Asilimia kubwa ya watu wanaosali katika Kanisa hili naamini watakwenda mbinguni

Asilimia kubwa ya watu wanaosali katika Kanisa hili naamini watakwenda mbinguni

Exactly 💯
Hujamfikia C.S. Lewis. Huyo alikuwa professor wa Oxford Univ na Atheist wa viwango vya juu. Hatimaye akagundua amepotea njia, akawa Mkristo. Soma vitabu vyake.
 
Hujamfikia C.S. Lewis. Huyo alikuwa professor wa Oxford Univ na Atheist wa viwango vya juu. Hatimaye akagundua amepotea njia, akawa Mkristo. Soma vitabu vyake.
Unajua kwa Nini alifanya hivyo
 
Unajua kwa Nini alifanya hivyo
Soma vitabu vyake vitatu ameeleza kwa kina sababu. Sio huyo tu. Kuna Lee Strobel na Francis Collins. Hao wote walikuwa vigogo wa Atheism wakagundua wamepotea, wakawa Wakristo. Wewe una kipi cha kuwazidi hao? Onyesha vitabu ulivyoandika vya Atheism
 
Soma vitabu vyake vitatu ameeleza kwa kina sababu. Sio huyo tu. Kuna Lee Strobel na Francis Collins. Hao wote walikuwa vigogo wa Atheism wakagundua wamepotea, wakawa Wakristo. Wewe una kipi cha kuwazidi hao? Onyesha vitabu ulivyoandika vya Atheism
Mbona umeamisha mada sasa hao kama wameandika si wao
 
Mbona umeamisha mada sasa hao kama wameandika si wao
Maswali yako ndiyo yananihamisha. Kwa sababu huulizi kwa lengo la kutaka kujua bali kupinga tu. Sasa soma vitabu vya Lewis, upinge points zake hapa kisomi ili tujue unajua au hujui Atheism
 
Maswali yako ndiyo yananihamisha. Kwa sababu huulizi kwa lengo la kutaka kujua bali kupinga tu. Sasa soma vitabu vya Lewis, upinge points zake hapa kisomi ili tujue unajua au hujui Atheism
Bado haujathibitisha story zako
 
Ingekua kuna mbinguni, MTU mweupe asingekuletea dini ili uende sehemu nzuri
 
Bado haujathibitisha uwepo wa yesu naona unaendelea kuamisha mada
Nahamisha kwa sababu umeishaniambia wewe ni Atheist 100%.

Atheists dawa yao ni kuwakutanisha na waliokuwa Atheists wabobevu ndio wataelewana lugha vizuri.

Sasa wewe onyesha vitabu vyako au makala zako za Atheism tuone kama una points kumzidi Lewis.
 
Waswahili husema: "Tembea uone!" Ukikaa sehemu moja tu huwezi kujua yanayoendelea katika sehemu nyingine duniani.

Jamani kuna watu wako "serious" na mambo ya rohoni. Hivi majuzi, nilipata fursa ya kusali kwa siku kadhaa katika Kanisa fulani lililoko nchi moja isiyo na vurugu vurugu.

Kanisa hilo linaamini kwamba watakaoingia mbinguni, ni wale tu waliookoka na wanaoishi maisha ya utakatifu. Kwa sababu hiyo taratibu za ibada na mwenendo wa Watumishi na waumini, unafuata Maandiko bila kuchuja au kufuata mapokeo.

Kwa ufupi, wanafanya mambo yafuatayo:

1. Mtu akiokoka, anafundishwa haraka umuhimu wa ubatizo wa maji mengi na kisha anabatizwa katika maji mengi. Wanasimamia andiko la Yn 3:23 na Marko 10:38-39.

2. Washirika wote wanahimizwa kuomba ubatizo wa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha ili wawe na ujasiri wa kuwahubiri wengine Injili kama ilivyokuwa kwa mitume walipojazwa Roho Mtakatifu(Mdo 2:4).

3. Mchungaji wao sio mpenda makuu na anaishi maisha safi ya utakatifu. Ni mnyenyekevu lakini amejaa nguvu ya Roho Mtakatifu. Wana siku za maombezi kwa wote wenye shida. Mchungaji huyo anawaombea watu bure kwa Jina la Yesu sawasawa na Mt 10:8, bila kuwaambia wagonjwa na wenye shida watoe kwanza sadaka au wanunue chumvi na mafuta ya upako. Miujiza ya uponyaji inafanyika sana lakini Mchungaji hatukuzwi wala kusifiwa. Yeye mwenyewe anasema sifa zote apewe Yesu Kristo.

4. Wakati wa chakula cha Bwana au meza ya Bwana hawatumii mvinyo wala divai yenye kilevi kwa kuzingatia Maandiko mengi yanayokataza ulevi.

5. Ibada zao sio za Jumapili tu. Wana ibada nyingine katikati ya wiki kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu(Bible Study). Wanafanya hivyo kama Waberoya walivyofanya(Matendo 17:11).

6. Mchungaji wa Kanisa hilo anapohubiri, anasisitiza sana wokovu na maisha ya utakatifu(Ebr 12:14). Na anafundisha wazi kabisa kwamba mtu akifanya dhambi ya uzinzi, atatengwa na kukemewa mbele ya wote kama ilivyoandikwa katika 1 Tim 5:20.

7. Washirika wanavaa mavazi ya heshima na yenye kusitiri mwili kama Maandiko yanenavyo katika 1 Timotheo 2:9–10. Kina kaka hawana utani utani na mizaha na kinadada hata kwenye kwaya!

8. Washirika wanashirikiana sana kwa upendo kama ilivyokuwa wakati wa Kanisa la kwanza(Mdo 2:43-47). Nyakati za huzuni kama vile misiba au nyakati za furaha, mtu akifunga ndoa au akipata mtoto, washirika wanajihusisha sana na matukio hayo kama watoto wa baba mmoja!

9. Ibada zao ni za kusisimua. Wakati wa sifa kuna vigelegele na sauti kubwa za shangwe kama Daudi anavyohimiza katika Zab 33:1-3 na Zaburi 47:1. Wakati wa kuabudu, washirika wengi wanabubujikwa na machozi ya furaha!

10. Kuna siku wanakuwa na ibada za mikesha ya maombi. Wanafanya hivyo kwa kukumbuka jinsi Yesu alivyokuwa akikesha mlimani kwa maombi(Luka 6:12). Maombi yao ni ya nguvu. Akiingia Kanisani mtu mwenye pepo, pepo wanatoroka upesi! Kuna uwepo mkubwa wa Mungu.

Ukikutana na washirika wa Kanisa hilo utajua tu kwa haraka wameokoka kwa jinsi wanavyovaa na jinsi wanavyoongea. Usemi wao unawatambulisha(Mt 26:73). Wamejaa Neno!

Ukisali katika kanisa hilo unajisikia kabisa ufalme wa Mungu uko karibu na wewe!

Kwa ujumla naamini asilimia kubwa ya washirika wa Kanisa hilo watakwenda mbinguni. Kama na wewe una nia ya kufika mbinguni nakushauri utafute Kanisa la namna hiyo ujiunge nalo.

Chuma hunoa chuma(Mit 27:17).
Lakini inaonekana una matatizo
 
Exactly 💯
Kama kweli wewe ni Atheist 100%, basi inashangaza hujaweka mawazo yako kwenye maandishi au kitabu chochote, ili watu wayasome na kuyachambua. Maana hoja kubwa za watu waliopinga imani kama C.S. Lewis (aliyebadilika na kuwa Mkristo), Bertrand Russell, au Richard Dawkins, ziko kwenye maandishi yao. Hapo ndipo watu hujifunza, kujadili, na kupima uzito wa hoja. Kama hoja zako zina mashiko, kwa nini unazificha?
 
Hapo akili yako ina mskheri
Nimekuuliza hujaona👍
Hao walioweka dole baada ya kusoma nyuzi zangu, nao akili zao zina mushkeli? Ukikosa hoja afadhali ulale upate afya
 
Nimekuuliza hujaona👍
Hao walioweka dole baada ya kusoma nyuzi zangu, nao akili zao zina mushkeli? Ukikosa hoja afadhali ulale upate afya
Una matatizo si bure! Inafaa uonane na madaktari wa akili haraka. Moja ya kiashiria ni kupenda şifa. Kama Huniamini, subiri kama hutaanza kuokota makopo barabarani
 
Back
Top Bottom