DOKEZO Asilimia kubwa za Mahakama ili upate msaada au huduma lazima utoe RUSHWA

DOKEZO Asilimia kubwa za Mahakama ili upate msaada au huduma lazima utoe RUSHWA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

La MaGique

Member
Joined
Jan 12, 2016
Posts
66
Reaction score
54
WAkuu habari, Moja ya taasisi ambazo ni muhimu nchini ni MAHAKAMA ambazo kisheria zinawajibu wa kusimamia haki na Sheria.

Sambamba na Hilo raia wanategemea Kuona unafuu wa kupata haki/ huduma/msaada wa Haki zao ukitoka MAHAKAMANI, lakini katika Hali ya kawaida inavyotakiwa kuwa sivyo badala yake MAHAKAMA badaya ya kuwa msaada wa raia imekuwa tishio na chuma ulete kwa raia.

Kiufupi ni kwamba asilimia kubwa za MAHAKAMA ili upate msaada au huduma Lazima utoe RUSHWA ndipo upate huduma, nakumbuka nilikiwa na form Fulani karibu 12 na zote zilitakiwa kuwa na muhuri wa MAHAKAMA, kwanza picha linaanza mapokezi napokelewa na karani ananiita pembeni ananiuliza shida, nikamwambia, kisha akaniuliza "Si unajua utaratibu wa kuonana na mkuu"? Nikasema ndiyo, nilijua ni kufuata foleni kumbe sivyo, basi nilikuwa mtu wa poli kufika hapo MAHAKAMANI baada ya kusubiri kwa muda walionitangulia nikaona hata waliokuja badala yangu wanaingia na kutoka.

Nikamfuata yule bwana nikamuuliza mbona mi siingii mapitwa na watu waliokuja nyuma yangu, akasema sijafuata taratibu, nikamuliza taratibu zipo, akasema si unataka kugongewa muhuri, nikasema ndiyo, akanambia unatakiwa kulipa 10k kulingana karatasi zinazotakiwa, maana yake 120k kwa fomu zote.

Nikajua anatania, baada ya muda wakatoka lunch nikamfuata Hakimu nikiwa na zile fomu, nikamweleza akanambia onana na Karani akupe utaratibu nikasema tayari, akamuita karani akamuuliza kama tumemalizana karani akasema Bado sijakamilisha, yule Hakimu akanambia hawezi kungonga muhuri bila wino kwa hivyo hakukuwa na wino siku hiyo pale mahakani, akanambia wakipata wino nitawsiliana na karani 😀

Basi ile siku nimeshinda njaa alafu nikarudi home bila bila, baadaye nikampigia karani akasema niandae nusu ya pesa ataniombea kwa Hakimu, yaani karani ananiomnea kwa Hakimu ili nipate huduma🤣🤣 halafu yeye binafsi nimpe 20k kwa kunisaidia kuniunganisha na Hakimu, nikaona mambo yasiwe mengi maana pia nilikuwa na uhitaji wa haraka na zile fomu, nikampa hizo Hela bana, baada ya kufanya Hilo zoezi huwezi amini dk 5 nyingi swala likaisha.

Maswali yalikuwa mengi kama unavyojiuliza wewe lkn sikuwa na mbadala,,,,,,,kwahiyo mahakimu wanapiga Hela kupitia migambo waliopo MAHAKAMANI na hao makarani wao, maana wenyewe hawapokei hizo pesa mkononi, nilichoka sana mpaka leo🤐
 
Sasa mbona unasema kwa sauti kubwa?
Utasababisha wasitusaidie tena.
Unajua hako karushwa wanakochukua hao mahakimu ni kiduchu sana kuliko ukienda kulipa kihalali kwenye ofisi za mawakili?
 
Miaka yote tafiti zinaonesha Mahakama na Polisi ndiyo wakali wa hizo kazi.

Makarani ni miungu watu kwenye korido za mahakama,waliatamia hundi za mgao wa mirathi kidogo ziishe muda kisa visenti vya chai tu.
 
Back
Top Bottom