Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nipe namba yako nikupigie uniwekee hizo bangi tuoneshane makali.ujasiri huo unao sababu upo nyuma ya keyboard.
Kwa Askari Polisi, matikio kama haya ni ya kawaida sana, kila siku yanatokea hapa nchini.Karibu kila Kijana Tanzania ana historia mbaya na chafu na askari wetu. Huyu alichukuliwa clip bila kujijua baada ya kumbambikia mtu kete za bange na kudai rushwa ya 2 mil na walipewa laki 6 wakamuachia mtuhumiwa.
View attachment 2670145
Mkasa kama unavyosimuliwa na mhanga Emmanuel Mwita
Jana usiku maaskari wa Oysterbay bila Uniform na mmoja akiwa kavaa uniform huku akiwa amevaa sweta juu (pichani chini) walinivamia kwenye gari wakasema nina bangi.Baada ya mabishano wakanipeleka nyuma ya kituo cha Oysterbay wakaniwekea kete 14 kwenye dashboard na kisha
Kunilazimisha niwape milioni 2 ili mambo yaishe. Nilipokataa wakaniweka ndani hadi mdada niliekuwa nae alipowapa laki 6 ndio wakaniachia bila sharti lolote. Nataka kusema ule ni uonevu mkubwa na ujambazi mnafanyia raia.
Ninawatambua askari wote waliohusika na ningependa haki itendeke,Niliwaomba wanifungulie kesi na kunipeleka mahakamani wakagoma na zaidi walinipiga na kunilazimisha nisizungumze Baada ya kupewa pesa na kuniachia waliniomba yaishe na tusameheani kwani walikasilishwa na mdomo wangu
Waliniteka maeneo ya Coco beach (WAVUVI KEMPU) majira ya saa nane usiku. Hata hivyo sitoshangaa kama tanpol hamtochukua hatua. Natarajia kwenda kwenye ofisi za afande Jumanne Mlilo ambaye nilimpigia simu bila mafanikio kesho majira ya saa nne asubuhi kutoa malalamiko yangu.
Msigwa Gerson nilikupigia simu kwa namba (0717 214 838) bila mafanikio. Waziri Mkuu
Askari wako wanaonea raia. Kweli nimeamini jeshi letu linabambikia watu kesi na kutisha watu wake na kuteka watu wake.
Ajabu ni kwamba waliziweka(Bangi) wao na mwisho wa siku walizichukua ili wakamfanyie mwingine mambo hayo. Hii kitu tusipoikemea itawaumiza wengi.
Unasemaje?????????All in all, TanPol wanafanya kazi nzuri sana.
Kuna wachafu wachache ila kiujumla jamaa wanafanya kazi nzuri sana.Unasemaje?????????
Ama kweli wewe ni WAKALA WA SHETANI, mmefanana kwa majina na sifa/sifa na hao unaowatetea kwamba wanafanya kazi nzuri sana.
Tanzania yatakiwa iwekeze kwa askari wake, wote wanunuliwe body cam kila aliye kazini azivae.
Gari zote za doria ziwe na kamera zinazofamya kazi muda wote
Mahabusu zote ziwe na kamera
Vituo vyote viwe na kamera
Polisi kazi yao kubwa kuiweka ccm madarakani hata waue mtu hawanaga kesi haohuyo ni tapeli anayetumia jeshi la polisi kufanya huo ujinga.
Ifike mahali sasa serikali itambulishe chombo mahalumu ambacho kitakuwa kinaoversees hivi vyombo vya ulinzi na usalama kama havitendi haki watu wakatoe ripoti huko ili na wao washughulikiwe ipasavyo..