mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
Karibu kila Kijana Tanzania ana historia mbaya na chafu na askari wetu. Huyu alichukuliwa clip bila kujijua baada ya kumbambikia mtu kete za bange na kudai rushwa ya 2 mil na walipewa laki 6 wakamuachia mtuhumiwa.
Mkasa kama unavyosimuliwa na mhanga Emmanuel Mwita
Jana usiku maaskari wa Oysterbay bila Uniform na mmoja akiwa kavaa uniform huku akiwa amevaa sweta juu (pichani chini) walinivamia kwenye gari wakasema nina bangi.Baada ya mabishano wakanipeleka nyuma ya kituo cha Oysterbay wakaniwekea kete 14 kwenye dashboard na kisha
Kunilazimisha niwape milioni 2 ili mambo yaishe. Nilipokataa wakaniweka ndani hadi mdada niliekuwa nae alipowapa laki 6 ndio wakaniachia bila sharti lolote. Nataka kusema ule ni uonevu mkubwa na ujambazi mnafanyia raia.
Ninawatambua askari wote waliohusika na ningependa haki itendeke,Niliwaomba wanifungulie kesi na kunipeleka mahakamani wakagoma na zaidi walinipiga na kunilazimisha nisizungumze Baada ya kupewa pesa na kuniachia waliniomba yaishe na tusameheani kwani walikasilishwa na mdomo wangu
Waliniteka maeneo ya Coco beach (WAVUVI KEMPU) majira ya saa nane usiku. Hata hivyo sitoshangaa kama tanpol hamtochukua hatua. Natarajia kwenda kwenye ofisi za afande Jumanne Mlilo ambaye nilimpigia simu bila mafanikio kesho majira ya saa nne asubuhi kutoa malalamiko yangu.
Msigwa Gerson nilikupigia simu kwa namba (0717 214 838) bila mafanikio. Waziri Mkuu
Askari wako wanaonea raia. Kweli nimeamini jeshi letu linabambikia watu kesi na kutisha watu wake na kuteka watu wake.
Ajabu ni kwamba waliziweka(Bangi) wao na mwisho wa siku walizichukua ili wakamfanyie mwingine mambo hayo. Hii kitu tusipoikemea itawaumiza wengi.