Askari anayedaiwa kutembea na kete za bangi kubambikia watu

Askari wa Oysterbay wengi ni majizi na majambazi na wanatamaa sana ya maisha mazuri. Wakipimwa nyutu wengi watakutwa hawana marinda

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
hawa si ndo HASHIM alisemaa naooo hawaa....!!
 
Polisi ni wachache sana wana ubinadamu...
Mi niliwahi kutoa ushauri.... Ukidakwa na polisi kuwa mpole na ujifanye mjinga..
Kuna watu wamefungwa kwa makosa ambayo hawajatenda...

Polisi anaweza kukupa kesi yoyote ile na akatengeneza ushahidi ukanyooka kwa hakimu ukafungwa hata miaka 10..

Ushauri kwa hali za polisi wetu ni bora kuwa mpole na kama unachochote we toa hela.. Ukijidai unajua sheria wanakupeleka kituoni na wanakushikisha silaha unaambiwa toa maelezo tumekudaka nayo ukijiandaa kufanya ujambazi
 
Nawajua polisi, nawajua wadau wa Usalama katika Taifa la Tanzania nauliza ni kweli Huyu polisi anae zunguka tweter amemwekea raia madawa ya kulevya?

Yaani Rais wa nchi anakemea madawa ya kulevya kumbe Kuna polisi wanayo?

Ushauri

Tulio ishi pale ostabey na sarenda tunajua michezo inayo chezwa polisi je mnataka tuwaumbue?

Mkuu wa polisi ingia hapa na fungua dm utaenjoy.
 
Huyu jamaa ndiye anaweza kwenda kuandamana kwa sababu ana ujasiri, ameona litakalo kuwa na liwe. Tungekuwa sisi Watanzania wengine waoga ingekuwa imeishatoka hiyo!

Mapolisi msiishi kwa mazoea kwamba Watanzania wote ni waoga, wapo majasiri mtaumbuka!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Askari Polisi, matikio kama haya ni ya kawaida sana, kila siku yanatokea hapa nchini.
Mimi nilishatoa Mapendekezo kwamba kwa hatua iliyofikia mapaka sasa na kutokana na namna ya utendaji wao, Jeshi la Polisi Tz pamoja na TISS, yanatakiwa maamuzi magumu sana kufanyika kwa kuyavunja yote kabisa na Kisha kuanza kuyaunda tena upya kabisa kuanzia tangu mwanzo. Wayendaji karibu wote waliooo sasa wanatakiwa kuyupwa nje, isipokuwa wale wachache sana ambao itathibitika baada ya uxhunguzi wa kina kufanyika kwa kila mmoja. Karibu wote hawafai kuendelea kuwa waajiriwa ktk hizo taasisi, waondolewe wote na kuajiriwa wapya wenye mawazo na mtizamo mpya, wazalendo wa kweli na waadilifu wa kweli, wenye sifa stahiki.
Aidha, kuwepo na mabadiliko ya Sheria, Kanuni na taratibu nzuri za uendeshaji wa taasisi hizo.
 
ulilazimika kutoa tsh 600k kwa sababu gani wakati unaamini na una uhakika kosa hujatenda!!!!

wewe ni mhalifu pia,maana umeibariki rushwa kwa kutoa badala ya kusimama upande wa haki.
 
Leo nimesimamishwa na ma-idiot wawili traffic.
Wakaniambia tairi langu lime-expire, nikawauliza kivipi? Wanasema lina zaidi ya miaka 4 hivyo tuna kuandika fine. Nikawakatalia nakuzozana nao kwa muda. Baadae traffic mmoja akaniambia ingia kwenye Gari tuyajenge.
Baada ya kuingia kwenye Gari akaniambia nimpe hela .
If those idiots are reading this, I want to tell them that, I have spared them for today, but next time I shall fix them.
 
Binafsi mm ningekataa na ningewaambia nyie ni sio polisi ni matapeli. Kama kweli ni polisi wanipeleke kituoni, at least hapo ningehoji uhalali wa kuniomba hiyo hela ni wa nn kama kweli nimetenda kosa.
Isije ikawa umetapeliwa na watoto wa mjini ndugu mtanzania!??!
 
Hawana akili ndio maana wanakufa masikini na ukimwi, me ndio maana nikisikia wameuwawa huwa nafurahi sana
 
Tanzania yatakiwa iwekeze kwa askari wake, wote wanunuliwe body cam kila aliye kazini azivae.
Gari zote za doria ziwe na kamera zinazofamya kazi muda wote

Mahabusu zote ziwe na kamera

Vituo vyote viwe na kamera

Naunga mkono hoja
 
Polisi kazi yao kubwa kuiweka ccm madarakani hata waue mtu hawanaga kesi hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…