Askari amshushisa dereva matusi na kipigo, Ni vipi tunaweza kujitetea na uonevu bila hofu ya kuuliwa, kubambikiwa kesi za madawa, ugaidi, n.k

Askari amshushisa dereva matusi na kipigo, Ni vipi tunaweza kujitetea na uonevu bila hofu ya kuuliwa, kubambikiwa kesi za madawa, ugaidi, n.k

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Cheo kinapopewa kwa mtu ambae sio muadilifu huwa ni janga kwa wananchi.

Baadhi (sio wote) ya ma askari hutumia cheo hiki kunyanyasa raia, mfano anaweza kukupora mali yako, anaweza kukataa kukurudishia ulichomkopa, anaweza kukupiga, n.k.

Ukijaribu kujitetea kwa askar ambae sio muadilifu kitendo hiki kinampa hasira na kukukomoa kwa kukushushia kipigo, kukubambikia madawa ya kulevya, anaweza kukuua kabisa kwa kusingizia wewe gaidi, n.k.

Inakuwa ngumu mtu kujitetea hasa ukiangalia ana familia inayomtegemea, akienda hata lokapu siku 2 tu familia inadhhofika, sasa akienda jela vipi?

Sasa ni vipi tunaweza kujilinda?

Hii ni video ya mda kidogo ila ni mfano wa uonezi ambao bado upo,

Video hii ni ya tukio la mwaka 2016​
 
we nae bhana, li video la zamaaan ulikuaga hujanunua smartphone au
Maada kuu ni jinsi ya kujilinda na huu uonezi, hio video ni mfano tu na hata iwe ya zamani bado haiondoi maumivu kwa huyo muhanga.
 
Enzi zangu ningekua lockup au mochwari. Kweli umri unaleta utulivu na ustahimilivu.

Askari wetu Wana stress sana. Niliwahi leta varangati Oyster bay police sitaki kumbuka hiyo siku.
 
Kuna Jamaa yangu mmoja alikataa kuonewa akaamua kupimana nguvu na Popoo, Jamaa alikuwa vizuri alimtandika Afande za kutosha sema wenzake wakaja fasta wakaanza kumchangia Jamaa kisha wakamsweka ndani na vitisho vya kufa Mtu..

Ni bahati tu Jamaa alikuwa ana connection huko juu na alikuwa Mtu mwenye umate mate, ingawa walihakikisha analala ndani ila siku inayofuata akatoka.

Ila ni risk maana wakikuweka kwenye 18 yao wote wanakuwa dhidi yako utakoma.
 
asee unipige nakurudishia!!
mi sio dandara asee.

Muda mwingine pia hadi upigwe kuna kosa kubwa umefanya.

Usikute jamaa kwenye zebra kidogo agonge denti asee
 
kuna siku niliwakalisha askar watano na mmoja akiwa na bunduki, ilikua show kama ya dakika 5. Hawa ndugu zetu sometimes wana kausengerema.
 
Kuna Jamaa yangu mmoja alikataa kuonewa walipimana nguvu na Popoo, Jamaa alikuwa vizuri alimtandika za kutosha sema wenzake wakaja fasta Jamaa wakamchangia na wakamsweka ndani.

Ni bahati tu Jamaa alikuwa ana connection huko juu, ingawa walihakikisha analala ndani siku inayofuata ndio akatoka.

Ila ni risk maana wakikuweka kwenye 18 yao wote wanakuwa dhidi yako utakoma.
Sababu ya authority ambayo wanayo,sasa huo ni upuuzi,means ukigombana na hawa wapuuzi,they can do anything.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom