendelea, inatutahadharisha tusiwe kama Mafarisayo na wanafiki wengine, matendo yetu katika jamii ndo kila kitu, tusijilinganishe na hao, "Amini nawaambia, wamekwishakupata thawabu yao".
Kwahiyo hayo yote wanayafanya kwa kuzingatia maandiko, ni vema na haki. Lakini je, wanazingatia yale maelezo ya Mtakatifu Yakobo kuhusu dini safi? Je wanaishi vipi na jamii inayowazunguka, ama ndio wamekwishajiona wao wa mbinguni wanajihadhari wasienenda na wale wa mataifa.
Mat 5:46 "Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru je, nao hawafanyi hayohayo?". Katika sifa zote za hao waumini nimeona unazungumzia wanavyoshirikiana na washarika wenzao tu, inamaana jamii nzima wanayoishi ni ya waamini wenzao tu?